Mizinga ya Kifuniko juu (Top bar)
Hii ni aina ya mizinga inayotumika sana na wengi. Gharama yake ni ndogo kiasi kulinganisha na mingine. Ni aina nzuri sana kwa mtu anaeanza ufugaji wa nyuki kwa kuwa ni wa gharama nafuu. Mfugaji wa nyuki anaweza kutengeneza mzinga Yya aina hii mwenyewe kama ana utaalamu wa useremala.Β

Mzinga wa Langstroth
Mzinga wa Langstroth unaweza kukupatia asali zaidi kulinganishwa na mizinga mingine Hii ni aina nzuri na rahisa sana ya mzinga. Mizinga hii hufahamika kama mzinga wa fremu, kwa kuwa ina fremu ambazo vichane vya masega hujishikiza. Chumba kikubwa ambacho malkia hutagia mayai. Malkia anazuiliwa kuhama kwenda chumba kingine kwa kutumia waya. Kwenye chemba maalumu ya kutagia juu yake pana chemba ya kuhifadhia asali.Β
Β
