Ni kweli kuwa daktari anaweza kufanya vipimo vya kugundua
kama mtoto aliye tumboni ni mwenye ulemavu au la. Baadhi ya
vipimo hivi ni βultra soundβ ambacho kinawezesha kuona picha ya
umbo la mtoto akiwa bado tumboni. Vipimo vingine vinaangalia
damu. Lakini ualbino hauwezi kugundulika kwa vipimo hivi.
Pia baada ya kuzaliwa daktari ana uwezo wa kutambua kama
mtoto ana ulemavu / hitilafu kama vile moyo, kwenye damu
kama vile βsickle cellβ. Ualbino unaweza kugundulika mara tu
mtoto anapozaliwa au baada ya wiki chache.

Je, ni kweli kuwa ulemavu unaweza kugundulika mara tu mtoto anapozaliwa?

Comments
Please log in or register to leave a comment or reply.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!