Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
eBooks: Makala za Tafakari za Melkisedeck Leon Shine - AckySHINE
Yafahamu Mawazo na Mipango ya Mungu Kwako
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-06-17 08:14:11 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Mungu daima anawaza Mema na Anampangia Mtu Mambo mema. Kama mtu ataenda katika njia ambayo Ipo katika mipango na mapenzi ya Mungu basi atapokea yale mema Mungu aliyopanga Kwake. Lakini kama mtu ataishi kwa kufuata mapenzi yake mwenyewe basi atapoteza yale mema Aliyopangiwa.
Updated at: 2024-06-17 08:24:01 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Rafiki yangu, Omba utafute uso wa Mungu, Aonaye kwa Siri atakujibu kwa wazi. Mungu ni Mwaminifu Sana hasa kwa wamwombao bila kukoma na kwa matumaini. Mungu yeye anasikia Sala zetu zote na kuzijibu zote.
Mambo ya kutafakari unapokuwa katika shida kubwa, unapoelekea kukata tamaa
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-06-18 07:53:30 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Leo tunatafakari kuhusu wakati wa shida.
Maisha ya mtu yanabadilika wakati wowote kwa namna yoyote yanaweza yakawa mazuri mpaka ukashangaa au yanaweza yasiwe mazuri kama unavyotarajia. Yote hayo ni sehemu ya maisha.
Updated at: 2024-06-18 07:57:56 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Kuwa makini sana na mawazo yako, Yanaweza kukupeleka Mbinguni au motoni.
Kumbuka vile unavyowaza ndivyo utakavyovitenda.
Amua kuwaza mema kutoka ndani ya moyo wako kisha utatenda mema katika maisha yako
Kumbuka Mungu humhukumu mtu kwa mawazo yake maana mawazo ya mtu ndiyo mtu mwenyewe
Tuwaze mema wapenzi ili tuwe wema
Mungu Anakuita Na Kukupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Akusamehe na Kukubariki
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-06-17 03:10:41 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Unaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Moyo Wako wote na kwa nia dhabiti. Mungu atakusamehe dhambi zako na kukufanya kuwa mpya. ...Ingekuwa heri leo usikie sauti yake! Usifanye moyo wako kuwa mgumu.
Updated at: 2024-06-17 17:19:24 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ili kuwa na Amani ya Moyoni unatakiwa uishi kwa kutimiza wajibu wako wa kiroho na kidunia kama inavyotakiwa na kwa uwezo wako wote, Huku ukiwa na Matumaini ya kua kile unachokifanya kitafanikiwa, ni sahihi na umekifanya vizuri.
Kwa nini Mungu hatendi mpaka umwambie au umuombe? Kwa nini tusali?
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-06-17 03:30:49 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Mungu anapenda kutenda jambo baada ya mtu kumuomba/kusali ili mtu aelewe Ukuu wa Mungu na ili Mungu atukuzwe.
Kama kila kitu mtu anachotaka kingekua kinafanyika, Binadamu asingemkumbuka Mungu na Mungu asingetukuzwa
Updated at: 2024-06-17 08:36:28 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Katika fadhila zote, upendo ndio unaonyesha uwepo wa fadhila nyingine
Upendo ni Amri kubwa kuliko zote
Upendo ni Utimilifu wa Sheria
Upendo ni Utakatifu
Updated at: 2024-06-18 10:20:36 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Mwenendo wenu na uongozwe na Roho, nanyi hamtafuata tena tamaa za kidunia. Maana tamaa za kidunia hupingana na matakwa ya Roho; na matakwa ya Roho hupingana na Tamaa za kidunia. Mambo hayo mawili hayaafikiani; kwa sababu hiyo hamuwezi kufanya yale mnayotaka nyinyi wenyewe.
Updated at: 2024-06-18 09:14:48 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Kumtafuta Mungu ni jukumu la mtu binafsi na nafsi yake. Huwezi kumfuata Mungu kwa kufwata njia ya wengine. Njia yako ya kukuwezesha kumfikia Mungu ni tofauti na wengine, Kwa maana Mungu amemwita kila mtu kwa namna ya kipekee.
TAFAKARI KUHUSU NAFASI YA MATESO NA SHIDA KATIKA MAISHA
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-06-17 08:17:40 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Mungu hapendi mtu Ateseke lakini ni kwa njia ya ya Mateso mtu anaweza akapimwa IMANI yake, UNYENYEKEVU, UTII na Matumaini yake kwa Mungu.
