Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI mara nyingi huenea sana kwa njia ya kujamii ana, na hauambukizwi kwa kumhudumia mtu mwenye maambukizi ya Virusi vya UKIMWI au UKIMWI. Hata hivyo ni muhimu kuwa mwangalifu na kuchukua tahadhari ili kuzuia kuambukizwa.
Ukimtibu vidonda vya mtu aliyeambukizwa na Virusi vya UKIMWI, ni vyema kuvaa mipira ya mikononi (glavu ) na daima ni vizuri kufunga kitambaa au plasta mahali penye jeraha. Vifaa vyenye ncha kali vinavyotumiwa na mtu mwenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI, kwa mfano nyembe, kutunzwa sehemu ya pekee na visitumiwe na watu wengine.
Hatua hizi ni muhimu na za msingi kwa wahudumu wa watu wenye virusi vya UKIMWI i ili kuzuia yeye au watu wengine wasipate maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Kama unamtunza / unamhudumia mtu aliyeambukizwa na Virusi vya UKIMWI na huna uhakika au una wasiwasi na tahadhari za kuchukua, unashauriwa kutafuta msaada kutoka kwa mtoa huduma wa afya i li akupe maelezo zaidi.

Ni tahadhari gani nichukue ninapomhudumia mgonjwa wa UKIMWI?

Comments
Please log in or register to leave a comment or reply.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!