Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/katoliki/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Namna ya kuvaa vizuri kwa mwanamme upendeze na kuwa mtanashati

Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image
Nimeona leo nitoe darasa kidogo kuhusu mavazi sababu na mimi ni kipaumbele changu katika maisha.

1.Epuka kuvaa marangirangi

Wakati unamatch mavazi jitahidi kupunguza idadi ya rangi, rangi 3 tu zinatosha kukutoa bomba.

2. Vaa kulingana na mazingira/sehemu

Mtu mjanja anajua kubadilika kulingana na mazingira, sio kuvaa jezi la Man utd lenye jina la Wazza kwenye sherehe

3. Masharti ya kuchomekea

-Marufuku kuvaa oversize/undersize -Usivae mlegezo -Hakikisha singlet haionekani -Usivae mkanda mrefu -Usivae makubanzi/sandals

4. Kama umevaa pensi /kaptula.

-Hakikisha unavaa soksi fupi zisizoonekana -Piga raba au makubanzi/sandals bila soksi -Haipendezi kuchemekea

5. Usivae shati jeupe kama la mwanafunzi

Shati nyeupe ni nzuri kama unaijulia wakati unanunua hakikisha ina urembo wa aina yoyote ile au ni ya kimtindo sio kuvaa shati la shule

6. Hakikisha una suruali nyeusi

Mwanaume yoyote yule wa kijanja anajua umuhimu wa suruali nyeusi sababu inamatch mashati ya rangi nyingi.

7. Saa

-Kama umevaa jeans/kadet unaruhusiwa kuvaa saa ya aina yoyote -Kama umevaa suti/suruali ya kitambaa epuka kuvaa saa ya mkanda wa plastic.

8. Miwani

Duh hapa pagumu kidogo lakini cha msingi zingatia muundo wa kichwa chako pamoja na aina ya macho uliyonayo na aina ya pamba ulizovaa pia.Sio umepiga jeans kali,kichwa kama madenge na macho kama bundi kisha unapiga miwani ndogo ya njano,ni

9. Vaa kofia za kijanja

Kofia pia huongeza mvuto,chagua kofia kulingana na aina ya kichwa na mavazi uliyovaa,haipendezi kuvaa suti na kapelo.Kanzu sharti ivaliwe na barakashia ndo utaeleweka la sivyo ni sawa na kuvaa dera tu

10. Mkanda

-Usivae mkanda mrefu km vile umefunga nyoka kiunoni -Mikanda ya vitambaa au madoidoi inafaa kuvaliwa na jeans/kadeti/kaptula -Jitahidi mkumatch rangi ya mkanda na viatu kama umevaa nguo za kuchomekea -Zingatia upana wamkanda na rux za nguo yako

11.Tupia cheni za ukweli

Mikufu ya kiume pia huongeza mvuto -Kama umevaa nguo za kuchomekea au suti itapendeza ukivaa cheni ndogo ambayo haitokezi nje ya shati -Kama umepiga pamba za kishua mfano T.shirt na jeans hapa tupia cheni kubwa lakini hata cheni ndogo zinakubali

12.Uvaaji wa Tai

-Vaa kulingana na urefu wako -Kama wewe mwembamba inapendeza kuvaa tie nyembamba -Jitahidi kumatch tie na rangi ya shirt/suruali -Hakikisha tie yako imefungwa vizuri shingoni

13.T.shirt na Jeans

Wanaume wajanja wa mjini hupenda kupiga t shirt na jeans na chini kutupia raba Kaliโ€ฆ..Vazi hili lina mvuto wa aina yake hasa likivaliwa kitaani na sehemu za mitoko kama vile kwenye Club za starehe.

14. Vaa viatu kijanja

Hapa pia Kuna changamoto -Usivaa suruali ya kitambaa na Raba -Usivae suruali ya kuchomekea na makubanzi -Ukipiga jeans unaweza kumatch t.shirt/shirt na rangi ya viatu -Ukivaa suti yakupasa upige kiatu kikali โ€ฆ.ulikosea itakuwa sawa na Toyota Mark X yenye matairi ya Fuso !!!
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Mambo ya Msingi kujua kuhusu uvaaji wa Tai

Mambo ya Msingi kujua kuhusu uvaaji wa Tai

Kuna mambo mengi ya kufanya ili tuwe watu wa kuvutia kila wakati.Mpangilio wa mavazi hufanya mtu kuo... Read More
Mambo ya kuzingatia kama una ngozi yenye Mafuta

Mambo ya kuzingatia kama una ngozi yenye Mafuta

Ngozi yenye mafuta kwa kawaida huwa inang'ara, nene na yenye rangi iliyotitia. Mara nyingi ngozi ... Read More

Madhara ya Kuvaa/ Kuweka Kope Za Bandia

Madhara ya Kuvaa/ Kuweka Kope Za Bandia

Mapokeo ya urembo wa kisasa katika nchi zinazoendelea ni sehemu ya mchango wa urembo na mvuto tun... Read More

Jinsi ya kuvaa viatu mbalimbali inavyotakiwa na ili upendeze

Jinsi ya kuvaa viatu mbalimbali inavyotakiwa na ili upendeze

Viatu ni kinga kwa ajili ya kuhifadhi miguu. Vile vile viatu ni vazi ambalo linaongeza urembo na ... Read More

Jinsi ya kung'arisha sura yako kwa kutumia Asali, Sukari, Maziwa, na Limao

Jinsi ya kung'arisha sura yako kwa kutumia Asali, Sukari, Maziwa, na Limao

Usafi wa uso ni moja ya mambo muhimu sana kwa mwanamke au mwanaume yeyote yule ambaye anapenda ku... Read More

Faida za kuogea maji ya Moto

Faida za kuogea maji ya Moto

Watu wengi hupendelea kutumia maji ya moto kuoga pale hali ya hewa inapobadilika na kuwa ya barid... Read More

Faida za kutumia mafuta ya Nazi

Faida za kutumia mafuta ya Nazi

Mafuta ya nazi hungโ€™arisha ngozi:

Siyo sehemu za ndani tu ya mwili zinazofaidika na maf... Read More

Mambo ya Kuzingatia ili uwe mrembo siku zote

Mambo ya Kuzingatia ili uwe mrembo siku zote

Katika Jamii nyingi duniani, dhana ya urembo imekuwa na mitazamo tofauti kwa watu wengi. Kila mmo... Read More

Umuhimu wa kuvaa soksi

Umuhimu wa kuvaa soksi

Miguu ni sehemu mojawapo inayotoa jasho sana hivvo ni vema kuiweka mikavu kuzuia ukuaji wa bacteria ... Read More
Namna ya Kuifanya ngozi yako kuwa laini bila Madoa

Namna ya Kuifanya ngozi yako kuwa laini bila Madoa

Ili kufanya ngozi yako kuwa laini bila madoa zingatia mambo haya yafuatayo;

1.TUMIA ANTIOX... Read More

Jinsi ya kuondoa kitambi Kitaalamu

Jinsi ya kuondoa kitambi Kitaalamu

Hapo zamani kidogo tuliona na tulishuhudia watu wakisema ya kwamba mwanaume ambaye ana kitambi nd... Read More

Madhara ya Kuvaa viatu virefu

Madhara ya Kuvaa viatu virefu

NI wazi kuwa viatu virefu huvutia sana vinapo kuwa vimevaliwa.Tulio wengi hasa mabinti au wanawak... Read More

๐Ÿ“– Explore More Articles
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About