Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Jamaa alikuwa anagombana na mkewe,hatimae
akamwambia kwa ukali
"Unajua nimechoka sasa, haya kusanya nguo
zako naβ¦β¦..
Updated at: 2024-05-25 18:06:32 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa alikuwa anagombana na mkewe,hatimae
akamwambia kwa ukali
"Unajua nimechoka sasa, haya kusanya nguo
zako naβ¦β¦..
Kabla hajamalizia sentensi simu
ya mkewe ikaita, kumbe alikuwa ni baba yake.
Basi mzee akaanza kuongea na binti yake huku
jamaa anasikia
"Aisee mwanangu nimebahatika kuuza ile
nyumba yangu sasa nimeona niwatumie milioni
20 mjaribu kuanzisha mradi na mwenzio.
Haya mwambie yeye nitampigia kesho kama
ana mradi mwingine nimpe hela kidogo".Baada
ya simu kukatwa mke akamgeukia jamaa
akamuuliza,"eeenhee!!! ulikuwa unasema
umenichoka nikusanye nguo zangu halafu
iweje? Jamaa kwa upole akajibu "Nilikuwa
nasema ukusanye nguo zako na unipe nifue".
Updated at: 2024-05-25 18:10:22 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mama mdaku alishangaa kila siku mchungaji anaingia nyumba ya jirani yake ambaye hana mume, akawa anajiuliza anakwenda kufanya nini? Uzalendo ukamshinda akamuuliza "Mwenzangu, mbona kila siku mchungaji anakuja kwako, vipi anakuja kukuombea?" Akajibiwa "Nyoo, umbea tu! Mbona kwako kila siku anakuja mwanajeshi kuna vita! chefuuuu π³π³π³π³π³
Updated at: 2024-05-25 17:02:15 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Et jamaa kawekwa jela kwa kosa la kupoteza mamiilion.ya kampun akiwa gerezan babayake alituma barua Ikisema yan.mwanangu tumapata shida maana shamba halijalimwa na jatujii litalimwaje na msimu ndio huo nataman.ungekuwepo ningepata msaada wa kulimiwa hili shamba
Yule kijana alijibu tafadhal baba usilime hilo shamba maana pesa zote nilizo ibwa nimeficha.huko
Kwakuwa barua zote laxima zipite kwa mkuu wa gereza ndio xiende kwa muhusika kesho yake mzee alikuwa shamba lote limelimwaa na polisi
Akatuma ujumbe tena yule kijana Nashukulu umepata msaada sasa nazan unaweza ukaendelea kupanda mazao shamban.kwetuπππππ
Jamaa aliamua kumtoa demu wake out kwaajili ya chakula cha usiku kufika hotelini wakakaa mezani mhudumu akaja,
Mhudumu: kaka nikuhudumie nini,
Jamaa: afathal NILETEE MENU LISTI
Updated at: 2024-05-25 18:03:52 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa aliamua kumtoa demu wake out kwaajili ya chakula cha usiku kufika hotelini wakakaa mezani mhudumu akaja,
Mhudumu: kaka nikuhudumie nini,
Jamaa: afathal NILETEE MENU LISTI
Mhudumu: dada na wewe?
Demu akajibu kwa pozi tena kwakujishaua, "NA MIMI NILETEE MENU LIST ILA USIWEKE CHUMVI NYINGI"
Chezea mbulula weweβ¦!!!
Updated at: 2024-05-25 17:56:35 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mfalme Sulemani alikuwa na wake 700 na alichepuka(cheated)na vimada 300 . Mpenzi wako/Mume wako unamfumania na kimada mmoja tu ugomvi na amani imapotea ndani ya nyumba,unasimulia kuanzia padri,mchungaji,ukoo wako mzima,mashoga, stress,vidonda vya tumbo,inapelekea mpaka unaokoka,eti kisa kamuonjesha mmojaβ sasa akionjesha 700 si utakutwa MirembeοΏ½
Updated at: 2024-05-25 17:09:19 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nimefumaniwa hapa na jamaa ameniambia nitulie tuyamalize kishikaji, yaani nisijali sasa ametoka nje nasikia ananoa kisu nadhani anataka anichinjie kuku!
Hii mitoto mingine mijinga, cheki alichokifanya huyu
Updated at: 2024-05-25 17:07:59 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nimeamka asubuhi nikiwa na elfu 1 tu mfukoni, nikamtuma mtoto wa jirani akaninunulie maandazi nipate kunywa chai. Baada ya muda namuona anarudi huku analamba askrimu ya AZAM kama Simba vile. Nikamuuliza maandazi yako wapi? Akanijibu eti wakati anafika yanapouzwa maandazi akagundua kuwa kapoteza hela yangu, hivyo akaanza kurudi, ila bahati nzuri wakati anarudi ili kuja kunitaarifu kuhusu kupotea kwa hela yangu, njiani akaokota elfu 1 ambayo kuna mtu alipoteza ndio akaamua kununua askrimuβ¦.kwa sasa niko polisi na mtoto yuko dispensari na mamakeπππππππ