Jamaa kaenda kanisani akakaa karibu na mrembo. Wakati mahubiri yakiendlea jamaa akaanza kuingiza vocal: Jamaa: dada mi nakupenda saana Dem: Kaka naomba umsikilize mchungaji Jamaa: nipe nafasi uwe msimamizi wa serikali ya moyo wangu… Dem: niache… Jamaa: kweli nakupenda mpnz Dem: (kwa sauti kubwa) nmesema NIACHEEEE!! Watu wote kanisani wakageuka… Jamaa kaona noma na ili atulize msala Jamaa: sikuachi hadi ukiri YESU kuwa Bwana na mwokozi wa Maisha yako.