JAMAA alimuaga mke wake mlokole kuwa anaenda semina ya siku tatu, kumbe anakwenda kwa bi mdogo. Mke akamwambia mumewe; "Tupige magoti tusali", Wakapiga magoti…: MKE: Eee baba msaidie mume wangu afike salama safari yake. MUME: Emen… MKE: Mpe nguvu katika yote atakayoyafanya huko. MUME: Emen… MKE: Akitaka kufanya uasherati ashindwe. MUME: Kimya… MKE: Akifanya uasherati apatwe na janga baya kwa uwezo wako bwana. MUME: …….!! MKE: Yaani akifanya uasherati afie hukohuko kwa mateso makali. MUME: Maombi gani sasa hayo!!?. Haya basi siendi semina ufurahi wewe. Chezea mawaifu walokole wewe!