Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/katoliki/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Tatizo la maumivu wakati na baada ya kufanya mapenzi

Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image
Wakati wa kufanya tendo la ndoa wapo baadhi ya watu hupatwa na maumivu wakati au baada ya kushiriki tendo, Maumivu haya yaweza kuwa;- Wakati tu uume unaingia, Unapoingiza kitu chochote hata kidole, Wakati uume ukiwa ndani na Maumivu ya kupita (throbbing pain) yanayodumu masaa kadhaa baada ya tendo.

Sababu za maumivu

Sababu zaweza kuwa za kimwili (physical) au za kisaikolojia.

Sababu za kimwili baadhi ni kama;

Kutokua na ute wa kutosha kwa ajili ya kulainisha uke kutokana na kukosa maandalizi ya kutosha, kupungua kwa homoni baada ya ukomo wa hedhi, kujifungua au kunyonyesha, baadhi ya dawa za magonjwa ya akili, presha na uzazi wa mpango. Ajali au upasuaji maeneo ya nyonga, ukeketaji na kuongezewa njia wakati wa kujifungua. Pia matibabu ya kutumia mionzi eneo la nyonga.

Tatizo la mishipa ya uke kusinyaa yenyewe (Vaginismus).

Tatizo la uumbaji linalopelekea mtu kuzaliwa wakati uke haujatengenezwa vizuri mfano โ€œvaginal agenesis na imperforate hymen.โ€

Magonjwa ya kizazi kama โ€œendometriosis, PID,fibroids.โ€

Sababu za kisaikolojia;

Msongo wa mawazo, wasiwasi, sonona, matatizo ya mahusiano, woga wa mimba, historia ya kuumizwa kimapenzi (sexual abuse) siku za nyuma.
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Dondoo Muhimu kuhusu ugonjwa wa kisukari

Dondoo Muhimu kuhusu ugonjwa wa kisukari

Wapendwa, napenda kushirikiana na nyinyi kujuzana hili nililolisikia kupitia channel ten leo asub... Read More

Mbinu 11 za kufuata ili uweze kuacha pombe

Mbinu 11 za kufuata ili uweze kuacha pombe

Pombe ni kinywaji kinachotumiwa na watu wengi pasipo hata kufahamu athari zake. Pombe ina athari ... Read More

Ifahamu Saratani ya Tezi Dume, chanzo, Dalili, Uchunguzi na Tiba

Ifahamu Saratani ya Tezi Dume, chanzo, Dalili, Uchunguzi na Tiba

Tezi Dume ni nini?