Tumia tasbihi ya kawaida yenye chembe ndogo 53.
Kwenye Msalaba Sali:
āEe Yesu tupe moyo wako kama amana ya upendo wako na kimbilio letu, ili tupate pumziko salama wakati wa maisha yetu na faraja tamu saa ya kufa kwetuā.
Baba Yetu ā¦ā¦..
Salamu Maria ā¦ā¦. (mara tatu)
Nasadiki ā¦ā¦ā¦..
Kwenye chembe kubwa Sali (Badala ya āBaba Yetuā):
āNinakuabudu, ninakutukuza na ninakupenda, Ee Moyo wa Yesu wangu mpenzi, uliopenywa na huzuni nyingi kwa ajili ya dhambi, ambazo zimekuwa zikitendwa hata leo, dhidi ya Sakramenti Takatifu sana ya Altare. Ninakutolea hapo kwa kuridhika, moyo wa Mama yako mpendevu, na mastahili ya watakatifu. Aminaā.
Kwenye chembe ndogo sali (Badala ya āSalamu Mariaā):
āEe Moyo Mtakatifu wa Yesu, uwakao mapendo kwetu, washa nyoyo zetu kwa mapendo yako"