Ukeketaji au tohara ya wanawake ni hatari sana kwa msichana anayetahiriwa. Wasichana hufa kutokana na madhara yake makubwa zaidi kwa vile: viungo vya ndani vya uzazi na kusababisha ugumba na hata vifo. ukeketaji. mwili wa mwanamke na kusababisha uambukizo. wakati wa kujifungua kutokana na kupungua ukubwa wa uke. Ukeketaji wa wanawake mara nyingi una madhara ya kisaikologia ambapo wasichana hupoteza tumaini na imani kwa walezi au wazazi na wanaweza wakapata mateso ya kujisikia waoga, kufadhaika, kutojiweza na kutokuwa kamilifu kimwili. Zaidi ya hayo, ukeketaji unampunguzia mwanamke hamu ya kujamiiana. Kufanikisha hamu ya ngono inategemea kwa kiasi kikubwa viungo vya uzazi vya nje. Ukeketaji hata hivyo unaharibu umbile na kazi za viungo vya uzazi vya nje vya mwanamke. Ina madhara kimwili na kisaikologia ambapo mara nyingi huleta matatizo ya mahusiano ya kimwili kati ya mwanamume na mwanamke. Kisimi ni sehemu ya mwili wa msichana chenye ashiki na hisia kali ya viungo vya uzazi. Kinasisimua ashiki kwa mwanamke anaposhikwa. Sehemu ya ndani ya mashavu na kisimi kwa kiasi kikubwa vinahusika na hali kiwango cha raha ya na kufikia mshindo wakati wa kujamiiana. Wakati kisimi na viungo vingine vya uzazi vimeondolewa, ashiki na raha hupungua kwa kiasi kikubwa. Endapo mwanamke amekatwa vibaya sana au uke umeshonwa, kuna uwezekano wa kupata maumivu na matatizo wakati wa kujamiiana na wa kujifungua.