Log in to access your menu with tools for managing ๐ tasks, ๐ฅ clients, ๐ฐ finances, ๐ learning, ๐ personal growth, and ๐ spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Mapishi ya Chai ya maziwa, mandazi, uyoga na mayai
Updated at: 2024-05-25 10:22:58 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mandazi (angalia jinsi ya kupika katika recipe ya mandazi ya nyuma) Uyoga (mashroom kikombe 1 cha chai) Mayai (eggs 4) Hoho (greenpepper 1/4 ya hoho) Nyanya (fresh tomato 1) Kitunguu (onion 1/4 ya kitunguu) Chumvi (salt) Mafuta (vegetable oil) Hiliki nzima (cardamon 4) Masala ya chai (tea masala 1 kijiko cha chai) Pilipili mtama iliyosagwa (ground black pepper 1/4 ya kijiko cha chai) Maziwa (fresh milk 1 kikombe cha chai) Majani ya chai (tea leaves) Maji kiasi. Sukari (sugar)
Matayarisho
Jinsi ya kupika chai, weka maziwa, maji kiasi,hiliki, masala ya chai, pilipili mtama na majani katika sufuria. Chemsha kwa muda wa dakika 10 na chai itakuwa tayari. Jinsi ya kupika mayai, weka mafuta kiasi katika fry pan na utie vitunguu, vikaange kidogo kisha tia nyanya, chumvi na hoho. Pika kwa muda wa dakika 4 kisha tia mayai na uyaache yaive mpaka yakauke kisha geuza upande wa pili na uyapike mpaka ya ive kisha ipua. Jinsi ya kupika uyoga, weka mafuta kidogo katika fry pan kisha tia uyoga na chumvi na ukaange mpaka uive katika moto wa wastani. Ukisha iva breakfast yako itakuwa teyari kwa kuseviwa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:04 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa dengu (gram flour 1/4 kilo) Kitunguu kilichokatwa (onion 2) Hoho (green pepper 1/2) Pilipili iliokatwakatwa (scotch bonnet pepper 1/2) Barking powder (1/4 ya kijiko cha chai) Chumvi (salt) Kitunguu swaum (garlic cloves 2) Mafuta ya kukaangia (vegetable oil) Binzari manjano (turmeric 1/4 ya kijiko cha chai)
Matayarisho
Changanya unga, chumvi, binzari, barking powder kwanza kisha weka maji kiasi na vitu vyote vilivyobakia (isipokuwa mafuta) na ukoroge vizuri kuhakikisha unga hauna madonge.Hakikisha unga hauwi mzito wala mwepesi sana. Kisha uache kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo choma bagia katika mafuta. Ukiwa unachoma hakikisha bagia zinakuja juu ya mafuta na hazigandi chini. Ikitokea zinaganda chini hapo itakuwa umekosea kitu. Pika mpaka ziwe za light brown kisha zitowe na uziweke katika kitchen towel ili zikauke mafuta na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:53 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga 2 Vikombe
Samli au shortening ya mboga 2 Vijiko vya supu
Maziwa ยพ Kikombe
Iliki Kiasi
Mafuta ya kukarangia Kiasi
Shira
Sukari 1 Kikombe
Maji ยพ Kikombe
Vanila ยฝ Kijiko cha chai
Zafarani (ukipenda) Kiasi
Jinsi ya kupika na kuandaa
Katika kisufuria pasha moto maziwa na wakati huo huo chemsha Samli katika kisufuria kengine. Tia unga katika bakuli na iliki, kisha mimina samli iliyochemka na huku unachanganya, kisha tia maziwa na uwendele kuchanganya vizuri isiwe na madonge, ikiwa maziwa haitoshi ongeza maji kidogo. Kisha uwache unga ukae mahali pa joto kwa muda wa dakika 10 hivi. Halafu fanya viduara vidogo vidogo, kisha finyiza kwenye greta yenye vishimo vidogo ili upate umbo kama kwenye picha. Kisha karanga kwenye mafuta yaliyopata moto hadi vibadilike rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. Chemsha shira, ikiwa tayari mimina visheti na upepete na kuzichanganya zipate shira kote. Weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa na kahawa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:11 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Mchele - 3 vikombe
Nyama ya kusaga - 1 LB
Mchanganyiko wa Nafaka upendazo; maharagwe, njegere, mbaazi n.k 1 mug
Vitunguu maji kata vipande vipande - 3 vya kiasi
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi - 2 vijiko vya supu
Mafuta - ยฝ Kikombe
Mchanganyiko wa bizari (Garam Masala) - 2 vijiko vya chai
Vipande vya supu (Maggi cubes) - 3
Maji (inategemea mchele) - 5
Chumvi - Kiasi
MAPISHI
Osha mchele na roweka. Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitunguu mpaka viwe brown. Tia Thomu na tangawizi, kaanga kidogo. Weka nyama ya kusaga, chumvi na garam masala, endelea kukaanga mpaka nyama iwive. Mwaga maji yaliomo katika kopo la nafaka na utie nafaka pekee humo. Tia maji na vipande vya supu (Maggi cubes) huku unavivuruga, koroga kidogo. Tia mchele, koroga kidogo. Funika na pika kwa moto mdogo mpaka karibu na kukauka ukikorogoka kidogo. (kama unavyopika pilau ya kawaida) *Epua uipike katika moto wa oven 350-400 Deg kwa muda wa dakika 15. *Kama sufuria uliyotumia sio ya kupikia katika oven, mimina katika chombo chochote kinachotumika kwa oven kama bakuli la pyrex au treya za foil. Pakua katika sahani na iko tayari kuliwa.