Vipimo
Wali:
Mchele mpunga - 4 Vikombe
Tui la nazi - 6 vikombe
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha mchele weka kando.
Bandika tui jikoni likichemka tia mchele na chumvi.
Funika uchemke, tui likikauka wacha moto mdogomdogo hadi wali uive ukiwa tayari. Ikiwa unatumia mkaa unapalia juu yake.
Maharage Ya Nazi
Maharage - 3 vikombe
Tui la nazi zito - 1 kikombe
Tui la nazi jepesi - 1 kikombe
Kitunguu maji - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa -1 kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Chemsha maharage mpaka yaive.
Katiakatia kitunguu maji na tia thomu, tia na tui jepesi kikombe kimoja.
Tia tui zito endelea kuweka katika moto mdogomdogo hadi yakaribie kukauka yakiwa tayari.
Samaki Nguru Wa Kukaanga
Samaki Wa Nguru - 4 vipande
Kitunguu saumu(thomu/galic) & tangawizi ilosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi - 4
Ndimu - 2 kamua
Bizari ya samaki -1 kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Mwoshe samaki kisha mtie kitunguu thomu, tangawizi ilosagwa, chumvi, pilipilimbichi ilosagwa, ndimu na bizari ya samaki.
Mwache akolee viungo kwa muda kidogo.
Makaange katika mafuta hadi aive akiwa tayari.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!