Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/katoliki/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Mbinu 9 za kuwavutia na kuwateka wanawake kimapenzi

Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image

Kati ya wanawake na wanaume wote wawili wanahitaji kuvutiwa na wenza wao ili wadumu katika mahusiano. Kama mwanaume lazima upate wakati wa kujua unatakiwa kufanya nini kwa ajili ya kulifanya penzi lako lizidi kuchanua.
Hali kadhalika kama bado haupo Kwenye mahusiano kuna mambo ambayo ni ya msingi kufanya au kuwa nayo ili uweze kuwa na mvuto zaidi kwa wanawake.

Yafuatayo ni mambo yakufanya ili kumvutia mwanamke.

1. Kuonyesha kuwa unamjali

Wanawake wanapenda sana wanaume wanaojali wao kama wao, wanaojali kile wanachokifanya na watu wao wa karibu kama ndugu na wazazi. Wanapenda wanaume wanawaona wao ni kila kitu na wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa ya kumkwaza mpenzi wako. Mwanamme anatakiwa amjali mpenzi wake kwa kila hali. Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa sana ya kuendelea kudumu katika uhusiano hai. Vile vile kuonyesha kujali mambo yake na watu wake wa karibu kunamvutia mwanamke.

2. Kuonyesha kuwa karibu na kupatikana unapohitajika

Mwanamke huvutiwa sana na mtu ambaye yupo karibu nae na ambaye anapatikana wakati anapohitajika. Kati ya vitu vinavyowapa wapendeza sana wanawake ni pamoja na kusogezwa karibu. Hapa ni kuwa naye katika mambo mengi unayoyafanya kila siku na kushiriki katika mambo yake hata kwa mawazo kama ukishindwa kwa matendo. Ni vizuri kuwa naye au kuwasiliana naye wakati wa kula, ukitaka kujua aina ya chakula alichokula siku hiyo au ikiwezekana mchagulie. Ni mambo madogo sana lakini yanayoongeza nakshi katika mapenzi na ambayo ni muhimu sana kwa wanawake. Yapo mengi sana ambayo kwa kuyafanya utakuwa umemsogeza mpenzi wako karibu yako, mfano kutembea pamoja, kuangalia movie pamoja, nakadhalika. Tumia ubunifu wako ili uweze kuteka hisia za mwenzi wako kisawasawa kwani mwanamke anavutiwa sana na mtu aliye karibu nae.

3. Kumsifia na kumuonyesha kuwa ni bora

Wanawake wanapenda kusifiwa na kuonekana kuwa bora. Mwanamke akisifiwa anahisi kupendwa kupita kiasi. Anajiona kamili, peke yake na mwenye nguvu kwako. Anajiamini na unamfanya azidi kukupenda kwa kuwa anaamini yupo na mwanaume ambaye anajivunia kuwa naye. Vilevile kumsifia mwanamke kwake ni njia ya kuonyesha upendo na Ishara ya kuonyesha kumjali kupita kiasi.

[products columns="2" ids="30827"]

4. Kupewa kipaumbele

Mwanamke anavutiwa zaidi na mtu anayeonyesha kumpa kipaumbele na kupewa nafasi. Kuna wakati wanawake huwa na mambo yao binafsi. Kazini au kifamilia. Inawezekana akatatizika katika eneo fulani ambalo kwa namna moja ama nyingine atahitaji usaidizi wako. Ikitokea mwanamke akawa katika hali hiyo, msikilize.
Mathalani ana tatizo la kifamilia, amekuambia mmoja wa wazazi wake anaumwa, msaidie. Si lazima kifedha, lakini kuonesha kujali kwako tu, kutampa matumani kwamba anaishi na mtu sahihi. Acha kupuuza mambo yake; hata yale madogo, kama ya โ€˜mtoto wa dada amerudishwa ada shuleniโ€™.
Msikilize, mshauri panapofaa kufanya hivyo na ukiweza msaidie hata kifedha. Katika upande wa pili ni hivyo hivyo. Labda una tatizo binafsi, kazini kwako au kifamilia, mshirikishe.
Unaweza kushangaa jambo ambalo uliamini unaweza kulimaliza peke yako, kwa kumshirikisha likawa jepesi zaidi na mambo yakaendelea vyema. Kipaumbele kwa namna yoyote ile, kunaongeza mapenzi zaidi kwa mwanamke.

