Ni kweli hiyo ni dhuluma na inaitwa unyanyasaji wa kijinsia kwa
mtoto. Watoto wanaweza kushawishiwa kwa kutumia hila kwa
mtu mzima anayejaribu kuwavuta ili waweze kujamiiana naye. Na
zaidi wanaweza wasielewe matatizo au madhara watakayopata
kutokana na kujamiiana kwa afya zao pia wanaweza wasiweze
kufanya maamuzi sahihi kwa vile hawana habari.
Mtoto hana uwezo wa kuchunguza mambo katika akili yake
kabla ya kujamiiana.
Uhusiano unaweza pia usiwe sawa kwa vile yule mtu mzima ana
uwezo na nguvu juu ya yule mtoto. Kwa hiyo itakuwa vigumu
kwa mtoto kujadiliana juu ya matumizi ya kondomu .Hizi ndiyo
sababu kwa nini watoto wanahitaji ulinzi maalum. Ni kosa
kujamiiana na msichana wa umri chini ya miaka 18.
Iwapo mtu anajamiiana na msichana chini ya miaka 18 mtu
huyo anawajibika kisheria, katenda kosa hata kama msichana
amempa ridhaa yake.

Iwapo mtu mzima amejamiiana na mtoto na wote wawili wamekubaliana

Comments
Please log in or register to leave a comment or reply.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!