Vipimo Vya Koshari

Mchele - 2 vikombe

Makaroni - 1 kikombe

Dengu za brown - 1 kikombe

Vitunguu vilokatwakatwa (chopped) - 2

Nyanya ziilokatwakatwa (chopped) - 4

Nyanya ya kopo - 1 kijiko cha supu

Kitunguu saumu(thomu/galic) ilosagwa - 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi ilosagwa - 1 kijiko cha chai

Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai

Mdalisini kijiti - 1

Bizari ya pilau (cumin seeds) - 1 kijiko cha supu

Hiliki - 2 chembe

Mafuta - 3 vijiko vya supu

Chumvi - kiasi

Vipimo Vya Kuku

Kuku - 3 LB

Kitunguu saumu(thomugalic) na tangawizi - 1 kijiko cha supu

Mtindi (yoghurt) - 1 kijiko cha supu

Pilipili ya masala nyekundu - 1 kijiko cha chai

Bizari upendazo - 1 kijiko cha chai

Ndimu - 1

Vitunguu slesi vilokaangwa - 3

Namna Kutayarisha Kuku

Kata kuku vipande vikubwa kiasi, osha, weka kando achuje maji.
Changanya vipimo vya kuku pamoja katika kibakuli.
Changanya pamoja na kuku, roweka muda wa kiasi nusu saa au zaidi.
Mchome (grill) kuku hadi aive weka kando.

Namna ya Kutayarisha Koshari

Tia mafuta katika sufuria, kaanga vitunguu hadi viive kuwa rangi hudhurungi.
Tia thomu ,mdalisini, bizari ya pilau na hiliki kaanga tena kidogo.
Tia nyanya, pilipili zote, nyanya kopo, chumvi changanya vizuri ukaange kidogo.
Epua sosi acha kando.
Chemsha dengu pamoja na kidonge cha supu ziive nusu kiini na ibakie supu yake. Muda wa kuchemsha dengu inategemea aina yake.
Tia mchele uchanganyike, funika, pika hadi uive vizuri pamoja na dengu
Chemsha makaroni hadi yaive , epua chuja maji.
Changanya pamoja wali wa dengu na macaroni.
Pakua katika sahani, kisha weka juu yake kuku aliyechomwa, mwagia vitunguu vilokaangwa, kisha mwagia sosi.