Mateso na shida katika maisha ni nafasi ya kujifunza na Kuonyesha unyenyekevu, Imani na Matumaini ya mtu.
Updated at: 2024-06-17 18:38:55 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Fadhila ya Unyenyekevu ni matunda ya Upendo na Uvumilivu kwa hiyo ili kufikia Unyenyekevu yakupasa kuwa na Upendo wa kweli kwa Mungu na Wanadamu huku ukiwa mvumilivu, Mwisho wa yote hayo utapata fadhila ya Unyenyekevu
Vile unavyoweza kuwa DARAJA au KIKWAZO kwa wengine
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-06-17 02:28:40 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Kwa namna unayoishi unaweza ukawa daraja au kikwazo cha wengine kuishi maisha ya Amani raha na fanaka.
Unaweza ukawa daraja kwa maana kwamba wewe unaweza kuwa sababu ya wengine kupata Baraka na neema za Mungu.
Unaweza kuwa kikwazo kwa maana kwamba unaweza kuwa wewe ni sababu ya wengine kutokupata Baraka na Neema za Mungu.
Updated at: 2024-06-18 07:23:24 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Kuna Zawadi moja ya Kipekee ya kumpa mtu ambayo ni Kusali na Kuomwombea Mtu aweze kuingia Mbinguni. Je, ulishawahi kutoa zawadi hii hasa kwa wale unaowapenda? Kila kitu kitabaki hapa duniani na kitapita na kusahauliwa lakini hili halina mwisho
Updated at: 2024-06-17 08:01:41 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Mipango ya Mungu daima ni myema, Mungu anapanga Mema katika maisha ya mtu kama akifuata mapenzi yake. Tatizo ni kwamba watu wanafuata mapenzi yao wenyewe na kisha kukosa yale mema Mungu aliyopanga kwao.
Mungu ni mwenye upendo, Huruma na Rehema hasa kwa Wenye dhambi
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-06-18 07:49:02 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Mungu ni mwenye upendo Huruma na Rehema hasa kwa Wenye dhambi.
Mungu yupo tayari kumsikiliza mtu yeyote mwenye dhambi kama ameutambua, amekiri na Kutubu makosa yake.
Mungu akishamsamehe mtu uovu wake anambariki.
Updated at: 2024-06-18 10:10:24 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Mungu anamakusudi na kila binadamu anayeishi duniani. Hakuna mtu aliyebora zaidi mbele ya Mungu au asiye wa thamani mbele ya Mungu kama anafwata mpenzi ya Mungu.
Karibu Ujitafakari: Kwa nini Unasali na Kumuabudu Mungu? Jifunze Kitu Hapa
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-06-17 03:27:56 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Embu tafakari kwa nini unasali na Kumuabudu Mungu!
Je unasali kwa hofu ya kutokua na uhakika na maisha?
Je unasali kwa sababu ya shida na matatizo katika maisha?
Je unasali kwa kuwa unaona wengine wanasali kwa hiyo unafikiri na wewe lazima usali?
Soma hii, Ujitafakari
Mambo yanayowazuia Waumini na Watumishi wa Mungu Kufikia Ukamilifu na Utakatifu
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-06-17 17:37:01 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Leo nimekuandalia Tafakari kuhusu Mambo yanayowazuia Waumini na watumishi wa Mungu Kuishi Kitakatifu na kufikia Ukamilifu. Mambo haya yanaweza yakaonekana sio dhambi au makosa kwa mtu lakini ni vikwazo kwa mtu kufikia Ukamilifu hasa anaposhindwa kuyajua na kuyaepuka. Wengi wanajiona kwamba wako salama lakini kumbe wako katika dhambi.
Yesu Yupo Karibu na Wewe Unapoanguka Dhambini: Huruma ya Yesu Kristo kwa Mwenye dhambi
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-06-18 07:33:25 (10 months ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Wakati mtu anapoanguka dhambini ndio wakati ambao Yesu anakua karibu na mtu sana hata kuzidi wakati mwingine wowote.
Wakati mtu anapoanguka dhambini ndio Yesu anakua karibu zaidi, lakini tatizo ni kwamba huo ni wakati ambao mtu hawezi kutambua uwepo wa Yesu. Neno moja tuu la Matumaini na Upendo wakati huo linaweza kumfungua mtu na kumbadilisha.