Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Angalia pombe ilichomfanya huyu jamaa, kweli pombe haimuachi mtu salama
Updated at: 2024-05-25 16:56:22 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo nimeiogopa pombe.
Nimetokea kuiogopa pombe baada ya kumwona jirani yangu akicheza muziki kwa sauti ya jenereta langu, akidhani yuko clubβ¦..nkamsikia anasema "wee dj noomaaaa"
Baada ya kuzima jenereta akaniuliza uo mziki kaimba nan?
Nlivyokuwa na roho mbaya Nikamwambia iyo ni collabo ya Yamaha na Petrol πππππ
Updated at: 2024-05-25 17:48:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tukiwa kanisani mdada alikuwa amelala , akaamka akasikia Pastor anasema " SIMAMA" Yule dada akasimama akashangaaa kanisa zima linamtizima kwa mshangao akiwemo mumewe, akaangalia kanisa zima akashtuka kujiona yeye peke yake ndiye aliesimama Pastor akaendelea vizur endelea kusimama, tumepata mmoja hadi sasa aliyesimama narudia kwa mara ya mwisho kama hujasikia vizuri " kama wew umewahi kumsaliti au bado unasaliti ndoa yako SIMAMA" Binti akazimia
Huyu bwana leo kapatikana, Jamani nyodo nyingine mbaya
Baada ya kumaliza Degree yake ya sheria Bwana Rwegashora aliamua kurudi nyumbani Bukoba mjini na kufungua ofisi yake kwa ajili ya huduma kwa wateja.
Siku moja akiwa ndani ya ofisi yake alimuona mtanashati na mdada mmoja mrembo anakuja ofisini kwake akajua ni mteja anamletea kesi.
Ndipo akanyanyua mkoni wa wa simu ya TTCL na kuanza kuongea huku anajizunguusha kwenye kiti cha kuzunguuka.
Updated at: 2023-04-29 22:52:17 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Baada ya kumaliza Degree yake ya sheria Bwana Rwegashora aliamua kurudi nyumbani Bukoba mjini na kufungua ofisi yake kwa ajili ya huduma kwa wateja. Siku moja akiwa ndani ya ofisi yake alimuona mtanashati na mdada mmoja mrembo anakuja ofisini kwake akajua ni mteja anamletea kesi.
Ndipo akanyanyua mkoni wa wa simu ya TTCL na kuanza kuongea huku anajizunguusha kwenye kiti cha kuzunguuka. Wakati mdada alipokaribia Rwegashora alimkaribisha kwa ishara maana alijifanya yupo busy na kuongea na simu ya umuhimu. Wakati anaongea na simu akisikika akisema No, No, Noβ¦.. Absolutely No. Wajuulishe hao lay person wa New York kua siwezi kushuhulika na kesi ambayo itanilipa chini ya 50 million. Mimi ni profesional lawyer and im crossing the border to sarve international community.
Aka pose kidogo na akanywa maji kisha akaendeleaβ¦.. Naweza kuanza kukusanya primary evidence next weak but tell them watume kwanza ten million kwa kuanzaβ¦ Hahahahaha you dont know my Account Mr Roger. Ok waambie watume kwenye Account ileile walionitumia million 100 last monthβ¦
Aka pose tena akameza fundo la maji na kurekebisha tai yake kisha akaendelea⦠Ok usisahau kumueleza muendesha mashtaka mkuu wa marekani kua nitakuja New York mwezi ujao maana nitapita kwanza Amsterdam kuwasilisha utetezi wa yule mteja wangu mholanzi kisha nitaenda Tokyo kulipia ile gari yangu niloagiza.
Wakati anaongea hayo yote yule mdada alikua ametulia na anamuangalia Bwana Rwegashora anavyojizunguusha kwenye kiti chake huku akiongea kwa tambo kwenye ile simu ya TTCL. Baada ya kumaliza kuongea na simu Bwana Rwegashora aliweka mkono wa simu yake ya TTCL chini kisha akamgeukia mdada mrembo.
Samahan sana kwa kukupotezea muda wako unajua tena kazi zetu zinaumiza kichwa sana kama unavyoona mwenyewe yaani niko busy sana ninapokea simu sana mpaka nimechoka na simu nyingi ni za wateja wa njee ya nchi.
Anyway nikusaidie nn? Mdada akajibu mimi ni mfanyakazi wa kampuni ya TTCL nimekuja kuunganisha line yako ya simu kwani haipo hewani tangu wiki iliyopitaβ¦!!!
Askari na yeye kumbe muoga, cheki anachomjibu afande
Askari wametumwa nyumba iliyokuwa kuna ugomvi wakafika wakatakiwa kuripoti kwa njia ya simu juu ya walichokikuta
ASKARI: Mkuu tumekuta mama mwenye nyumba kampiga mumewe chuma cha kichwa na kumuumiza vibaya sanaa
Updated at: 2024-05-25 18:08:32 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Askari wametumwa nyumba iliyokuwa kuna ugomvi wakafika wakatakiwa kuripoti kwa njia ya simu juu ya walichokikuta ASKARI: Mkuu tumekuta mama mwenye nyumba kampiga mumewe chuma cha kichwa na kumuumiza vibaya sanaa
AFANDE: Kha! kisa mkasa mpk akafanya hivyo ASKARI: Mama mwenye nyumba alikua anapiga deki mumewe akaingia ndani viatu kabla sakafu haijakauka AFANDE: Sasa mmesha mkamata huyo mwanamke ASKARI: Bado mkuu AFANDE: Kha! sasa mnangoja nini ASKARI: Si tunangoja sakafu ikauke
Updated at: 2024-05-25 17:03:18 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mama mwenye nyumba anajipodoa anashinda saloon kujipodoa lakini house girl hata mafuta usoni hapaki lakini akipita na khanga yake moja tuu nyumba inatetemekaππππππππππππππ huu mchezo hautaki mekapu