Hapa Tanzania utoaji wa mimba hauruhusiwi kisheria. Hata hivyo watu wengine wanaamua kutoa mimba kwa sababu mimba zao hazikutarajiwa. Kwa mfano, msichana mdogo ambaye bado anaenda shule, au mama ambaye tayari ana watoto wengi au umri mkubwa sana. Wanawake wengine wanaamua kutoa mimba kwa sababu wamepata mimba kutokana na kulazimishwa kufanya mapenzi au kubakwa, au kwa sababu baba wa mtoto anakataa kuchukua jukumu la kumlea mtoto. Hizi ni baadhi tu ya sababu za kutoa mimba, na kila mwanamke anayeamua kutoa mimba ana sababu zake.
Kwa sababu utoaji mimba hauruhusiwi, huduma za kutoa mimba hazipatikani kwa urahisi na wanawake wengi wanajiamulia kuitoa mimba wenyewe au kwa msaada wa mtu asiyesomea kufanya hivyo. Kama tulivyosema hapo juu, hii ni hatari sana kwa afya ya mwanamke

Kwa nini watu wengine wanaamua kutoa mimba?

Comments
Please log in or register to leave a comment or reply.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!