Je, mimba hupatikanaje?
Ukitaka kuelewa jinsi mimba i inavyopatikana, lazima uelewe mzunguko wa hedhi wa mwanamke. Baada ya kuvunja ungo (yaani kupata hedhi kwa mara ya kwanza) msichana hupata hedhi mara moja kila mwezi. Kwa wanawake wengi ni kila baada ya siku 28, hata hivyo wengine huweza kupata hedhi chini au zaidi ya siku hizo.
Siku ya kwanza ya hedhi huhesabiwa kama siku ya kwanza ya mzunguko. Baada ya damu kutoka, yai moja linaanza kukua ndani ya kokwa. Na vilevile utando ndani ya mfuko wa uzazi huanza kujengeka i ili ukaribishe mimba. Kati ya siku 11 au 14 yai hupevuka ndani ya kokwa na halafu husafiri kwenye mrija wa kupitisha mayai hadi mfuko wa uzazi. Mwanamke anapata mimba kama yai litaungana na mbegu ya kiume ndani ya mrija wa kupitisha mayai. Ina maana kwamba endapo atajamii ana kipindi cha siku chache kabla ya yai kupevuka au siku yai linapopevuka na kutoka kwenye kokwa, linarutubishwa wakati linaelekea kwenye mji wa mimba, na linapofika hapo kwenye mji wa mimba linatulia kwenye utando wa mji wa mimba. Mtoto anahifadhiwa na kukua ndani ya mji wa uzazi mpaka siku ya kuzaliwa. Kama yai halikurutubishwa, basi yai hufa na hutoka pamoja na utando wa mfuko wa uzazi na hutoka nje ya mwili wa mwanamke kama damu ya hedhi. Yaani, mwanamke atapata hedhi kama kawaida na atafahamu kwamba hajashika mimba.
Ni siku gani katika mzunguko wa hedhi yai linapoweza kurutubishwa?
Yai mmoja hupevuka siku 14 kabla ya hedhi i i inayofuata. Baada ya yai kukomaa ndani ya kokwa la upande wa kulia au wa kushoto, yai husafirishwa kwenye mrija wa kupitisha mayai mpaka kwenye mfuko wa uzazi.
Yai likijiunga na mbegu ya kiume ndani ya mrija wa kupitisha mayai siku zilezile, linaweza kurutubishwa. Yaani, endapo mwanamke anajamii ana kipindi cha siku chache kabla ya yai kupevuka au siku yai linapopevuka anaweza akapata mimba.
Kwa sababu wasichana wengi hawapati hedhi ya kawaida, yaani mzunguko wa siku 28 katika kila mwezi, ni vigumu sana kwao kufahamu tarehe ya hedhi i i inayofuata. Hivyo ni vigumu kujua lini litakuwepo yai linalongojea kurutubishwa.
Mzunguko wa hedhi kwa msichana unaweza kuathiriwa na mfadhaiko, huzuni, safari au mabadiliko mengine katika maisha ya msichana. Hata kama msichana ana mzunguko wa kawaida wa hedhi hali hiyo inaweza kubadilika ghafla na ukawa sio wa kawaida. Wanawake wengi na hasa wasichana hawawezi kutegemea kuhesabu siku kama njia ya kuzuia mimba, kwa sababu hawawezi kuwa na uhakika i iwapo lipo yai linalongojea kurutubishwa au la. Hakuna siku salama za kuepukana na mimba!
Ninaweza kupata mimba wakati nipo kwenye hedhi?
Ili mwanamke aweze kushika mimba, i inabidi yai lililopevuka likutane na mbegu za kiume. Yai pevu linapokosa mbegu hufa na kwa vile utando kwenye tumbo la uzazi ulishajiandaa kupokea yai lililorutubishwa hubomoka. Kwa pamoja, yai na utando hutoka kama damu kupitia ukeni na i le damu huitwa hedhi.
Hedhi ni dalili, kwamba yai halikurutubishwa na hivyo limeshakufa na kutoka. Kwa kawaida, wakati huo halitakuwepo yai jingine lililopevuka kuweza kurutubishwa na kwa hiyo uwezekano wa kupata mimba hautakuwepo. Lakini, mara chache kuna hitilafu katika mzunguko wa hedhi na yai jingine linakuwepo tayari kwa kurutubishwa, hata ukiwa kwenye hedhi. Kwa hiyo uwezekano wa kupata mimba wakati wa hedhi upo, hata kama ni mdogo.
Je, inawezekana msichana akapata mimba kabla ya kuvunja ungo?
Ndiyo, msichana anaweza kupata mimba kabla ya kuvunja ungo, yaani kabla ya kuona hedhi kwa mara ya kwanza. Kwa uhakika utajiuliza kwa nini.
Kabla ya kuona hedhi, yai ndani ya kokwa linapevuka na kusafiri kutoka kwenye kokwa mpaka tumbo la uzazi. Hedhi yenyewe ni dalili kwamba lile yai pevu halikurutubishwa na kwa hiyo linatoka pamoja na utando wa tumbo la uzazi kupitia ukeni.
Kuna maana kwamba hata kama msichana hajavunja ungo, i inawezekana kwamba ndani ya tumbo lake yai limeshaanza kupevuka. Lile yai linaweza kurutubishwa na msichana anaweza kupata mimba, hata kama hajaona hedhi yake kwa mara ya kwanza.
Je, msichana akijamiiana mara moja tu anaweza akapata mimba?
Ndiyo, msichana anaweza kupata mimba akijamii ana mara moja tu. Inategemea na mzunguko wa hedhi. Kama ndani ya tumbo la msichana lipo yai pevu ambalo ni tayari kwa kurutubishwa, na siku i ileile msichana anajamii ana na mvulana anaweza kupata mimba. Isitoshe, anaweza kupata mimba hata kama ni mara ya kwanza ya kujamii ana
No comments yet. Be the first to share your thoughts!