Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya Dengu (Dengue fever)
Updated at: 2024-05-25 10:35:15 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ugonjwa wa dengue ni tishio la ugonjwa hatari linaongezeka siku hadi siku. Dengue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoenezwa na mbu aitwae aedes.
Ugonjwa huu huenea zaidi msimu wa nvua. Huchukua siku 3-14 kwa mgonjwa kuonyesha dalili za dengue. Dalili kuu za dengue huwa ni maumivu makali ya kichwa, mgongo pia kutokwa na damu maeneo ya wazi kama puani maskioni (Hasa watoto) .
Siku zote kinga ni bora kuliko tiba hivyo huna budi kufanya yafuatayo kujikinga na ugonjwa hatari wa dengue:
1. Epuka Kuvaa nguo fupi kama kaptura, shati au tisheti kata mikono. Vaa suruali na shati/sweta la mikono mirefu 2. Usiweke Makopo chini ya Viyoyozi kwani hudondosha maji yanayoweza kuwavutia mbu. 3. Maji ya kwenye makopo ya maua yabadilishwe mara kwa mara. 4. Epuka Kuanika nguo Mbichi ndani ya nyumba. Hii huwavuta mbu kuzaliana 5. Osha vyombo visivyotumika angalau mara moja kwa wiki. 6. ondoa madimbwi yoyote yanayotuwamisha maji. 7. Tumia chandarua unapolala nyakati za mchana. 8. Funika makopo ya taka ili kutowavutia mbu. 9. Kunywa maji mengi na jenga mazoea ya kunywa juice za matunda. 10. Usiache milango wala madirisha wazi bila sababu ya msingi.
Updated at: 2024-05-25 10:35:20 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mayai ni kitu kilichozoeleka na kinachopatikana kwa gharama nafuu. Kutokana na kuzoeleka huku watu wengi wamekuwa wakipuuza umuhimu au nafasi ya mayai katika afya zao. Pengine kupuuza huku kunatokana na mazoea au ukosefu wa elimu juu ya faida zinazopatikana kutokana na ulaji wa mayai.
Zifuatazo ndizo faida za kula mayai wakati wa kifungua kinywa;
Hutunza shibe
Protini zilizoko ndani ya mayai hukufanya kutohisi njaa mapema. Ina maana kuwa ukila mayai unaweza kukaa muda marefu zaidi bila kula ikilinganishwa na mikate au vyakula vingine vya ngano.
Husaidia ukuaji wa ubongo na uwezo wa kumbukumbu
Kirutubisho kinachojulikana kama “Choline” kinachopatikana kwenye mayai ni muhimu katika ukuaji na maendeleo ya ubongo. Pia kinahusishwa katika kuongeza uwezo wa ubongo wa kutunza kumbukumbu.
Hulinda macho
Kemikali za leutin na zeaxanthin zinazopatikana kwenye mayai zinaaminika kulinda macho dhidi ya madhara ya mionzi mibaya. Pia inaaminika kuwa zinazuia kutokea kwa tatizo la mtoto wa jicho uzeeni.
Husaidia kupunguza uzito
Ulaji wa mayai husadia kupunguza uzito wa mwili. Utafiti uliofanyika umeonyesha kuwa watu wanaokula mayai wamefanikiwa kupunguza uzito wa miili yao kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na wasiokula.
Mayai ni bei rahisi
Ukilinganisha na vyakula vingine vya protini kama vile nyama, mayai ni bei rahisi zaidi. Hivyo basi, mayai yanaweza kupatikana na kuandaliwa kwa urahisi wakati wa kifungua kinywa kuliko vyakula vingine.
Mayai ni chanzo kikubwa cha protini
Kama nilivyotangulia kusema kuwa mayai yana kiasi kikubwa cha protini kinachohitajika katika kujenga miili yetu. Hivyo basi ni vyema kula mayai asubuhi wakati wa kifungua kinywa ili kujipatia virutubisho hivi.