5. Usafi binafsi

Wanawake wanapenda mwanamme ambaye ni msafi, hii ni kwa sababu kiasili wamejaliwa kupenda usafi ndio maana ni nadra sana kukutana na mwanamke asiyejipenda. Ndiyo maana wanaitwa mapambo ya nyumba au la nyumba! Ni kwa sababu ya hulka yao ya kupenda sana usafi. Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini kuwa na wewe. Hata nyumbani kwako, lazima uishi katika nyumba safi. Hata anapokuja kukutembelea, anakuta mazingira masafi kuanzia sebuleni hadi chumbani. Anapokukuta katika hali ya usafi, inakuwa rahisi zaidi yeye kuanzia hapo alipokukuta na kuendelea mbele.

6. Anavutiwa na mwanamme anayejiamini

Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na mwanaume ambaye anajiamini yaani mwenye uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza sawia pale anapotakiwa kufanya hivyo au wakati wowote ule. Siyo anayebabaika na kuyumba yumba. Suala la msimamo binafsi, kwa mwanamke ni kubwa kuliko hata kumnunulia nguo mpya.
Mwanamke anapenda kukuona ukiwa katika hali halisi ya maisha yako, usiyeyumbishwa na mwenye kutoa maamuzi yasiyoyumba.
Wakati mwingine, mwanamke anaweza kukupima hata katika jambo ambalo amekosea yeye, ataangalia unavyotoa maamuzi yako, lakini pia atafuatilia kuona kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha.
Anataka kuona msimamo wako muda wote. Mwanamke hapendi mtu anayebadilikabadilika Kwenye maamuzi na misimamo yake.

7. Malengo ya maisha

Mwanamke anapenda mwanaume mwenye malengo na anayemshirikisha katika mipango yake. Mwanamke anavutiwa na mwanamke mwenye malengo katika maisha yake. Vilevile anapenda mtu anayemshirikisha katika malengo yake na kumuweka katika mipango yake. Faida ya kumshirikisha katika malengo yako ni pamoja na kunampa nguvu na nafasi ya kujiona mama katika familia yenu. Msaidizi kamili wa nyumba yenu. Mweleze juu ya malengo yako, wakati mwingine anaweza kukusaidia sehemu ambayo hukutarajia.

8. Anayeweza kujitetea

Mwanamke hupenda mwanamme anayeweza kujitetea. Mwanaume aliye โ€˜fitiโ€™ ni chaguo la wanawake wengi. Si mnyonge. Mpole kupitiliza na aliye tayari kuonewa! Huyu hana nafasi.
Wanawake hawapendi kuwa na wanaume ambao wapo tayari kuonewa. Wanataka wenye uwezo wa kusimama kidete kuona haki zao hazichukuliwi kirahisi. Hili si suala la kutetea tu haki yako pekee kama mwanaume, bali inapobidi kusimamia haki ya mwanamke wako. Nisieleweke vibaya katika hili, lakini mwanaume imara ni yule ambaye ana nguvu โ€“ anafanya mazoezi na ambaye yupo tayari kwa lolote! Inapowezekana, uwe na uwezo wa โ€˜kuzichapaโ€™ ikiwa mtakutana na vibaka au watu wabaya wenye lengo wa kukudhuru/kuwadhuru au kumdhuru mpenzi wako.

9. Anayemtosheleza tendo la ndoa

Mwanamke anavutiwa zaidi na mwanamme anayeweza kumridhisha katika tendo la ndoa. Anataka mwanamme anayeweza kufanya kile anachotaka yeye na kile anachokipenda. Mwanamke hapendi mwanamme anayemkomoa katika tendo la ndoa au anayefanya mambo asiyoyapenda. Mwanamke anataka kuridhishwa na kujaliwa katika tendo la ndoa.

