Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
eBooks: Sala za Katoliki: Sala Muhimu Kwa Mkristu Mkatoliki - Topic 2 - AckySHINE
SALA YA NOVENA KWA MOYO MTAKATIFU WA YESU
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-27 07:13:51 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ee Moyo Mtakatifu sana wa Yesu, chemchemi ya kila baraka, ninakuabudu, ninakupenda, na kwa majuto halisi ya dhambi zangu, nakutolea moyo wangu dhaifu. Nifanye mnyenyekevu, mvumilivu na safi, nikikubali na kuyatii kabisa mapenzi yako. Ee Yesu mwema, unijalie niishi nawe na kwa ajili yako.
Updated at: 2024-05-27 07:14:24 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Baba yetu uliye mbinguni Jina lako litukuzwe Ufalme wako ufike Utakalo lifanyike Duniani kama mbinguni Utupe leo mkate wetu wa kila siku Utusamehe makosa yetu Kama tunavyowasamehe Na sisi waliotukosea Usitutie katika kishawishi Lakini utuopoe maovuni. Amina.
Updated at: 2024-05-27 07:14:12 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Yesu, Mungu wangu mpenzi,/ upo hapa katika Altare mbele yangu;/ na mimi napiga magoti mbele yako.// Waniangalia sana,/ siyo kwa kunipeleleza,/ lakini kwa sababu wapenda kuniona hivi karibu na wewe,/ wafurahiwa nikija kukuabudu./ Wayasikiliza maneno yangu yote/ yenye kutoka mdomoni mwangu,/ na zaidi wapokea maneno yangu yanayotoka moyoni./
Updated at: 2024-05-27 07:13:45 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ee Mt. Yosefu, Baba Mlishi wa Mwokozi wangu, na mchumba safi wa Mama wa Mungu, leo ninakuchagua wewe, kama mwombezi wangu kwa Mungu Mwenyezi, na pia kama mfano wangu, na mlinzi wangu, na baba yangu, katika bonde hili la ugenini.
Updated at: 2024-05-27 07:14:04 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
βββ
Sala ya saa tisaππΎ
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. A mina
Yesu, ulikufa, lakini chanzo cha uhai kilitoka kwa ajili ya watu, na bahari ya huruma ilifunguka kwa ajili ya ulimwengu mzima. Ee chemchemi ya Uhai, huruma ya Mungu isiyo na mwisho, ikafunika ulimwengu mzima na ukajimwaga mwenyewe juu yetu.
Updated at: 2024-05-27 07:14:08 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ewe Mungu Mwenyezi, sisi kama familia tunakushukuru kwa zawadi ya Mama Kanisa Katoliki ambaye siku zote hutupatia malezi bora kwa ajili ya wokovu wetu. Kanisa halichoki kutuhimiza tutafakari na kuishi utakatifu wa familia ya Nazareti ya Yesu, Maria na Yosefu. Familia hii iliishi upendo uliojengwa kwa fadhila za imani, uaminifu, utii, uvumilivu na upole hata wakawa watakatifu. Tunapoadhimisha mwaka wa Familia, tunaiweka mbele yetu familia ya Nazareti iwe dira, baraka na mfano kwa familia zetu.
Updated at: 2024-05-27 07:13:47 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
TUWAZE KATIKA MOYO WETU MAKOSA YA LEO TULIYOMKOSEA MUNGU KWA MAWAZO,KWA MANENO, KWA VITENDO NA KWA KUTOTIMIZA WAJIBU (HUSUBIRI KIDOGO) NAKUUNGAMIA MUNGU MWENYEZI,NANYI NDUGU ZANGU,KWANI NIMEKOSA MNO KWA MAWAZO,KWA MANENO,KWA VITENDO NA KWA KUTOTIMIZA WAJIBU,NIMEKOSA MIMI,NIMEKOSA SANA.NDIYO MAANA NAKUOMBA MARIA MWENYE HERI,BIKIRA DAIMA,MALAIKA NA WATAKATIFU WOTE,NANYI NDUGU ZANGU,MNIOMBEENI KWA BWANA MUNGU WETU.
Updated at: 2024-05-27 07:14:25 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu, utulinde katika vita, uwe kinga yetu katika maovu na maoteo ya shetani, Mungu amtiishe, tunaomba sana, nawe Mkuu wa Majeshi ya Mbinguni kwa nguvu ya Mungu uwaangushe motoni shetani na pepo wabaya wengine wote, wanaozunguka duniani, ili kuzipoteza roho za watu.Β Amina.
Updated at: 2024-05-27 07:14:10 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ee Yosef mwenye heri, tunakimbilia kwako, katika masumbuko yetu, na kishaomba shime ya Mchumba wako Mtakatifu, tunaomba pia kwa matumaini usimamizi wako. Kwa ajili ya mapendo uliyompenda nayo Bikira Mtakatifu, Mzazi wa Mungu, na kwa ajili ya tunza ya Baba, uliyomtunza nayo Mtoto Yesu, tunakuomba sana, utuangalie kwa wema, sisi tuliokuwa fungu lake Yesu Kristo, tuliokombolewa kwa damu yake, utusimamie katika masumbuko yetu, kwa enzi na shime yako.
