Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
eBooks: Biashara - Mbinu za Ujasiriamali na Biashara Kufanya tofauti - AckySHINE
AMINI UNA AKILI YENYE UWEZO MKUBWA WA KUBUNI WAZO LA KUWEZA KUKUSAIDIA KUFANIKIWA KIMAISHA
📃 ✅
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:05 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Huwa nikikaa na kufikiri ni namna gani binadamu aliweza kubuni ndege, meli kubwa hasa za mizigo, gari na vitu vinginevyo na badae kuja kuwa msaada mkubwa katika dunia yetu ya siku leo hata kurahisisha maisha katika eneo fulani lililokuwa na ugumu kwetu, basi nauona uwezo wa Mungu aliouweka ndani ya binadamu huyu ingawa yeye binafsi kama binadamu wakati mwingine hatulitambui hilo na kama tunalitambua basi ni wachache na wakati mwingine hatujakaa vizuri kuitumia hii fursa ya uwezo huo tuliopewa. Hii inaonyesha ni jinsi gani binadamu alivyo na uwezo mkubwa wa kufanya ubunifu kwa kupitia akili aliyonayo na kuleta mageuzi na mshangao mkubwa katika ulimwengu tunaoishi.
Hii ndio sababu kwa nini huwezi kufanikiwa kibiashara
📃 ✅
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:12 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
HUWEZI KUFANIKIWA KIBIASHARA KAMA UNAPENDA KUJIHURUMIA HURUMIA! 💥Mama mmoja Mzungu alitembelea mlima Kilimanjaro miaka iliyopita. Alikuwa amepanga kupanda mlima Kilimanjaro mpaka kileleni, yaani Kibo na Mawenzi, ili hatimaye apewe cheti cha kupanda mlima mrefu Afrika.
Kukosa hela sio tatizo bali ndio kigezo ya kutafuta hela
📃 ✅
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:19 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ukimonyesha mtu fursa akakwambia hana hela mwambie hiyo ndio sababu ya wewe kumonyesha fursa ili awe na hela tukumbuke kuwa hela haitokani na helahela inatokana na fursa
Updated at: 2024-05-23 16:07:20 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
1.💥Umejipa jukumu la kuwa "mpelelezi" wa maisha ya wengine na umesahau maisha yako.
2.💥Umebeba vinyongo na visasi moyoni vinavyokufanya uwafikirie waliokuumiza zaidi kuliko kufikiria furaha na maendeleo yako.
3.💥 Una marafiki wengi ambao ni kama kupe, wapo kukutumia tu na hawachangii lolote katika maendeleo zaidi ya kujifanya ndio watu wako karibu lakini kumbe wapo kwa maslahi yao!
Updated at: 2024-05-23 16:07:22 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Batiki inatengenezwa kama ifuatavyo
MAHITAJI:
1.Vibanio vyenye urembo mbalimbali. 2.Sponji zenye urembo mbalimbali. 3.Brash kubwa/ndogo. 4.Meza kubwa yenye urefu wa mita moja mpaka mbili. 5.Sufuria. 6.Vitambaa vya mpira. 7.Misumari midogo. 8.Jiko.
Ushauri wangu kwa leo: Zingatia hili, hamasika, badilika
📃 ✅
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tupo kwenye dunia ambayo tulikuta watu na tutawaacha watu. Vyote tulivyovikuta vilianzishwa na binadamu wengine wenye mawazo mema na wenye mawazo mabaya pia. Vitu vingi tunavyovifanya tunaendeleza tulivyovikuta ni mara chache kukuta kitu kipya ambacho hakitegemei mazingira na asili ya tulivyovikuta.
Updated at: 2024-05-23 16:07:34 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ikiwa leo ni tarehe **1/12 huwezi amini kuwa hakuna tarehe 1 nyingine tutakayoiona ya mwaka huu hivyo sichelei kusema kuwa mwaka umeisha .Lakini mwaka unaishaje??? pengine hili ndilo swali gumu na la muhimu la kujiuliza .Je, Mwaka unaisha ukiwa umefanya nini cha kujipongeza??? .Je mwaka unakaribia kuisha maarifa yako yakiwa yameongozeka kwa kiasi gani???.Haya ni maswali muhimu sana unavyooanza kufikiria juu ya sherehe za mwisho wa mwaka.