Ili kufahamu mambo Mbalimbali ya muhimu kuhusu wanawake, Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE
[products columns="2" ids="30827"]
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya kushirikiana na mke wako katika Kulea Watoto

Jinsi ya kushirikiana na mke wako katika Kulea Watoto

Kushirikiana na mke wako katika kulea watoto ni muhimu katika kujenga familia yenye nguvu na yenye u... Read More
Jinsi ya Kuelewa na kuheshimu mipaka ya kifamilia na urafiki na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kuheshimu mipaka ya kifamilia na urafiki na mpenzi wako

Kuelewa na kuheshimu mipaka ya kifamilia na urafiki ni muhimu katika kudumisha uhusiano mzuri na mpe... Read More
Jinsi ya Kudumisha Heshima na Utu katika Familia: Kuheshimu Tofauti na Upekee

Jinsi ya Kudumisha Heshima na Utu katika Familia: Kuheshimu Tofauti na Upekee

Familia ni sehemu muhimu sana katika maisha yetu. Ni mahali ambapo tunakua na kujifunza maadili y... Read More

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kukosa Uaminifu katika Familia: Kuhamasisha Uaminifu na Urejesho

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kukosa Uaminifu katika Familia: Kuhamasisha Uaminifu na Urejesho

Katika maisha yetu ya kila siku, tunakabiliana na changamoto mbalimbali katika familia zetu. Moja... Read More

Jinsi ya Kuzungumza na mpenzi wako kuhusu mipango ya elimu na ukuaji binafsi

Jinsi ya Kuzungumza na mpenzi wako kuhusu mipango ya elimu na ukuaji binafsi

Kuzungumza na mpenzi wako kuhusu mipango ya elimu na ukuaji binafsi ni njia nzuri ya kuendeleza na k... Read More
Jinsi ya Kuunda Mazingira ya Kuunga Mkono Talanta na Ndoto za Familia

Jinsi ya Kuunda Mazingira ya Kuunga Mkono Talanta na Ndoto za Familia

  1. Elewa Ndoto na Talanta za Familia: Kuelewa na kuzingatia ndoto na talanta za familia ya... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kijinsia wenye Kuridhisha katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kijinsia wenye Kuridhisha katika Familia

  1. Kuhamasisha ushirikiano wa kijinsia wenye kuridhisha katika familia ni jambo muhimu lin... Read More

Njia za Kuonyesha Msichana Wako Kuwa Ana thamani Kwako

Njia za Kuonyesha Msichana Wako Kuwa Ana thamani Kwako

Kama mwanaume, kuna mambo mengi ambayo unaweza kufanya ili kuonyesha msichana wako kuwa ana thama... Read More

Kujenga Ushirikiano wa Kifedha na Kuweka Malengo ya Pamoja katika Familia

Kujenga Ushirikiano wa Kifedha na Kuweka Malengo ya Pamoja katika Familia

  1. Kuweka malengo ya pamoja katika familia ni jambo muhimu sana katika kujenga ushirikiano... Read More

Je, watu wanapendelea kujaribu njia za kuleta msisimko wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kujaribu njia za kuleta msisimko wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Karibu sana kwenye makala hii ya blog, ambapo tutajadili kuhusu kwa nini watu wanapendelea kutafu... Read More

Jinsi ya Kushirikiana na mpenzi wako majukumu ya nyumbani na majukumu ya kifedha

Jinsi ya Kushirikiana na mpenzi wako majukumu ya nyumbani na majukumu ya kifedha

Kushirikiana na mpenzi wako katika majukumu ya nyumbani na majukumu ya kifedha ni muhimu katika kuje... Read More
Jinsi ya Kuwa Msikivu: Sanaa ya Kusikiliza katika Mahusiano ya Familia

Jinsi ya Kuwa Msikivu: Sanaa ya Kusikiliza katika Mahusiano ya Familia

Kuwa msikivu ni moja ya sanaa muhimu sana katika mahusiano ya familia. Kuwa msikivu kunaweza kusa... Read More

๐Ÿ“– Explore More Articles | โœ๐Ÿป Re-Write Articles
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About