Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 16:53:24 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
HAHAHAHAHAAAAAA DUH TAMAA MBAYA
Muokota makopo katika uokotaji wake wa makopo akaona chupa ambayo ndani kuna ki2, alipoifungua likatoka jitu la ajabu. Huku akitetemeka lile jitu likamwambia kijana asante sana kwa kuniokoa omba vi2 viwili sasa hivi. Kijana kwa hofu akaomba pesa za kumiliki magari na majumba ya kifahari. Ghafla fuko la hela na pete ya bahati vikadondoka. Akaambiwa ombi la pili,akasema nibadilishe niwe kivutio ili nipendwe sana nakina dada Hapohapo akageuzwa akawa chipsi yai.!!ππ€£π€£π€£
Padri Akimbia wakati wa kuungamisha, chanzo ni hiki
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani
peke yake.
Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa
pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama
{confess}
"Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya
dhambi kubwa sana."
Padri, "Endeleaβ¦"
Updated at: 2023-04-29 22:53:14 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani peke yake. Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama {confess} "Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana." Padri, "Endeleaβ¦"
"Bosi wangu aliniita nyumbani kwake, akaniambia amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema nisipozitoa atanipeleka polisi, sa kwa ukweli mi naogopa kufungwa. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu,nikatoa bastola nikamuuaβ¦.. Yesu atanisamehe?"
Padri: "Utasamehewa." "Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa kutazama, Loh! Mke wa bosi, alipoona kilichotokea akasema anapiga polisi simu. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye pia⦠Yesu atanisamehe hilo?" Padri: "Utasamehewa."
Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke, lakini mlinzi akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuuaβ¦.. Yesu atanisamehe?" Padri:"Utasamehewa."
"Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi, nikawaza mambo gani tena, akasema alirudi nyumbani na kukuta yaliyotokea akanionesha diary ya babake, inayoonesha nilikuwa na appointment naye wakati nilipomuua. Nikamuuliza nani mwingine anayejua? Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi.
Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke yetu, nikamuuaβ¦.. Yesu atanisamehe na hilo?"
Kimyaaβ¦. "Padri yesu atanisamehe?" kimyaβ¦.
Jamaa akatazama kwenye confession booth padri hayupo, lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.
Jamaa, "Sasa baba mbona umekimbia?" Padri kwa taabu akajibu, "Nilitazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetuβ¦β¦."
Updated at: 2024-05-25 17:59:16 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Huwa naenjoy sana kusoma yaliyoandikwa nyuma ya daladala hasa ninapokuwa kwenye foleni. Misemo maarufu ya kwenye daladala.
1.Yatima hadeki 2.Utamu wa chips mimba 3.Ukitaka kujua ugumu wa kudai kopesha ukweni 4. Usiyempenda kaja 5. Kobe hapimwi joto 6. Acha kazi uone kaz kupata kaz 7. Ukichezea koki utalowa 8. Heshima pesa kipara kovu tu! 9. Mtumbwi hauna saitmira. 9. Silaha pesa bastola mzigo 10. Hata uoge mjini huendi 11. Chezea mshahara usichezee kazi. 12. Ukiona manyoya ujue kishaliwa 13. Ikisimama Panda 14. Pombe pombe tuu kunywea bar mbwebwe 15. Njia ya chooni haioti nyasi 16. Likizo ya maskini ugonjwa 17. When i grow up i want to be a scania 18. Hata bibi alikuwa binti 19. Kisigino hakikai mbele 20. Kama mapenz pesa kaolewe na benki 21. Hata barabara ina matuta lakin huwez panda viazi 22. Mavi hayana miba lakin ukikanyaga lazma uchechemee 23. Paka haishi kwa msela 24. Ukipendwa ujue kuna boya kaachwa 25. NIPO NIPO KWANZA 26. Mchana nzi ucku mbu 27. Ucmshangae funza kukata viuno ndio mwendo wake 28. Kama umelipenda(gari) bonyeza nyota liwe lako 29. Supermarket hawauzi mkaa 30. We nisubiri mi nakungoja. 31. Zetu dagaa kuku tamaa 32. Hata uwe na heshima vipi huwezi kumpokea askari bunduki H ππππππππππ
Updated at: 2024-05-25 17:45:32 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Et jana usiku mwiz kavunja mlango kwangu akaanza kutafuta kitu kila kona ikabid na mie niamke namuuliza unatafuta nini ananijibu hela ndipo nilipoanza na mie kutafuta nae maana hta hela ya kula Jana sikua nayo alichoka zaid nilipomuliza una uhakika uliweka humu?
Updated at: 2024-05-25 17:13:28 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
β¦Upo kazini umeacha familia yako nyumbani mara ghafla unapigiwa simu kutazama unakutana na no ngeni na kuamua kuipokea ndipo unakutana na Sauti ya msichana ya kuvutia lakin kabla hajasema shida yake anaamua kukata simu. Unashikwa na hamu ya kujua ni nani. Tamaa ya mchepuko inakujia ghafla na kuamua kuipiga ile no tena kwa mara nyingine inakuwa haipatikani.
Siku hiyo hiyo usiku ukiwa umelala chumba kimoja na mkeo meseji inaingia tena kwenye cm yako kwa ile namba iliyokupigia mchana ikikuomba umpigie kwa mida ule na kusisitiza kuwa ana hamu ya kukufahamu. kila ukimtumia meseji ya kumdanganya upo sehemu mbaya hasikii anakubipu mara nyingi. Uzalendo unakushinda, unamuangalia pembeni mkeo kalala fofofo kajifunika shuka hadi usoni. Unaamua kuondoka kwa kunyata mpaka sebuleni kwenda kuipiga Ile namba kwa lengo la Kumwambia kesho mkutane. Ile unafika sebuleni na kuanza kuipiga ile cm ndipo unakutana na sauti hii:-Β MUME WANGU ACHA MCHEPUKO, NILIKUWA NAKUPIMA TU RUDI TU CHUMBANI TULALEΒ ππππππππ Hapo ndo utajua kwann bata hata ale kokoto anaharisha ππππππππ