Sidebar with Floating Button
AckySHINE Katoliki
AckyShine

Jinsi ya kumfanya mwanamke afurahi na akupende kwa kumfanyia mambo anayoyataka

Featured Image

Kuna mambo ya msingi ambayo mwanamke anahitaji kutoka kwa mwanamme ili kufurahi na kutulia katika mahusiano japokuwa sio rahisi kukwambia mojakwa moja.


Mambo hayo ni kama ifuatavyo;


Kupewa nafasi na kipaumbele.


Wanawake wanapenda kuwa namba moja au kupendwa kuliko yeyote. Kumpenda mwanamke haikuishii kwenye kumpata na kumliki, kisha kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete ya uchumba, ni zaidi ya hapo. Wanawake wanapenda watangulizwe katika mapenzi na kusiwepo na mwingine wa kuchukua nafasi yao katika mazungumzo na mapenzi kwa ujumla na katika maisha yao.


 

Kuheshimiwa


Wanawake wanapenda kueshimiwa kwa maneno na matendo. Wanawake hawapendi kuitwa majina mabaya kwa mfano mjinga, Malaya au kulinganishwa na wanawake wenzao wabaya. Wanawake hawapendi kukosewa heshima hasa mbele za watu, hata kama ni kwa mambo madogo madogo.


Kuridhishwa Kwenye tendo la ndoa


Mwanamke anapenda aridhishwe Kwenye tendo la ndoa. Hata kama utakuwa na kiwango kikubwa cha mapenzi juu ya mpenzi wako kwa kiwango gani, ukiwa dhaifu katika tendo la ndoa utayumbisha penzi lako. Utundu na ufundi unahitajika ili kumkata kiu mpenzi wako. Mwanamme anatakiwa kuhakikisha kuwa anamtosheleza mpenzi wake katika tendo hilo.


 

Nafasi ya kuongea na kujieleza


Wanawake wanapenda wapewe nafasi ya kuongea na kujieleza vile watakavyo. Mpe uhuru mpenzi wako kuzungumza na kumsikiliza bila kumkatiza kwa ukali pale anapoongea sana. Kwa kawaida wanawake wanatajwa kuzungumza maneno 25,000 kwa siku, wakati wanaume wakibaki na kiwango cha maneno 5,000 kwa siku, wanawake hupenda zaidi kujieleza walivyo mbele ya wengine. Kwa hiyo wakizuiwa wasiongee hujiona kama wanakosa nafasi muhimu ya kueleza mawazo yao.


 

Kusaidiwa katika shida na matatizo yao


Wanawake wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi watasaidiwa katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo. Kwa mfano ushauri juu ya maisha yao, kulindwa na hatari za kimaisha, kusaidiwa katika shida na kuongozwa pale wanapohisi kushindwa kufanya jambo. Kama mwanaume hatamfanyia mpenzi wake hili atakuwa amekosa sifa za kuteka penzi la mwanamke.


Kubembelezwa


Wanawake hupenda kubembelezwa hasa pale wanapokuwa na huzuni. Wanawake wengi hupenda kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa. Wanawake hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa.






Mfahamu zaidi Mwanamke kwa Kupitia Kitabu hiki kizuri cha SIRI ZA MWANAMKE




[products columns="2" ids="30827"]


AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, unafaa kujadili historia yako ya ngono/kufanya mapenzi na mwenza wako?

Je, unafaa kujadili historia yako ya ngono/kufanya mapenzi na mwenza wako?

Je, unafaa kujadili historia yako ya ngono/kufanya mapenzi na mwenza wako? Swali hili limekuwa li... Read More

Je, una ndugu wa kiume au wa kike?

Je, una ndugu wa kiume au wa kike?

Habari za leo! Leo tutazungumzia swali ambalo mara nyingi huulizwa kwa watoto wadogo: "Je, u... Read More

Ushirikiano katika Kufanya Mapenzi: Jinsi ya Kuunganisha Hisia za Kimwili na Kihisia

Ushirikiano katika Kufanya Mapenzi: Jinsi ya Kuunganisha Hisia za Kimwili na Kihisia

Hapa ni muhimu kujifunza jinsi ya kuunganisha hisia za kimwili na kihisia kwa ushirikiano katika ... Read More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Kuwa na Urafiki katika Familia Yako

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Kuwa na Urafiki katika Familia Yako

Kuimarisha ushirikiano wa kijamii na kuwa na urafiki katika familia yako ni muhimu sana kwa afya ... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya maendeleo binafsi na ukuaji

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya maendeleo binafsi na ukuaji

Wakati mwingine haifai kuwa mzaha kuhusu kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya maendeleo b... Read More

Jinsi ya kutambua Mahitaji ya Mawasiliano ya mke wako

Jinsi ya kutambua Mahitaji ya Mawasiliano ya mke wako

Kutambua mahitaji ya mawasiliano ya mke wako ni muhimu katika kudumisha uhusiano wenye afya na furah... Read More
Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya upangaji uzazi na familia yenye watoto wachache

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya upangaji uzazi na familia yenye watoto wachache

Kama unapanga kuwa na familia yenye watoto wachache, ni muhimu kujadili suala hili na mpenzi wako... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Msichana Mzuri wa Kuwa Naye

Vidokezo vya Kuwa na Msichana Mzuri wa Kuwa Naye

Vidokezo vya Kuwa na Msichana Mzuri wa Kuwa Naye

Kila mwanaume anapenda kuwa na msichana m... Read More

Jinsi ya Kujenga na kudumisha urafiki na ndugu wa mpenzi wako

Jinsi ya Kujenga na kudumisha urafiki na ndugu wa mpenzi wako

Kujenga na kudumisha urafiki na ndugu wa mpenzi wako ni muhimu kwa kukuza uhusiano wako na mpenzi wa... Read More
Jinsi ya Kufanya Familia Yako Kuwa ya Kipekee na Bora Zaidi

Jinsi ya Kufanya Familia Yako Kuwa ya Kipekee na Bora Zaidi

Kila familia inahitaji kuwa na uhusiano thabiti na wa upendo ili iweze kukua na kuwa bora. Ni muh... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kujifunza katika Mahusiano: Kuwa na Mwelekeo wa Kukuza Maarifa

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kujifunza katika Mahusiano: Kuwa na Mwelekeo wa Kukuza Maarifa

  1. Kuhamasisha ushirikiano wa kujifunza katika mahusiano ni muhimu sana kuwa na mwelekeo w... Read More

Jinsi ya Kuunda Amani na Furaha katika Familia Yako

Jinsi ya Kuunda Amani na Furaha katika Familia Yako

Kuunda amani na furaha katika familia yako ni muhimu sana. Familia ni eneo la usalama, upendo na ... Read More

📘 About 🔒 Login 📝 Register 📞 Contact