Kuna aina mbalimbali za ulemavu na kuna sababu mbalimbali za kuzaa mtoto mlemavu. Ulemavu wa mtoto unaweza kuwa wa kurithi au ukatokea katika hatua tofauti wakati mimba inakuwa, kama vile , wakati wa utungaji mimba, wakati wa ujauzito na wakati wa kuzaa.
Baadhi ya ulemavu ni kwa sababau ya hitilafu ya kinasaba (jenetiki) ambayo tayari i i inajulikana kwenye familia, au inayojitokeza ghafla. Hii ni aina ya ulemavu ambao hauwezi kuzuilika.
Ili mimba i iweze kutungwa, kuna mlolongo wa mambo mengi ambayo yanatakiwa yatokee wakati mwafaka. Ule mwenendo wa kujiunga yai lililopevuka likutane na mbegu ya kiume siyo kitu rahisi na i inawezekana yakatokea makosa. Makosa kama hayo siyo rahisi kuyazuia na mara nyingi kutokea kwake ni kwa bahati mbaya.
Sababu mojawapo ni mwanamke kuumwa wakati wa ujauzito. Kama mwanamke mjamzito anaumwa kwa mfano, malaria na anakunywa madawa makali, ugonjwa wenyewe au matumizi ya dawa yanaweza kuleta madhara kwa mimba i inayokua tumboni. Malaria ni ugonjwa mmojawapo unaosababisha mimba kutoka na ulemavu kwa watoto wanaozaliwa. Wanawake wanashauriwa kuwa wangalifu sana wasiugue malaria wakati wa ujauzito. Sababu nyingine ni matumizi ya madawa ya kulevya, pamoja na sigara au pombe wakati wa ujauzito. Vitu hivi sio vizuri kwa mwili wa binadamu, hasa kwa mimba.
Wakati mwingine, ulemavu wa mtoto unatokea wakati wa kuzaliwa. Kwa hiyo ni muhimu sana mwanamke ahakikishe anahudumiwa na mhudumu mwenye ujuzi wa kutosha ambaye anayajua madhara na namna ya kukabiliana nayo.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!