Kanuni ya fedha ya matumizi na mipango ambayo itakusaidia ukiifuata
📃 ✅
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:00 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jifunze kanuni za fedha kama ilivyoainishwa hapo chini. Fedha inatakiwa uwe na nidhamu nayo katika kutumia Hii kanuni inatumika kwenye vyanzo vyako vyote vya fedha ili uwe na mafanikio yenye amani
Jifunze kupitia mfano huu Ili uishi kwa amani na watu
📃 ✅
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Siku moja nilichukua taxi aina ya UBER nikiwa naelekea uwanja wa Ndege Mwl. Nyerere Dereva huku akiendesha kwa ustaarabu sana mara ghafla pasipo kutegemea gari ya taka ikajitokeza mbele yetu kutokea nje ya barabara. Dereva wa taxi kwa umakini na neema ya Mungu akalikwepa gari hilo na ilikuwa kidogo agonge gari zingine mbele yetu.
Updated at: 2024-05-23 16:07:34 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Sikia haihitaji ukalishwe chini ndo uelewe, Ukweli ni kwamba unajishughulisha Sana na mambo yasiyo Kuhusu katika mafanikio.wazungu husema mind your own business sasa Sijui huu msemo unauchukuliaje?? Imagine unamjua Ali kiba hadi bafuni kwake, tour zote za mwaka huu unazijua hadi nyingine unataka kumpangia, nikuulize wewe ni mwanamziki??
Updated at: 2024-05-23 16:07:18 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jifunze kujikagua, jifunze kujiuliza je hapa ndipo napotakiwa kuwa? Usifurahie tu kwamba upo hapo kwa muda mrefu yamkini unaona panakufaa and you are settled lakini ukweli ni kwamba sio pako na haukutengenezwa kuwa hapo. Hata kama tai ataonekana kwenye banda la kuku lakini ukweli ni kwamba tai kaumbiwa kuwa angani tofauti na kuku aishie bandani. Jiulize hapo ulipo ni pako??
Updated at: 2024-05-23 16:07:17 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Watu ambao hawana pesa ila wana muda wa bwerere. Hawajui thamani ya muda. Hawa ndo wale ambao hawajui cha kufanya. Anaamka mpaka analala usiku hana specific timetable. Unaweza kumkuta anaenda dukani ukamwambia nisindikize saluni na akakubali. Yupo yupo tu. Unaweza kuta ameingia Facebook hajui hata kwa mini. Basi tu kwa sababu ana bando. Akiperuzi akaona mahali wanaongelea mpira yumo
Kuwa na kawaida ya kujiwekea Akiba ni njia na Siri ya kuwa tajiri
📃 ✅
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:30 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Watu wengi wanajiuliza, “Siri ya utajiri ni nini?” Je ni mbinu gani zinaweza kumsaidia mtu kupata utajiri? Siri kubwaya utajiri ni kujifunza elimu ya namna ya kutafuta mtaji, kuwekeza kwa busara kwa namna ambayo daima panakuwa naziada na faida.
Updated at: 2024-05-23 16:07:13 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
kadri temperature inavyo ongezeka chura nae huwa ana increase temperature ya mwili wake..
pindi inapokaribia kufika boiling point yaani nyuzi 100 chura atashindwa kuongeza temperature ktk mwili wake na hapo ndipo atataka kutoka ktk maji hayo ya moto na yanayo endelea kuchemka.. kutokana na kutumia nguvu nyingi sana ktk kuongeza temperature ktk mwili wake,pindi anapotaka kuruka atashindwa na atakufa humo ndani ya chombo cha maji yanayochemka..
