Wali Wa Mpunga
Mchele wa mpunga - 4 Vikombe
Tui la nazi - 6 vikombe
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha mchele kisha
Bandika tui jikoni likichemka tia mchele na chumvi.
Funika uchemke, tui likikauka wacha moto mdogomdogo hadi wali uive ukiwa tayari. Ikiwa unatumia mkaa unapalia juu yake.
Mchuzi wa nyama Ngβombe
Nyama - 1 kilo
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa -2 viijiko vya supu
Viazi/mbatata - 2
Kitunguu maji kilokatwakawa (slice ndogo) - 2
Nyanya/tungule - 4
Nyanya kopo - 3 vijiko vya supu
Majani ya mchuzi/mvu - 3 msongo (bunches)
Bizari ya mchuzi (simba 2) - I kijiko cha chai
Ndimu - 1 kamua
Mafuta - ΒΌ kikombe
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Weka nyama katika sufuri, tia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi, ndimu na chemsha nyama hadi iwive na ibakie supu yake kidogo.
Weka mafuta katika sufuri nyingine, kaanga kitunguu. Vinapogeuka rangi tia majani ya mchuzi endelea kukaanga hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (golden brown)
Tia nyanya/tungule, viazi/mbatata, endelea kukaanga mpaka nyanya ziive.
Tia nyama na supu yake kisha tia nyanya ya kopo, kotmiri, bizari ya mchuzi, chumvi uache mchuzi kidogo katika moto hadi viazi viive vikiwa tayari.
Mboga Mchicha
Mchicha - 4 michano/vifungu
Kitunguu - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 3
Nyanya/tungule - 2
Tui la nazi zito - 1 kikombe cha chai
Chumvi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha mboga iache ichuje maji.
Ikatekate kisha weka katika sufuria.
Katika kitunguu maji, kitunguu thomu kisage au kikatekate kidogodogo (chopped), nyanya.
Weka jikoni ipikike kwa maji yake na mvuke.
Tia tui endelea kuweka katika moto mdogomdogo hadi ikaribie kukauka ikiwa tayari.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!