Ndiyo. Nikotini iliyo kwenye tumbaku ni sumu. Ukiwa na kiwango kikubwa cha nikotini katika damu utajisikia kichefuchefu, kutapika, kujaa kwa mate mdomoni, maumivu ya sehemu za chini ya tumbo, kuharisha, na kujihisi dhaifu. Dalili nyingine ni kuumwa na kichwa, kizunguzungu, kuongezeka kwa mapigo ya moyo, kupata shinikizo la damu, kutetemeka na kutokwa na jasho baridi. Nikotini nyingi inaweza kusababisha ukosefu wa umakini na pia ukosefu wa usingizi.