Sidebar with Floating Button
AckySHINE Katoliki
AckyShine

Ishara 10 za mwanamke aliyekuzimia na anayekupanda

Featured Image

Ishara hizi zinaweza zikakusaidia kumgundua msichana anayekupenda, wasichana wanatofautiana ila wengi wao wana-share ishara tofauti. Mwanamke anayekupenda hatakosa kati ya hizi


 

Siyo kwamba ishara hizi zote anaweza kuwanazo msichana mmoja, ila kila mmoja kwa ishara zake.


Ishara hizo ni kama ifuatavyo


1. Mnapokutana na kuongea


Msichana anayekupenda anakuwa na tabasamu unapoongea naye kama amekuzoea, ila kama hajakuzoea anapokuona gafla tabasamu hutoweka maana anakuwa na aibu. Hawezi akakuangalia machoni atakuwa anakuangalia kwa kuibia. Sikiliza sauti yake, kama anaona aibu sauti yake itakuwa ya upole/laini anaweza akaanza kushika shika nywele zake au kuweka sawa mavazi yake.


 

2. Ajali za kijitakia


Anaweza akatafuta sababu yoyote ilimradi tu akushike. Anaweza akaona kitu kidogo tu au mdudu halafu anakurukia, au anakukumbatia.


3. Anaibia kukuchunguza


Unapokuwa umetulia zako unakuta anakuangalia kwa kuibia, ukigeuka anajifanya yuko bize na mambo yake kumbe anakuchunguza taratibu.


4. Anapenda mgusane


Mwanamke anayevutiwa na wewe mnapotembea naye mahali anapenda kushika mkono wako, au unapokutana naye anaweza kukukumbatia.


 

5. Anatafuta ukaribu


Mwanamke aliyevutiwa na wewe anapenda kuwa karibu na wewe muda wote. Mfano akiwa na marafiki zake halafu mkakutana gafla atakufuata halafu waangalie marafiki zake utakuta kama wanateta, ukiona hali hiyo kuna siri yao yeye na marafiki zake kuhusu wewe. Anapokuwa na marafiki zake akikuona anaweza akajitenga, hata kama mmeenda out pamoja na marafiki
zake utakuta yupo karibu na wewe.


6. Anapenda umjali


Anapokuwa na tatizo au anajisikia vibaya lazima akuambie, mfano mmeenda mahali kukawa na baridi hata kama si baridi sana atasema anahisi baridi ili mradi umsaidie koti lako, hata kama kuna watu hawezi kuona aibu kuvaa badala yake atajisikia vizuri anapovaa koti lako.


7. Hawezi kuzuia tabasamu


Unapomwonyeshea tabasamu lazima na yeye akuonyeshee, hata kama kuna kitu kimemwudhi atakuonyeshea tabasamu ili mradi aonyeshe umemkuta katika hali ya furaha.


 

8. Ishara za mwili


Anapopita mbele yako anaweza akafanya madoido mengi ambayo yatakuvutia ila kama anajiamini. Kama hajiamini anapokuona gafla anakosa amani, utamwona anashtuka gafla.


9. Anafurahishwa na vituko vyako


Mwanamke anayekupenda daima ni mwenye furaha mkiwa pamoja. Huwezi ukamboa, hata kama ukifanya kituko ambayo haichekeshi utakuta anafurahia.


10. Anakujali


Anakuwa anakujali, mfano akiona umeumia labda umejigonga, yupo radhi akuhudumie. unapokuwa naye anaweza kuuliza "unahitaji chochote? unaweza ukasema "nina kiu ngoja ninunue maji" utamsikia "nina maji, kunywa haya yangu kwanza".basi ujue kwamba anakujali.






Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE




Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke





Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.





[products columns="2" ids="30827"]


AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kukuza na kudumisha afya ya kimwili na akili

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kukuza na kudumisha afya ya kimwili na akili

Kusaidiana na mpenzi wako katika kukuza na kudumisha afya ya kimwili na akili ni jambo muhimu kat... Read More

Jinsi ya Kuunda Mazingira ya Kuwawezesha Watoto kufikia Malengo Yao

Jinsi ya Kuunda Mazingira ya Kuwawezesha Watoto kufikia Malengo Yao

Kuwawezesha watoto kufikia malengo yao ni jambo muhimu sana katika kuhakikisha kuwa wanakuwa na m... Read More

Jinsi ya Kuunga Mkono Kazi na Mafanikio ya Mke wako

Jinsi ya Kuunga Mkono Kazi na Mafanikio ya Mke wako

Kuunga mkono kazi na mafanikio ya mke wako ni muhimu sana katika kujenga uhusiano imara na kuimarish... Read More
Jinsi ya Kujenga Furaha ya Kijinsia baada ya Kuzaa: Kurejesha Ukaribu

Jinsi ya Kujenga Furaha ya Kijinsia baada ya Kuzaa: Kurejesha Ukaribu

Kuzaa ni tukio lenye changamoto nyingi kwa mama na baba pia. Baada ya kuzaa, mama mara nyingi huw... Read More

Kuweka Mazingira ya Kufurahisha na Amani katika Familia Yako

Kuweka Mazingira ya Kufurahisha na Amani katika Familia Yako

  1. Kujenga mahusiano mazuri ya familia ni jambo muhimu katika kuhakikisha kuwa kila mtu an... Read More

Namna ya Kukuza Umoja na Ushirikiano wa Kudumu na mke wako

Namna ya Kukuza Umoja na Ushirikiano wa Kudumu na mke wako

Kukuza umoja na ushirikiano wa kudumu na mke wako ni muhimu katika kujenga ndoa yenye furaha na thab... Read More
Jinsi ya Kuwa na Mvuto wa Kipekee kwa Msichana

Jinsi ya Kuwa na Mvuto wa Kipekee kwa Msichana

Kila mtu anataka kuwa na mvuto wa kipekee kwa msichana. Lakini je, unajua jinsi ya kuwa na mvuto ... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya kijamii na kujitolea

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya kijamii na kujitolea

Mawasiliano ndio msingi wa mahusiano yoyote ya kimapenzi. Kuwa na uwezo wa kuzungumza na mpenzi w... Read More

Mwanamme: Jinsi ya Kuwa na Ushirikiano na Jamii na Wanaume Wenzako

Mwanamme: Jinsi ya Kuwa na Ushirikiano na Jamii na Wanaume Wenzako

Read More
Kuweka Kipaumbele cha Kujifunza na Kukuza Maarifa katika Familia yako

Kuweka Kipaumbele cha Kujifunza na Kukuza Maarifa katika Familia yako

Kujifunza ni jambo muhimu sana katika maisha yetu, na familia ni sehemu muhimu sana ya kukuza maa... Read More

Njia za kuamsha hamu ya kufanya mpenzi ya mwanamke

Njia za kuamsha hamu ya kufanya mpenzi ya mwanamke

Njia za kuamsha hamu ya kufanya mpenzi ya mwanamke au Hatua za kufuata kuamsha hisia za mwanamke ... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Uhusiano Mzuri na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Uhusiano Mzuri na Msichana

Mara nyingi, wanaume wamekuwa wakipata wakati mgumu kuwa na uhusiano mzuri na msichana. Inawezeka... Read More

📘 About 🔒 Login 📝 Register 📞 Contact