Ukitaka kuelewa jinsi mimba i inavyopatikana, lazima uelewe mzunguko wa hedhi wa mwanamke. Baada ya kuvunja ungo (yaani kupata hedhi kwa mara ya kwanza) msichana hupata hedhi mara moja kila mwezi. Kwa wanawake wengi ni kila baada ya siku 28, hata hivyo wengine huweza kupata hedhi chini au zaidi ya siku hizo.
Siku ya kwanza ya hedhi huhesabiwa kama siku ya kwanza ya mzunguko. Baada ya damu kutoka, yai moja linaanza kukua ndani ya kokwa. Na vilevile utando ndani ya mfuko wa uzazi huanza kujengeka i ili ukaribishe mimba. Kati ya siku 11 au 14 yai hupevuka ndani ya kokwa na halafu husafiri kwenye mrija
wa kupitisha mayai hadi mfuko wa uzazi. Mwanamke anapata mimba kama yai litaungana na mbegu ya kiume ndani ya mrija wa kupitisha mayai. Ina maana kwamba endapo atajamii ana kipindi cha siku chache kabla ya yai kupevuka au siku yai linapopevuka na kutoka kwenye kokwa, linarutubishwa wakati linaelekea kwenye mji wa mimba, na linapofika hapo kwenye mji wa mimba linatulia kwenye utando wa mji wa mimba. Mtoto anahifadhiwa na kukua ndani ya mji wa uzazi mpaka siku ya kuzaliwa. Kama yai halikurutubishwa, basi yai hufa na hutoka pamoja na utando wa mfuko wa uzazi na hutoka nje ya mwili wa mwanamke kama damu ya hedhi. Yaani, mwanamke atapata hedhi kama kawaida na atafahamu kwamba hajashika mimba.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!