Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 17:54:01 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Usije ukaenda kwa mganga, mwenzako yamenikuta, yani masharti niliyopewa, acha tu, yalikua hivi:-
1.Jasho la nyoka. 2.Manyoya ya mende. 3.Sisimizi Shoga. 4.Mbwa mjane. 5.Kuku aliye single. 6.Samaki mwenye miaka miwili bila kuoga 7.Mti wenye ujauzito. 8.Mbavu za Nzi. 9.Nywele za Kiroboto. 10.Mwanya wa Mbu. Duuh..!! mwanangu kwa hali hii mbona itakula kwako. Wengine wanasemaga IGA UFE! Rizik anagawa Mungu tu shetan simuelew!
Kilichotokea kati ya mkaka na mdada walipokutana hotelini
Mkaka aliingia kwenye hoteli moja akaketi meza moja na mdada mrembo maarufu sana; MKAKA: Samahani dada sijui saa ngapi? MDADA: Nani kakwambia saa yangu ndio ya kuangalia kila mtu?
Updated at: 2024-05-25 18:08:53 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mkaka aliingia kwenye hoteli moja akaketi meza moja na mdada mrembo maarufu sana; MKAKA: Samahani dada sijui saa ngapi? MDADA: Nani kakwambia saa yangu ndio ya kuangalia kila mtu?
MKAKA: Samahani sanaβ¦.jamaa akachukua Galaxy yake akapiga simuβ¦.aise saa ngapi saa hizi? mi ndio nimeingia toka USA nataka kurekibisha saa yangu ifwate muda wa huku. Na wewe uwahi kuchukua iPad nimekuja nazo tatu tu za zawadi. Halafu ntafutie mtoto mzuri nimumwagie midola niliyokuja nayo, ok ciao tuonane badae. MDADA: Kaka samahani saa hizi ni saaβ¦.. MKAKA: Achana na mimi wewe
Updated at: 2024-05-25 17:09:46 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo nimechoka zangu alafu shangazi amekuja anataka nimuunganishe facebook. Imebidi nimwambie lazima awe na picha passport size 4 kwaajili ya kuweka profile picture, barua kutoka kwa afisa mtendaji na Atm card ya nmb bank. Alafu awe na marefa wanne ambao wamekuwa facebook for more than 3 years. Amesema hataki tena kujiunga fb!
ππππππππππππππ Saa ivi niko zangu nimelala naendelea kupunguza uchovu
Updated at: 2024-05-25 17:17:06 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
01.π Wale wanafunzi walioongoza Mashuleni, wanaenda kwenye Engineering na Medical school.
02.π Wale waliokuwa wa pili, wanachukua MBA na LLB na kuja kuwa Mameneja wa wanafunzi walioshika nafasi ya kwanza. 03.π Wale waliokuwa wa tatu, wanageukia Siasa na kuwaongoza wote hapo juu. Yaani wa kwanza na wa pili. 04.π Wale waliofeli, wanaenda Jeshi, hawa wakigoma, basi hao wa juu wote hawana raha. 05.π Wale waliopata Zero na waliokataa shule wanakuwa waganga wa kienyeji, wote hapo juu watamtafuta huyu, pale mambo yao yanapokwenda kombo. Tuache kudharauliana, kila mtu ni boss akiwa kwenye nafasi yake. πππππππππππππππ
Updated at: 2024-05-25 18:09:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
FUNDISHO : SAFARI NI SAFARI
Maisha ni ya ajabu sana, wakati mwingine maisha ni mazuri na mwingine ni mabaya, katika maisha yetu tumeshapitia safari nyingi sana na za aina mbalimbali kwa nyakati mbalimbali. Lakin kiukweli kila safari ni safari tuu.
Japokua kila safari ina changamoto zake lakini mwisho wake ni ule ule , kila safari ina uzuri na upekee wake.
Vile vile kila safari ina ubaya wake, kwa mfano kila safari ina gharama yake kulingana na upekee wake.
Usiwe na wasiwasi na mashaka na aina ya safari ulionayo, jipe moyo utaimaliza na kupata ulichokitarajia. Haya ndio maisha na wote tunatakiwa tuyafurahie.
Ingawa kila mtu ana safari yake bado wote tunatakiwa tufurahie pamoja kwa safari tuliyo nayo. Hata Uwe Na safar ya aina gani wewe furahi tuu. Hii ni kwa sababu safari mwisho wake ni mmoja kwa wote burudani ni ile ile
SafariπΊ ni safari πΊhata kama ni ya chupa au ya kopo mwisho wake π€π€
Updated at: 2024-05-25 16:57:53 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ukimchoka mkeo, waweza kumtaftia sababu za kumuacha kama hizi
_ 1. Missed calls 16? Umeua betri la simu yangu. Kwa hiyo hata mimi unaweza kuniuaβ¦ It's Over!!! _ 2. Hata hunieshimu. Mi naongea na wewe lakini we upo bize unavuta pumzi? It's over! _ 3. Nimekupigia umepokea simu hapohapo. Huna subira. Itβs over!! _
4. Nilikwambia huwa napenda chakula cha moto lakini hujanipashia ice cream. Hunijali. It's over! _ 5. Nimekupa mayai mawili, moja uchemshe jingine ukaange. We umekaanga ambalo ulitakiwa kuchemsha na umechemsha ulilotakiwa kukaanga. Huniheshimu, Itβs over! _ 6. Nimekuita DARLING na wewe ukaniita HONEY. Yani kwa maana nyingine unamuita mama yangu NYUKI. Huheshimu wazazi wangu, fungasha kilicho chako. its over.