Log in to access your menu with tools for managing ๐ tasks, ๐ฅ clients, ๐ฐ finances, ๐ learning, ๐ personal growth, and ๐ spirituality, all in one place!.
eBooks: Biashara - Mbinu za Ujasiriamali na Biashara Kufanya tofauti - Topic 3 - AckySHINE
USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE
๐ โ
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:03 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kwa lugha nyepesi ni kwamba ukiajiriwa maana yake umeshindwa kujitegemea kwa ujuzi wako (yaani hujui ufanyie nini) hivyo umeona uukabidhi ujuzi wako kwa wenye "akili na uwezo" wa kuupangia matumizi ya huo ujuzi wako.
Ndio maana licha ya kwamba elimu ni yako wewe, maarifa ni yako wewe, vyeti ni vyako wewe; na kazi unafanya wewe; lakini hao waliokuajiri ndio wanakuamulia kiasi gani wakulipe! Si hivyo tu bali pia wanao uhuru wa kukupiga mkwara, kukutishia na hata kukufukuza muda wowote (utakapowakosea, watakapojisikia ama watakapokuchoka)! Nini nakwambia? Kama umeajiriwa, usiridhike wala usibweteke na mshahara pekee kwa 100%, hebu jiongeze aiseee, una uwezo wa kuzalisha zaidi sambamba na mshahara (waliojisikia) kukulipa.
Updated at: 2024-05-23 16:07:25 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Katika mambo ambayo nadhani nimeshawahi kujidanganya ni kufikiri kwamba nikipata kazi ndiyo utakuwa mwisho wa matatizo yangu na kuwa huru kufanya kila kitu ninacho kitaka. ๐๐๐๐๐ Sasaa baada ya kuipata iyo kazi nimekuja kupata ukweli kwamba kumbe kazi ya kuajiriwa siyo Mwarobaini wa Yale niliyo Nayo kumbe ndiyo safari inaanza na siyo mwisho kama nilivyo dhani.
Updated at: 2024-05-23 16:07:18 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ili kutoka hapo ULIPO uweze kwenda HATUA inayofuata kuna SWALI muhimu sana unahitaji kujiuliza. Watu ambao huwa wanashindwa kupiga hatua katika maisha yao ni kwa sababu huwa wanajiuliza kinyume cha swali hili. Swali hili ndilo wanalojiuliza watu wote waliofanikiwa:
Swali: "Hivi kwa sasa nina nini ambacho naweza kuanza kukitumia kama mtaji wa kwanza kuanza kufanya ninachotaka"?
Jifunze kupitia mfano huu Ili uishi kwa amani na watu
๐ โ
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:10 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Siku moja nilichukua taxi aina ya UBER nikiwa naelekea uwanja wa Ndege Mwl. Nyerere Dereva huku akiendesha kwa ustaarabu sana mara ghafla pasipo kutegemea gari ya taka ikajitokeza mbele yetu kutokea nje ya barabara. Dereva wa taxi kwa umakini na neema ya Mungu akalikwepa gari hilo na ilikuwa kidogo agonge gari zingine mbele yetu.