Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Angalia sababu ya mwanamme kubadili jina na Kuitwa jina la kike, hii dunia ina mambo kweli
Updated at: 2024-05-25 17:00:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Rashidi alimpa ujauzito mwanafunzi, akashtakiwa. Kumbe Rashidi ana bibi yake mtaalamu wa yale mambo yao ya Sumbawanga, akampachika Rashidi i jinsia ya kike.
Alipofika mahakamani kuhojiwa Rashidi akasema sijampa ujauzito kwa sababu mimi pia nina jinsia ya kike. Kwa kuthibitisha Rashid wakaenda kumkagua basi akashinda kesi, kufika nyumbani Rashid akawakuta watu wamejaa wanalia, akauliza kulikoni? Akaambiwa bibi yako amefariki. 😭😭😭😭😭😭😰😰😰😆😆😆😆😆😆 Kwa sasa Rashid anaitwa Leila😀😀😀
Updated at: 2024-05-25 17:46:22 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mtalii: Do you have vegetables here. Mtafsiri: Mnavyo vijimeza hapa. Waiter: Vijimeza vidogo hatuna. Mtafsiri: No sir, they don't have. Mtalii: OK, fine, do you have hot dogs. Mtafsiri: Sawa, je mnao mbwa wa moto. Waiter: Loh! Bwana we, hatupiki mbwa hapa. Mtafsiri: They don't cook here Mtalii: What type of snacks do you have here. Mtafsiri: Aina ngapi ya nyoka mnao hapa, Waiter: We bwana we hapa hatupiki aina yeyote ya nyoka, mwache akale nyumbani kwao. Mtafsiri: They don't cook any type of snacks here, maybe you can go back and eat at home. Mtalii: OK, at least give us a cocktail juice. Mtafsiri: OK, tupatie hata juisi ya mkia wa jogoo. Waiter: Hebu tokeni na bangi zenu hapa, tena sasa hivi kabla sijakasirika. Mtafsiri: Lets get out of here 😝😝😝😂😂😂 Usicheke pekeyako
Updated at: 2024-05-25 17:13:37 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mama alichukuwa simu akampa mwanawe. Mama..Mpigie babako mwambie chakula tayari. (Mtoto akachukuwa na kupiga) Mtoto…Mama simu ya baba imepokelewa na mwanamke. (Mama kwa hasira) Akirud atanitambua leo. (Baada ya muda kidogo baba akarud,kufika mlangon tu kapokewa na sufuria ya kichwa. Hajakaa vzur mwiko wa pua) Mama..Mwanangu ulipopiga simu ya babako mwanamke wake alisemaje?? Mtoto..Alisema mteja unaempigia hapatikan kwa sasa…..
Angalia kilichojiri katika semina ya wanandoa kuhusu upendo
Updated at: 2024-05-25 18:00:09 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kulikuwa na semina ya wanawake kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa. Mwalimu aliwauliza ni wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono kama ishara ya kuwa wanawapenda waume zao. Mwalimu akauliza tena, “Ni lini mara ya mwisho umemwambia mumeo “Nakupenda Mpenzi”?
Majibu yalikuwa kama ifuatavyo: Wengine wakisema Asubuhi ya leo, Wengine jana, Wengine wiki iliyopita Wengine mwezi uliopita Na wengine wakasema hawakumbuki! Mwalimu aliwapa kazi kila mwanasemina achukue simu yake na kumtumia mume wake meseji yenye neno “NAKUPENDA MPENZI” Baada ya meseji kwenda aliwaamuru kubadilishana simu kila mtu na jirani yake. Kila mwanasemina aliambiwa kusoma meseji za majibu kwenye simu aliyoshika
Simu ya 1 – “Samahani, nani mwenzangu”! Simu ya 2 – “Samahani, wrong number”! Simu ya 3 – “Si nimekuambia usinitumie messages kwenye namba hii”! Simu ya 4 – “Mh! leo mvua itanyesha”! Simu ya 5 – “Nikija tutaongea zaidi”! Simu ya 6 – “……Imedhibitishwa umepokea Tsh300,000 kutoka kwa ……”! Simu ya 7 – “Me too”! Simu ya 6 – “Huu ujumbe ndio ulikuwa unamtumia huyo hawara yako ee, leo utanikoma”!
Updated at: 2024-05-25 17:05:08 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo nikaamua niingie misa ya asubuhi kwenye kanisa moja la kilokole kulikua na ugeni wa mchungaji kutoka Bulgaria, Mahubiri yameanza saa 1 asubuhi hali ikawa kama hivi:
MCHUNGAJI: My name is Pastor Livingstone MKALIMANi: Kwa jina naitwa mchungaji Jiwe linaloishi MCHUNGAJI: We thank God for All goals we set by our hands MKALIMANI: Tunamshukuru Mungu kwa Magoli yote tuliyoweka kwa Mkono
Hivi navyoongea kanisa halina viti waumini wote tumekimbia nje naona Mkalimani amebaki na kiatu cha kushoto tu. Sunday joke
Cha kufanya msichana akikukimbia halafu atake kukurudia
Updated at: 2024-05-25 17:05:23 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
……… Kama msichana atakutupa kwa sababu huna pesa, na baadaye unapopata pesa akarudi tena kuomba msamaha… Ndugu yangu….. Msamehe…. Mpe ahadi ya ndoa, mwambie utamuoa…. iambie familia yake unataka kufanya ukarabati wa nyumba yao…… Ondoa paa lote la nyumba yao halafu TOWEKA…..