Kumbuka hili ni sawa na kusema kuwa amino asidi zote muhimu tunazozihitaji katika mlo zinapatikana kwenye mayai.
Mayai hayaongezi lehemu (Cholesterol)
Ni dhahiri kuwa mayai yana kiwango fulani cha lehemu. Lakini utafiti uliofanyika hivi karibuni umebaini kuwa lehemu iliyoko katika mayai inapoliwa haina athari kwenye kiwango cha lehemu kwenye damu. Hivyo hakuna haja ya kuhofu juu ya magonjwa ya moyo yatokanayo na lehemu.
Kumbuka afya yako ni muhimu sana. Jali afya yako kwa kuzingatia ulaji bora wenye tija. Kumbuka kuwa huwezi kuwa na tija katika shughuli zako bila kuwa na afya njema. Badili mtazamo wako leo; tafuta mayai na ule kwa ajili ya afya yako.
PROSTATE GLAND (TEZI DUME) TATIZO SUGU KWA WANAUME
Updated at: 2024-05-25 10:37:49 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
-Hii ni tezi ya wanaume yenye sifa zifuatazo. ~Ina umbo km yai(oval shape) ~Ina ukubwa wenye vipimo hivi, upana 4cm na unene 3cm ingawaje hivi vipimo vinatofautiana kwa kila mwanaume. ~Tezi hii ipo inazunguka shingo ya kibofu cha mkojo na kuzunguka mrija unaopeleka mkojo nje(urethra) ~Tezi hii hua yenye ukubwa wa kawaida lakini huongezeka ukubwa kadri ya umri. ~Tezi hii hutengeneza majimaji yenye rutuba ya mbegu za kiume(shahawa)
SEHEMU KUU ZA TEZI YA KIUME
1.PERIPHERAL ZONE(SEHEMU YA NJE) ~Hii ni sehemu ya nje ya tezi ambayo madakari wengi hutumia hii tezi kubaina kama kuna tatizo kwenye tezi kwani ni virahisi kiugusa km daktari akiingiza ikiingiza index fingure(kidole cha kusontea) kwenye njia ya haja kubwa. Kukua kwa sehemu hii hakuwezi kuathiri utokaji wa mkojo. 2. TRANSITIONAL ZONE(SEHEMU YA KATI) ~ Hii ni sehemu ya tezi ambayo ikikua yani ikiongezeka ukubwa tunasema KUVIMBA KWA TEZI TUME kitalamu BENIGN PROSTATIC HYPERPLASIA (BPH) kuna uwezekano mkubwa wa tezi dume iliyovimba kuzuia njia ya mkojo kupita. Kwani ndio sehemu ya tezi iliyo karibu kabisa na njia ya mkojo. Mara nyingi hii sehemu ikikua ndio inayo sababisha matatizo ya kukojoa(obstructive symptoms). Tezi hii pia daktari anaweza kuibaini kwa kutumia kidole kipomo hiki huitwa DIGITAL RECTAL EXAMINATION(DRE) hii ni kwa sababu ikikua inasukuma ile sehemu ya pembezoni yani peripheral zone kuelekea njia ya haja kubwa. Hivyo dakatri anaweza kubaini km tezi imekua au laa. 3. CENTRAL ZONE(SEHEMU YA KATI) ~Hii sehemu iko mbele ya transitional zone hivyo uvimbe katika sehemu hii ni vigumu kubaini kipitia kipimo hiki cha haraka cha kutumia kidole hivyo tunatumia vipomo vya picha kinaitwa CYTOSCOPY. Hiki ni kipimo cha picha kinacho angalia kipofu cha mkojo na njia ya mkojo na kutoa majibu katika mfumo ya picha au video.
KUKUA KWA TEZI YA KIUME ~Kukua kwa tezi ya kiume kitalamu tunaita BENIGN PROSTATIC HYPERPLASIA (BPH). Hili tatizo mara nyingi huanza baada ya miaka 40 hivi na dalili huja kujionesha uzeeni. Hivyo tezi inaweza ikawa kubwa sana lakini haina dalili hii ni kutokana na sehemu gani ya tezi iliyovimba au kuongezeka. Tezi inapoonesha dalili jua tatizo hilo ni sugu na liko ktk hali mbaya.
