Mawingu yametanda napanda kwenye kitanda,
macho nayaangaza,
taratibu navuta shuka na kujitanda,
mishumaa pembezoni inaniangaza,
mziki laini wanibembeleza kitu pekee nilichokikosa
ni joto lako na vijimambo vyako kunako kitanda!