FURSA HAIJI MARA MBILI: Jinsi unavyoweza kupata faida au hasara ukitumia Nafasi au fursa uliyonayo
📃 ✅
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:29 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kwenye maisha fursa moja tu inatosha kabisa kubadilisha hali yako ya sasa na kukuweka kwenye kiwango kingine kabisa cha mafanikio.Kuna watu wengi sana ambao waliwahi kufikiria kuwa maisha yao yatachukua miaka mingi sana kabla hayajabadilika na kwa mshangao wao walipoanza kufanya vitu sahihi wakakutana na mabadiliko makubwa sana katika maisha yao kwa kupitia fursa moja tu.
Updated at: 2024-05-23 16:07:17 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu anayejenga GHOROFA na yule anayejenga Nyumba ya KAWAIDA.
Anayejenga Ghorofa anatakiwa achimbe msingi Mrefu kwenda chini kabla hajaanza kuinua Ghorofa yake juu. Hivyo wakati huyu mwingine anapokuwa anajenga Nyumba ya kawaida atakapokuwa tayari anakaribia hata kuezeka, unaweza kukuta yule anayejenga Ghorofa bado yuko kwenye Msingi. Ila siku akianza kuinua Ghorofa lake, kila mtu atashangaa urefu wa juu atakaoenda nao.
Updated at: 2024-05-23 16:07:12 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kila mtu ambaye ni hai amepewa muda Wa masaa 24 kila siku,168 kwa wiki,672 kwa mwezi,8064 kwa miezi 12 au kwa mwaka.
Katika hayo masaa 24 unayoyapata kila siku unayatumiaje katika suala zima la kukufikisha katika ndoto na malengo au mafanikio yako?
Kwa nini kuna matajiri na maskini na wote tunapewa masaa 24??? Tucheki mgawanyo Wa masaa 24 ulivyo….katika masaa 24 unayopewa kwa siku masaa 8 ni ya kazi,masaa 8 ni ya kulala na masaa 8 ni ya kufanya mambo yako mengine.
Updated at: 2024-05-23 16:07:32 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
UJASIRIAMALI
Ni uthubutu au ujaribu wa ufanyaji wa shughuli yoyote halali na kupitia shughuli hiyo mtu watu huweza kupata kipato.
MJASIRIAMALI
Ni mtu mwenye yeyote mwenye uthubutu au kujaribu kufanya shughuli yoyote halali,ambapo kupitia shughuli hiyo anaweza kupata kipato ambacho kitamfanya apige hatua ya kimaendeleo ya kiuchumi.Shughuli za kijasiliamali zinaweza kuwa za biashara ya uzalishaji mali au bidhaa.
Updated at: 2024-05-23 16:07:23 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna baadhi ya LEVEL huwezi kufika…Kuna MAFANIKIO huwezi kuyafikia…Kuna HELA huwezi kuzipata…Kama umezungukwa na watu BASIC… Kuanzia asubuhi mpaka jioni wanaongelea WATU TU..Fulani kamegwa na yule..halafu yule naniliu saivi anatembea na yule ex wa nanii…Asubuhi mpaka jioni DISCUSSING PEOPLE…Hawa ndio watu BASIC…Hata siku 1 hawatakupa Ushauri kuhusu HOW TO REACH SOMEWHERE…NEVER
Updated at: 2024-05-23 16:06:57 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mbinu 5 za kukufanikisha maishani Unaweza ukawa upo kwenye hali ya kulalamika maisha yako ni magumu na unashangaa kwa nini hufanikiwi katika maisha yako kama jinsi unavyotaka wewe. Hali hii inaweza ikawa inakuumiza pengine kila ukiangalia rafiki zako ama maisha ya wengine yanavyozidi kuwa mazuri, wakati wewe upo katika hali ngumu. Na pengine umekuwa ukijiuliza nini siri kubwa ya mafanikio yao ambayo wanaitumia ambayo wewe huna. Kutokana na hali hiyo umekuwa ukijilaumu kujilaumu na kujiuliza kwanini nyingi ambazo hazina majibu. Kitu usichokijua watu hawa huwa wanatumia mbinu fulani kufanikiwa.