Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Unganisha imani na maisha yako kupitia 🙏 Sala, 📜 Masomo ya Misa, 📖 Mafundisho, 💡 Tafakari, 📰 Makala, na 🔐 My System kwa usimamizi wa maisha binafsi. Tunakukaribisha kwenye safari ya kiroho na kimwili!.
Wabongo ni noma! Angalia huyu mbongo anachokifanya
Basi juzi kati hapa sehemu ndogo ya ukuta wa Ikulu ya Magogoni ilianguka!..
Wakapelekwa contractors watatu ili achaguliwe mmoja atakayejenga vzr na kwa bei nafuu!..
Wakwanza alikuwa MUHINDI, wa pili MCHINA na MBONGO!…
Updated at: 2024-05-25 18:02:33 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Basi juzi kati hapa sehemu ndogo ya ukuta wa Ikulu ya Magogoni ilianguka!..
Wakapelekwa contractors watatu ili achaguliwe mmoja atakayejenga vzr na kwa bei nafuu!..
Wakwanza alikuwa MUHINDI, wa pili MCHINA na MBONGO!…
MUHINDI: "ntajenga kwa milioni 90!.., 40 za vifaa, 40 za mafundi na milioni 10 faida yangu"
MCHINA: "mi ntajenga kwa milioni 70!.., 30 za vifaa, 30 za mafundi na milioni 10 faida yangu"
MBONGO kuona vile akamvuta chemba msimamizi wa Magogoni!..
MBONGO: "mi ntajenga kwa milioni 270"
MSIMAMIZI WA MAGOGONI: "we una wazimu nn!.. yaani unathubutu kusema hivyo na unaona wenzako wametaja kiwango kidogo?!."
MBONGO: "milioni 100 zako, 100 zangu alafu hiyo milioni 70 tunaajiri yule mchina"
SOMA HII: Kama wewe ndo baba au mama hapa ungefanyaje!???
Updated at: 2023-04-29 22:52:37 (1 year ago by Melkisedeck Leon Shine)
Bakari ni house boy mara nyingi huiba wine ya boss wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili boss asigundue. Mara kadhaa boss alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika. Ilikua ni bahati tu alimvizia na kumbamba Bakari akichakachua wine, kwa kuwa mkewe alikua anamtetea Bakari, ili kumthibitishia mkewe kuwa Bakari ndo culprit, boss alianza kwa kumuuliza Bakari maswali. Siku hiyo Bakari alikua jikoni,boss na mkewe walikua sebuleni.
Boss:- Bakariiii! Bakari:- Naam baba! Boss:- Nani anakunywa wine yangu?
Boss akaamua amfuate hukohuko jikoni. Boss: Kwanini nikikuita unaitikia, nikikuuliza unanyamaza? Bakari: Baba huku jikoni ndo kulivyo, unasikia jina tu likiitwa lakini maneno menginehusikii, na kama huamini baki jikoni mi niende sebuleni.
Bakari akaenda sebuleni akaanza kuita. Bakari:Babaa! Boss: Naam Bakari! Bakari: Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl? Boss:- kimyaaaa! Bakari:- Baba babaa! Boss:- Ndio Bakari! Bakari:- Nauliza hivii, chumbani kwa house girl saa sita za usiku huwa wafuata nini? Boss:- kimyaaaaaaa!
Boss akatoka nje: Bakari huku jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya jina!. Mama akasema msinizingue nyie…Mbona siwaelewi.. Bakar: mama kama uamini na ww nenda uone.
Mama akaenda jikoni.. Bakari: akaita mamaa Mama : bee bakari Bakari: eti hiyo mimba niya baba au yangu.? Mama kimya Bakari; mama nakauliza tena hiyo mimba niyababa au yangu.
Mama akatoka aisee kweli humu unasikia jina tu…..😄😄😄😄😄
Angalia kilichojiri katika semina ya wanandoa kuhusu upendo
Updated at: 2024-05-25 18:00:09 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kulikuwa na semina ya wanawake kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa. Mwalimu aliwauliza ni wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono kama ishara ya kuwa wanawapenda waume zao. Mwalimu akauliza tena, “Ni lini mara ya mwisho umemwambia mumeo “Nakupenda Mpenzi”?
Majibu yalikuwa kama ifuatavyo: Wengine wakisema Asubuhi ya leo, Wengine jana, Wengine wiki iliyopita Wengine mwezi uliopita Na wengine wakasema hawakumbuki! Mwalimu aliwapa kazi kila mwanasemina achukue simu yake na kumtumia mume wake meseji yenye neno “NAKUPENDA MPENZI” Baada ya meseji kwenda aliwaamuru kubadilishana simu kila mtu na jirani yake. Kila mwanasemina aliambiwa kusoma meseji za majibu kwenye simu aliyoshika
Simu ya 1 – “Samahani, nani mwenzangu”! Simu ya 2 – “Samahani, wrong number”! Simu ya 3 – “Si nimekuambia usinitumie messages kwenye namba hii”! Simu ya 4 – “Mh! leo mvua itanyesha”! Simu ya 5 – “Nikija tutaongea zaidi”! Simu ya 6 – “……Imedhibitishwa umepokea Tsh300,000 kutoka kwa ……”! Simu ya 7 – “Me too”! Simu ya 6 – “Huu ujumbe ndio ulikuwa unamtumia huyo hawara yako ee, leo utanikoma”!
Updated at: 2024-05-25 17:16:07 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo kuna mdogo wangu nimemtumia meseji nimemuomba aniazime chaja yake ya simu. Akanijibu 21002 Nikawa mkali nikamuambia kuchajia mara moja tu ndio HELA yote hio si bora nikanunue Chaja yangu mpya. Akaniambia nimesema TUMIA TU 😂😂mtatuua na lugha zenu😜
Polisi::: hodi, hodi
Jamaa::: kimya
Polisi::: hodi, hodi
Jamaa::: we nani kwani?
Polisi::: sisi polisi
Jamaa::: mnataka nini?
Updated at: 2024-05-25 18:08:23 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Polisi::: hodi, hodi Jamaa::: kimya Polisi::: hodi, hodi Jamaa::: we nani kwani? Polisi::: sisi polisi Jamaa::: mnataka nini?
Polisi::: kuongea na wewe Jamaa::: kuongea na mimi?! Polisi::: ndio Jamaa::: mko wangapi? Polisi::: tuko watatu Jamaa::: kama mko watatu si muongee wenyewe…!!!
Alipelekwa Hospitali na baba yake, baada ya vipimo Doctor akawa anamuandikia dawa, baba yake akatoka nje kuongea na cm.
Mtoto akamwinamia Doctor na kusema kwa sauti ya chini:- "Doctor Kwenye dozi ya dawa niandikie na
Updated at: 2024-05-25 18:06:22 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Alipelekwa Hospitali na baba yake, baada ya vipimo Doctor akawa anamuandikia dawa, baba yake akatoka nje kuongea na cm.
Mtoto akamwinamia Doctor na kusema kwa sauti ya chini:- "Doctor Kwenye dozi ya dawa niandikie na FANTA BARIDII, CHIPS na MISHIKAKI kutwa mara 2 kwa siku 30.