Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/katoliki/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Faida 25 za kutembea kwa Miguu

Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image
Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamebadili mfumo wa maisha ya watu pamoja na kuathiri afya zao kwa kiasi kikubwa. Hivi leo watu wanatumia vyombo mbalimbali vya usafiri kwenda karibu kila eneo. Kwa hakika kutembea kwa miguu kuna manufaa mengi sana kwa ajili ya afya ya mwili, uchumi na maisha yako ya kijamii.

Ikiwa unapenda kuwa bora na mwenye tija zaidi katika nyanja zote, basi fahamu faida za kutembea kwa miguu.

  1. Hukabili maradhi ya moyo kwa kuhamasisha mzunguko mzuri wa damu.
  2. Huimarisha mifupa.
  3. Huondoa au kupunguza hatari ya kupata kiharusi.
  4. Husaidia kupunguza uzito.
  5. Huzuia saratani ya utumbo mpana.
  6. Hukuwezesha kupata vitamini D kutoka kwenye jua.
  7. Hukusaidia kuboresha usawa wa mwili wako (balance).
  8. Hukabili maradhi ya kisukari. Unapotembea unafanya mazoezi yanayoleta uwiano wa urefu na uzito โ€“ BMI; jambo litakalokukinga na aina ya pili ya kisukari (Type 2 Diabets).
  9. Hukabili shinikizo la damu.
  10. Huondoa msongo wa mawazo.
  11. Huongeza utayari.
  12. Hukufanya ujifunze mambo mbalimbali kwa kuona.
  13. Hukuokolea gharama za nauli au mafuta.
  14. Hupunguza lehemu mbaya mwilini (cholesterol)
  15. Huimarisha misuli.
  16. Husaidia mmengโ€™enyo wa chakula kwenda vizuri.
  17. Huwezesha kinga mwili kujiimarisha na kujijenga (kutokana na sababu kuwa kutembea ni aina ya zoezi).
  18. Huboresha uwezo wa kumbukumbu.
  19. Hukujengea mahusiano ya kijamii. Unapotembea utakutana na watu mbalimbali.
  20. Huzuia kuzeeka. Utafiti uliofanyika ulibaini kuwa watu wanaotembea umbali mrefu huishi zaidi.
  21. Hukuweka katika hali nzuri (mood).
  22. Hukusaidia kulala vizuri. Kumbuka mazoezi ni chanzo cha usingizi mzuri.
  23. Huboresha afya ya uzazi hasa kwa wanaume. Kutembea kama zoezi ni njia ya kuwapa wanaume nguvu katika afya ya uzazi.
  24. Huzuia kuharibika kwa mimba. Mazoezi ni muhimu sana kwa mama mjamzito kwa ajili ya afya yake na mtoto; hivyo zoezi rahisi na jepesi kwake ni kutembea.
  25. Huboresha mwonekano wa mwili. Mazoezi ni njia moja wapo ya kuufanya mwili wako uonekane katika umbo zuri. Hivyo kutembea kama aina mojawapo ya zoezi kunaweza kukusaidia sana.
Naamini umeona jinsi ambavyo kutembea kwa miguu kuna manufaa makubwa sana kwenye afya, uchumi na hata mahusiano yako ya kijamii. Inashauriwa kuhakikisha unatembea kwa miguu angalau dakika 30 kila siku. Kwa njia hii utapata manufaa mengi yaliyotajwa hapo juu.
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Magonjwa hatari 10 yanayotibika kwa kutumia mbegu za Maboga

Magonjwa hatari 10 yanayotibika kwa kutumia mbegu za Maboga

Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya mhimu zaidi mwilini kama madini ya zinki,... Read More

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia kitunguu swaumu

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia kitunguu swaumu

Kitunguu swaumu hujulikana kama kitu cha kushangaza katika tiba huko mashariki ya mbali, Kitunguu... Read More

Matumizi ya kahawa kutibu presha ya kushuka au shinikizo la chini la damu

Matumizi ya kahawa kutibu presha ya kushuka au shinikizo la chini la damu

Kahawa husaidia kuongeza presha au shinikizo la damu. Unashauriwa Kunywa kikombe kimoja cha kahaw... Read More

Madhara ya kisukari kwa nguvu za kiume

Madhara ya kisukari kwa nguvu za kiume

Kulingana na baadhi ya chunguzi zilizofanywa na wanasayansi asilimia 60 โ€“ 70 ya wanaume hupotez... Read More

Vyakula visivyotakiwa kipindi cha ujauzito

Vyakula visivyotakiwa kipindi cha ujauzito

Ili mtoto azaliwe akiwa na afya njema pamoja na akili timamu, akiwa tumboni lazima alishwe lishe ... Read More

Jinsi ya kuongeza kiasi cha utokaji wa maziwa kwa kina mama wanaonyonyesha na kwa afya ya mtoto

Jinsi ya kuongeza kiasi cha utokaji wa maziwa kwa kina mama wanaonyonyesha na kwa afya ya mtoto

Maziwa ni chakula kikuu cha mtoto punde anapozaliwa. Mama anahitaji kuwa na Maziwa ya kutosha ili... Read More

Ifahamu Saratani ya Tezi Dume, chanzo, Dalili, Uchunguzi na Tiba

Ifahamu Saratani ya Tezi Dume, chanzo, Dalili, Uchunguzi na Tiba

Tezi Dume ni nini?