DALILI ZA KUVIMBA KWA TEZI 1. Kukojoa mara kwa mara 2. Kubakiza mkojo kwenye kibofu 3. Kukujoa sana usiku 4. Maumivu wakati wa kukojoa 5.Kupungukiwa nguvu za kiume 6. UTI ya mara kwa mara 7. Mawe kwenye kibofu kutokana na mrundikano wa mkojo. 8. Figo kujaa maji. Hii sababu mkojo huo unarudi nyuma kuelekea figo(hydronephrosis) 9. Kupoteza fahamu(uremia) HIZI DALILI NIMEZITAJA KULINGANA NA TATIZO LINAVYOKUWA SUGU KWA MGONJWA HIVYO UGONJWA HUU NI HATARI USIPO WAHI.
JINSI YA KUBAINI KUVIMBA KWA TEZI ~Kumbuka BPH sio kansa ni uvimbe tu wa kawaida wa tezi lkn kumbuka tezi hii inaweza kuvimba pia kutokana na kansa ya tezi dume (prostate cancer) 1. Uchunguzi wa kawaida kwa kutumia kidole kupitia njia ya haja kubwa kuangalia kama tezi ina tatizo. Kipimo hiki huitwa DIGITAL RECTAL EXAMINATION. Baada ya kipimo hicho daktari huandika alicho kigusa kama ni ugonjwa au iko kawaida. 2. Hiki ni kipimo cha kupiga picha kibofu cha mkojo kinaitwa CYTOSCOPE. Kumbuka kipimo hiki una ingiziwa waya flani wenye tochi mbele kwenye njia ya mkojo huku huo waya umeunga nishwa kwenye screen. Hivyo chochote huo waya utakacho murika kitaonekana kwenye screen. Ubaya wa hiki kipimo ni kwamba kinaweza kuumiza kuta za njia ya mkojo na baada ya wiki km mbili njia inaweza kuziba mbili jeraha linapo pona. Ila ni kipimo kizuri sana. 3. Kipimo kingine kinaitwa RECTAL UTRASOUND hiki ni kipimo cha kupiga picha kupitia njia ya haja kubwa (rectal) na kutoa picha kwenye jarida gumu kumsaidia daktari kusoma. 4. Kipimo cha kutofautisha kati ya uvimbe wa kawaida(BPH) na kansa ya kipofu(PROSTATE CANCER) Kipimo hiki kinaitwa PROSTATIC SPECIFIC ANTIGEN. Hii ni protein inatolea kwa wingi endapo kuna kansa ya tezi dume. Hivyo damu ya mgonjwa itachukuliwa na kupekwa maabala kuchunguza km ni nyingi kupita kiasi kwenye damu. Kama hii protein ipo kawaida basi uvimbe huo sio kansa ni BPH. Lakini km kiwango ni kingi uvimbe huo ni KANSA. Hivyo uchunguzi zaidi unahitajika kama kuchukua sample ya kinyama kutoka katika tezi na kupeleka maabala.