Updated at: 2024-05-27 07:13:57 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ee Mama mbarikiwa na Bikira mwenye uchungu, Malkia wa Mashahidi, uliyesimama chini ya msalaba na uliyemtazama Mwana wako akifa, unitazame kwa huruma ya kimama ninayekusikitikia. Kwa sababu ya upanga uliochoma moyo wako, kwa mateso ya maisha yako nakuomba uniangalie kwa wema ukasikilize maombi yangu.Β
Updated at: 2024-05-27 07:14:14 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ee Moyo Mtakatifu wa Yesu, ninakukimbilia, ninakuja kwako katika mikono yako yenye huruma. Ndiwe tegemeo langu na tumaini langu dhabiti. Ndiwe mwenye dawa ya maovu yangu yote, malipizi ya makosa yangu yote. Waweza kunipatia haja zangu na neema ninazoziomba mimi na wengine. Wewe uko ili kutusaidia sote, ndiwe mwanga mkuu usiozimika, ndiwe chanzo cha nguvu, uvumilivu, amani na faraja.Β
Updated at: 2024-05-27 07:14:06 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Kwa jina la Babaβ¦..
Ee Baba yetu Mungu mkuu,umenilinda usiku huu. Nakushukuru kwa moyo, ee Baba,Mwana na Roho. Nilinde tena siku hii,niache dhambi nikutii.Naomba sana Baba wee, baraka yako nipokee. Bikira safi, Ee Maria nisipotee nisimamie. Mlinzi mkuu malaika wee kwa Mungu wetu niombee,nitake nitende mema tu na mwisho nije kwako juu.Amina.
Updated at: 2024-05-27 07:14:19 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Mungu wangu, natumaini kwako nitapewa kwa njia ya Yesu Kristu, neema zako duniani na utukufu mbinguni, kwani ndiwe uliyeagana hayo nasi, nawe mwamini. Amina
Updated at: 2024-05-27 07:14:07 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
1. NDIMI BWANA MUNGU WAKO, USIABUDU MIUNGU WENGINE. 2. USILITAJE BURE JINA LA MUNGU WAKO. 3. SHIKA KITAKATIFU SIKU YA MUNGU. 4. WAHESHIMU BABA NA MAMA, UPATE MIAKA MINGI NA HERI DUNIANI.
Updated at: 2024-05-27 07:14:01 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ee Bwana Mungu, utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na mwili siku zote; na kwa maombezi matukufu ya Maria Mtakaatifu Bikira daima, tuopolewe na mashaka ya saa, tupate na furaha za milele. Kwa Kristo Bwana wetu, Amina.
Updated at: 2024-05-27 07:13:46 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ee Bwana Yesu Kristo. Mkombozi wetu, kwa mapendo na tamaa yako ya kutaka kulinda vema Kanisa lako, ukachagua Mapadri wawe Wachungaji na Viongozi wa roho za watu. Nakuomba sana; ubariki nia na bidii inayowapasa Mapadri wote katika kazi zao. Uwaongezee Utakatifu.
Novena ya Siku tisa kwa Mtakatifu Agustino wa Hippo: Sala zote na Litania
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-27 07:14:16 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Pamoja na Mtakatifu Augustino tunasema β Umetuumba kwa ajili yako ee Bwana, kwani ni wewe peke yako ndie Mungu wetu, na nyoyo zetu hazitapumzika, hadi tupumzike ndani mwako.β
Updated at: 2024-05-27 07:14:21 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Kwa njia ya Maji haya ya Baraka, na kwa njia ya Damu yako azizi, na kwa maombezi ya Moyo Safi wa Maria, unioshe na uovu wangu wote na uwasaidie roho zinazoteseka toharani. Amina.
Updated at: 2024-05-27 07:14:15 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Bwana utuhurumie Bwana utuhurumie Kristo utuhurumie Kristo utuhurumie Bwana utuhurumie Bwana utuhurumie Kristo utusikie Kristo utusikilize Baba wa mbinguni Mungu Utuhurumie Mwana, Mkombozi wa dunia Mungu Utuhurumie Roho Mtakatifu Mungu Utuhurumie
Updated at: 2024-05-27 07:13:53 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Tuusifu Utatu Mtakatifu wa Mungu Mwenyezi, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, milele na milele, Amina.
Ee Utatu Mtakatifu wa Mwenyezi Mungu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, nasadiki kuwa upo hapa na mahali pote. Ee Mungu wangu, umeniumba, umenikomboa, umenifanya mkristo, umenizidishia neema zako hapa duniani, umenitayarishia makao yangu mbinguni, umenijalia na siku hii nikutumikie.Β
Updated at: 2024-05-27 07:14:23 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ewe Mtakatifu Yuda Tadei,/ mtume mtukufu na shahidi wa Kristo,/ umesifika pote kwa wepesi wako wa kutoa misaada/ kwa wanaokukimbilia katika matatizo yao mazito./ Pia ni mwombezi wa waliopondeka moyo./
Updated at: 2024-05-27 07:14:10 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Kumheshimu Mungu wangu, Namtolea roho yangu, Nifanye kazi nipumzike, Amri zake tu nishike, Wazo neno tendo lote, Namtolea Mungu pote, Roho, mwili chote changu, pendo na uzima wangu, Mungu wangu nitampenda, Wala dhambi sitatenda, Jina lako nasifia, Utakalo hutimia, Kwa utii navumilia, Teso na matata pia, Nipe Bwana neema zako, Niongezee sifa yako, Amina.
Updated at: 2024-05-27 07:14:19 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ee Baba yetu Mungu Mkuu, Umenilinda usiku huu, Ninakushukuru kwa moyo, Ee Baba, Mwana na Roho, Nilinde tena siku hii, Niache dhambi nikutii, Naomba sana Baba wee, Baraka yako nipokee, Bikira safi ee Maria, Nisipotee unisimamie, Mlinzi Mkuu Malaika wee, Kwa Mungu wetu niombee, Nitake nitende mema tu, Na mwisho nije kwake juu, Amina.