Nikitafuta rafiki kwa nia ya kuoana (mchumba), je ni sifa gani niangalie kwa msichana/mvulana?
Date: April 17, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Kuchagua mchumba ni moja ya maamuzi ambayo kijana anahitaji kuyafanya kwa uangalifu mkubwa sana. Kwa sababu huyo ndiye atakayekuwa mwenzi wake wa maisha. Katika kuchagua mchumba kila mtu ana mawazo yake kuhusiana na kilicho muhimu kuzingatiwa. Mara nyingi mhemuko una nguvu zaidi kuliko uamuzi wa kimantiki
Hata hivyo, vifuatavyo ni kati ya vigezo ambavyo vinaweza kuangaliwa:
β’ Chagua mtu anayekuheshimu wewe na wengine; Chagua mtu unayemwamini;
β’ Chagua mtu ambaye unaweza kuongea, kujadiliana, na kuhojiana naye kwa uwazi bila kugombana;
β’ Chagua mtu mwenye umri unaokaribiana na wa kwako;
β’ Chagua mtu anayependelea vile unavyopendelea;
β’ Chagua mtu ambaye ataelewa matatizo yako na yuko tayari kukusaidia kuyatatua; na
β’ Chagua mtu mwenye afya nzuri.
Hii inamaanisha pia kumpata mtu ambaye kabla ya kuanza kujaamiana naye, atakuwa tayari kwenda kupima kwa hiari kujua hali yake ya VVU na pia kuwa tayari kutumia kinga kwa maana ya kondomu hadi hapo mtakapojua hali zenu.
Wafahamishe wazazi wako mtu uliyemchagua kama mchumba na mtambulishe kwao i ili wamfahamu na yeye awafahamu wazazi wako. Wakati huohuo na wewe jaribu kuwafahamu wazazi wake. Usifanye uchumba wa haraka. Pata muda wa kutosha kumwelewa rafiki yako.
Please log in or register to leave a comment or reply.
Related Posts
Hakuna mtu wa kulaumiwa, lakini i i inabidi kila mtu awajibike. Kila mtu i inambidi afanye lolote...
Read More
Mapenzi ni kitu muhimu sana katika maisha ya kila mwanadamu, na kwamba uhusiano wa kimapenzi ni s...
Read More
Maana halisi ya neno βbikiraβ ni mwanamke au mwanaume ambaye hajawahi kabisa kujamii ana. Kuj...
Read More
Je, kuna tofauti ya kiumri katika ngono/kufanya mapenzi? Ndio! Kuna tofauti kubwa sana kati ya wa...
Read More
Kuwashirikisha wasichana katika malengo ya pamoja ni jambo muhimu sana katika jamii yetu. Wasicha...
Read More
Kuna baadhi ya vidokezo ambavyo vinaweza kukusaidia:
1. Usikae faragha na mwenzi wako kabla hujawa t...
Read More
Ni vigumu kuelewa nini kinamfanya mtu aweze kubaka mwingine.
Ubakaji ni aina nyingine ya uka...
Read More
Uwezekano wa kuambukizwa virusi vya UKIMWI kwa kunyonyana ndimi ni mdogo sana. Kwa kubadilishana ...
Read More
Ni kweli kwamba kupata hedhi ni dalili ya mwili wa msichana kuwa tayari kwa kubeba mimba, lakini ...
Read More
Kufuatia vitendo vibaya vya mauaji ya Albino, vilivyozuka
Tanzania tangu mwaka 2007 hadi sas...
Read More
Hii ni kweli kabisa. Watu wanaoishi na ualbino ni watu wa
kawaida kama binadamu wengine wote...
Read More
Je, unafikiri ni muhimu kuwa na uelewa wa masuala ya afya na usalama katika ngono/kufanya mapenzi...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!