Sidebar with Floating Button
AckySHINE 🔁
AckyShine

Ujumbe wa leo kwa mtu anayetaka kufanikiwa katika maisha kiuchumi

Featured Image

Kila mtu aliyefanikiwa ukifuatilia historia yake pengine unaweza kukata tamaa kabisa Na kusema mimi hii njia siiwez.

Lakin siri ya mafanikio ni uvumilivu Na kujituma ktk kazi uifanyao.

Ni kweli vijana wengi humaliza vyuo Na kusubiri ajira wanashindwa kusoma alama za nyakati, hawatambui kuwa sasa wasomi ni wengi sana ajira chache.

Mimi pia ni mwanafunzi wa Chuo kikuuu lakini ni mjasiri amali vilevile.

0 💬 ⬇️

Kwa ushauri huu jitambue upate mafanikio

Featured Image

Ukiona unalala masaa 9 wakati Donald Trump analala manne tu. Afu unaamka huna nauli na bado kesho unalala masaa manane tena.. Ujue unashabikia mafanikio.

Ukiona Bill Gates anasoma kitabu kimoja kwa wiki. Na wewe unasoma kimoja kwa miezi sita ujue nod maana kuna tofauti ya Bill Gates na wewe.

0 💬 ⬇️

Usiruhusu tabia hii itawale akili yako

Featured Image

Tabia ya kijidharau na kujiona hufai ama huwezi kufanya lolote ukafanikiwa maishani, hakuna mwanadamu aliyeumbwa ili ashindwe,, sote tu washindi zaidi, tunatofautiana njia za kufikia huo ushindi.

Rafiki yawezekana umeshajidharau… na kujitamkia maneno kadha wa kadha ambayo kimsingi yamekukatisha tamaa kabisa ya kufikia lengo fulani maishani… na ukabaki kushuhudia mafanikio ya wengine kila siku maishani.

0 💬 ⬇️

Ni vizuri kujua haya

Featured Image

👉🏿Degree au vyeti ulivyo navyo haviwezi kukupa mafanikio.
👉🏿Uzuri ulio nao hauwezi kukupeleka kwenye ndoto zako.
👉🏿Usipobadilisha hao marafiki ulio nao hutofika mahali popote.

👉🏿Usipobadilisha vitendo unavyovifanya kila siku hivyo hivyo mafanikio utayasikia kwa wengine.

0 💬 ⬇️

Siri za mafanikio na Jinsi ya kufanikiwa

Featured Image

Tafuta fursa kila kona.
Tumia kipaji chako.
Kuwa na nidhamu katika fedha - matumizi mazuri ya pesa, nidhamu kwa watu wanaokuzunguka, usijikweze, usibague jamii, heshimu wote waliokaribu yako nk.

Kuwa na nidhamu katika afya yako: Afya ndio mtaji sahihi katika biashara yoyote - kuwa na mazoea ya kuangalia afya yako mara kwa mara nk.

0 💬 ⬇️

Jiwekee Utaratibu utakaokuwezesha kuamua vizuri juu ya fedha utakazopata

Featured Image

Jiwekee utaratibu utakaokupa uzoefu wa kuamua vizuri juu ya fedha unazopata. Watu tumekuwa tukitumia fedha tunazopata bila kufikiria jinsi ya kugawa ktk matumiz badala yake baada ya kutumia ndio una/ninaanza kujuta Kwa nin nime/umetumia tofauti na mahitaji uliyonayo. Kiasi cha fedha ulichonacho chaweza kukufanya uwe maskini au tajir kutokana na maamuz unayofanya juu ya hiyo fedha.

0 💬 ⬇️

Uhusiano uliopo kati ya pesa na muda

Featured Image

Bila shaka upo uhusiano mkubwa kati ya pesa na muda..

-Ndio maana nauli ya ndege ni kubwa kuliko ya basi, why..?

Kwa sababu ndege hutumia mda mchache (mf. Ukitoka dar kwenda moshi ni dk45 tu kwa ndege bt kwa gari ni takriban masaa 7-8)

0 💬 ⬇️

Sababu inayopelekea kushindwa kuishi maisha ya ndoto zako

Featured Image
0 💬 ⬇️

Jipe moyo kamwe usikate tamaa

Featured Image

Nilikuwa naangalia mpira wa miguu katika uwanja wa
shule.
Nilipokaa, Nilimuuliza kijana mmoja juu ya Matokeo ya mchezo.

Kwa tabasamu, alijibu "Wako mbele yetu 3-0"!
Nikasema, Kweli!
Mbona huonekani kukata tamaa..?

"Kukata tamaa?
"Yule mvulana aliuliza kwa mshangao…."!?

0 💬 ⬇️

Una thamani gani?

Featured Image

Kazi au shughuli unayoifanya ina thamani gani kwa wengine?unawasaidia au unawaumiza??
Biashara unayoifanya ina thamani gani kwa wengine?ni lazima uwaumize ndipo ufaidike au uwasaidie ili nawe upate faida?

Elimu yako uliyo nayo ina faida au thamani gani kwako na kwa wengine?unawadharau na kujiona wewe ndiye msomi pekee au unawasaidia?

0 💬 ⬇️
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About