MATIBABU YA KUKUA KWA TEZI DUME
1. Tezi dume kama haina dalili zozote mara nyingi waga haishighulikiwi sana hospitali lakini dawa za kupunguza kasi anaweza pewa mgonjwa. Lakink ni mara chache. 2. Kama tezi imesha anza kuleta dalili kama usumbufu wakati wa kukojoa siku hizi kuna operation ya bila kukata inaitwa TRANSURETHRAL RECTIONING OF PROSTATE AU CHANNEL TURP. Hii operation inafanywa kama akiwa anafanya kipimo cha CYSTOSCOPE. Lakini hapa anaweka wire mbele kiko chamviringo kinapitishwa njia ya mkojo kina enda kukata kinyama kinachoziba i mean tezi iliyovimba. Hapa inazibua njia ya mkojo ili mtu akojoe. Ukifanyiwa operation hii vizuri tezi hujirudia baada ya miaka kama 3-5 tangu siku ya operation. MADHARA YA TIBA HII 1. Kukosa uwezo wa kufikia kishindo yani hutoi shahawa(RETROGRADE EJACULATION) wazee wengi hulalamika sana baada ya hii operation hivyo ushauri nasaha lazima utolewe ili mgonjwa ajue nini madhara yake kabla ya operation. 2. Kuziba kwa njia ya mkojo kutoka na kuumia kwa njia hizo wakati wa kitendo hicho. Panapokua panapona hilo kovu linaziba njia ya mkojo. 3. Operation kubwa ya kuondoa tezi hio hufanyika kwa kufungua kibofu cha mkojo na kutoa hio tezi. Madhara ni mengi sana kuhusu hii bora ile no mbili. Kama unahisi unatatizo ili nione mapema kabla mambo aya jakuwa makubwa zaidi
Updated at: 2024-05-25 10:35:12 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kufanya Masaji kuna faida hizi zifuatazo;
Masaji uongeza kinga ya mwili
Masaji kushuka kwa homoni inayohusika na kupunguza maambukizi mbalimbali homoni ijulikanayo kama ‘cytokines’ vile vile masaji inashusha homoni inayohusika na matendo ya mashari homoni ijulikanayo kama ‘cortisol’.
Kufanya masaji hakukufanyi ujisikie ni mtulivu peke yake, bali pia kunaweza kukuongezea kinga yako ya mwili.
Masaji ya dakika 45 kwa siku imethibitika kuongeza uwingi wa seli nyeupe za damu (lymphocytes) ambazo ndizo hupigana dhidi ya vijidudu nyemelezi vya magonjwa mbalimbali mwilini.
Kufanya masaji huondoa tatizo la kukosa usingizi
Tafiti nyingi zinasema masaji inao uwezo wa kuamsha mawimbi ndani ya ubongo yanayohusiana na kutengenezwa kwa usingizi mzito (delta waves) na hii ndiyo sababu kwanini wengine hupitiwa na usingizi mzito mara tu baada ya mazoezi ya masaji.
Tatizo la kukosa usingizi linaweza kutibika kwa kufanya masaji tu kwakuwa masaji husaidia kupunguza uchovu na kuongeza uwezo wa kupata usingizi mtulivu kwa watu wa rika zote yaani watoto wadogo mpaka wazee ikihusisha wale wenye matatizo ya akili, kansa na magonjwa ya moyo, machache kati ya magonjwa mengi yawezayo kutibika kwa masaji tu.
Kuondoa mfadhaiko wa akili au Stress
Masaji huondoa hamaki na maumivu huku yakiongeza uwezo wa kupata usingizi mzuri na wa uhakika.
Masaji huondoa huzuni
Watafiti wanasema kuwa masaji kuongezeka homoni ijulikanayo kama ‘oxytocin’ na kupungua kwa homoni nyingine iitwayo ‘adrenocorticotropin’.
Oxytocin inahusika na matendo ya huruma, maono, upendo na ushirikiano wa kijamii. Wakati adrenocorticotropin yenyewe huhusika na kupungua kwa mfadhaiko (stress) moja kwa moja.
Kuondoa maumivu mbalimbali mwilini
Masaji hupunguza maumivu hasa ya mgongo na maumivu ya kichwa na maumivu ya kwenye mishipa.
Kutibu shinikizo la chini la damu kwa kutumia maji chumvi
Updated at: 2024-05-25 10:35:34 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kunywa Maji yenye chumvi husaidia kutibu shinikizo la chini la damu sababu sodiamu iliyomo kwenye chumvi hupandisha juu shinikizo la damu. Usizidishe dawa hii kwa sababu chumvi nyingi kuzidi ina madhara kiafya.
Matumizi:
Changanya nusu kijiko cha chai cha chumvi ndani ya maji glasi moja (robo lita) na unywe mchanganyiko huu mara 1 au 2 kwa siku