Sidebar with Floating Button
AckySHINE Katoliki
☰
AckyShine

Angalia kilichomkuta huyu dada mwenye zarau, mwanae alikufa kwa zarau zake

Featured Image

Dada mmoja akiwa ofisini alipigiwa simu kuwa mwanae amepata ajali wakati anatoka shule, alikuwa ameumia sana. Kwa harakaharaka yule dada aliwasha gari na kuanza safari kuelekea hospitali ili kumuona mwanae.

Akiwa njiani katika mistari ya Zebra huku akiwa na mawazo alitaka kumgonga Kaka mmoja ambaye alikuwa akivuka barabara kwa kukimbia. Katika kumkwepa gari iligonga ukingo wa barabara na kukwaruizika kidogo.

Kwa hasira yule dada alishuka na kuanza kumtukana yule kijana kuwa kamsababishia ajali na kumchelewesha. Alimtukana sana, hali iliyowafanya watu kujaa. Watu walipofika walianza kuuliza nini ndipo yule dada kwa uoga alidanganya kuwa yule kaka alitaka kumuibia.

Watu walianza kumpiga Kaka wa watu kama mwizi, kuona vile yule dada aliingia kwenye gari na kuelekea hospitalini kumuona mwanae. Huku nyuma Polisi walikuja na kumuokoa yule kijana lakini akiwa ameumizwa sana.

Alifika hospitalini na kumkuta binti yake akiwa katika hali mbaya, alikuwa akitakiwa kufanyiwa upasuaji wa haraka ili kuokoa maisha yake, manesi walishamuandaa mtoto na alikuwa akisubiriwa Daktari ambaye alipigiwa simu na alikuwa njiani.

Wakati wakimsubiri Daktari, Nesi alikuja na kuwamabia kuwa, wampeleke hospitali nyingine kwani Daktari waliyekuwa wakimsubiri asingeweza kumfanyia upasuaji mtoto wao kwani alikuwa amepigwa na wananchi wakati akija hospitalini wakimuita mwizi.

Dada na mumewe walichanganyikiwa, mtoto kutokana na hali yake mbaya alichukuliwa harakaharaka na gari la wagonjwa ili kuhamishwiwa hospitalini nyingine. Wakati wanatoka kuelekea kwenye gari kulikuwa na gari ya Polisi inaingia.

Kijana mmoja akiwa hoi alishushwa, yule Dada alimtambua ni yule kijana ambaye alimuitia mwizi kule barabarani. Kwa hasira yule Dada allimuambia Mume wake.
β€œHuyu Kaka namfahamu ni kibaka tu alitaka kuniibia, ndiyo amenichelewesha kufika huku hospitalini!”
Nesi ambaye alikuwa akimsaidia kumpandisha mtoto katika gari la wagonjwa alimkatisha na kusema.
β€œHapana Dada huyu kaka si kibaka, ni Daktari ambaye alipaswa kumfanyia upasuaji mwanao. Amepigwa wakati akikimbia kuja hospitalini, mimi ndiyo nimempigia simu kuja…”

Dada wawatu nguvu zilimuishia ilibidi anyamaze, walifika hospitali nyingine, mtoto alikuwa katika hali mbaya. Aliandaliwa na kuingizwa katika chumba cha upasuaji lakini kabla hajafanyiwa chochote yule mtoto alifariki.

Baada ya uchunguzi ilionekana damu ilishaingia kwenye ubongo. Wangeweza kuokoa maisha yake kama angefanyiwa upasuaji katika hospitali ya mwanzo, kule kusafirishwa tena na kurushwa rushwa barabarani kulisababisha damu kuendelea kuvuja kwa kasi ndani.

Yule dada alizimia baada ya kupata habari zile, maneno yake yalisababisha kuondoa maisha ya mwanae.

FUNZO

Usimdharau mtu kutokana na hali yake kwani hujui ni kitu gani anaweza kukusaidia.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya kutunza heshima yako: Mbinu 15 za kulinda heshima na utu

Jinsi ya kutunza heshima yako: Mbinu 15 za kulinda heshima na utu

Kutunza heshima yako ni muhimu katika kujenga uhusiano mzuri na kuwa na mai... Read More

Misemo 50 ya Uongozi na Ubunifu ya kubadili mtazamo wa maisha yako

Misemo 50 ya Uongozi na Ubunifu ya kubadili mtazamo wa maisha yako

1. "Uongozi ni kuwa mwangalizi wa nyota zinazoongoza wengine kwenye giza." ... Read More

Kama una miaka 24 hadi 29 huu ni ujumbe wako, Soma hii tafadhali

Kama una miaka 24 hadi 29 huu ni ujumbe wako, Soma hii tafadhali

ITAKUSAIDIA KIJANA PLEASE ISOME NA UITAFAKARI

SINTOFAHAMU MAISHANI KATI YA MIAKA 24 HADI 29... Read More

Njia 15 za kukabiliana na chuki za watu

Njia 15 za kukabiliana na chuki za watu

Kukabiliana na chuki za watu ni muhimu ili kujilinda na kuhifadhi afya yako... Read More

MBINU 15 Za jinsi ya kuwa na busara

MBINU 15 Za jinsi ya kuwa na busara

Kuwa na busara ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku. Hapa kuna vidokez... Read More

Misemo 50 ya Uhusiano na Marafiki ya kubadili mtazamo wa maisha yako

Misemo 50 ya Uhusiano na Marafiki ya kubadili mtazamo wa maisha yako

1. "Marafiki ni familia tunayochagua wenyewe." - Unknown

1. "Mafanikio ni matokeo ya kujituma na kutokuacha kamwe." - Unknown

Read More
Jinsi ya kuwa jasiri: Njia 9 za kukuwezesha kuwa jasiri

Jinsi ya kuwa jasiri: Njia 9 za kukuwezesha kuwa jasiri

Kuwa jasiri ni jambo ambalo linaweza kujifunza na kukuza kwa kujitolea. Hap... Read More

Mbinu 15 za kutambua Maadui zako

Mbinu 15 za kutambua Maadui zako

Kutambua maadui zako ni muhimu katika kulinda na kuhifadhi afya yako, ustaw... Read More

Jifunze kupitia mfano huu wa ufutio na penseli ✏

Jifunze kupitia mfano huu wa ufutio na penseli ✏

ΒΆ>PENSELI: "Nisamehe sana"

UFUUTIO: kwa nini? Mbona hujanikosea lolote?

PENSELI: ... Read More

Vitu (6) sita usivyotakiwa kufanya kabla ya kulala

Vitu (6) sita usivyotakiwa kufanya kabla ya kulala

1. USILALE UKIWA UMEVAA SAA.


Saa ya mkononi ina madhara iwapo
utaivaa kwa muda... Read More

Misemo 50 ya Ujasiri na Motisha ya kubadili mtazamo wa maisha yako

Misemo 50 ya Ujasiri na Motisha ya kubadili mtazamo wa maisha yako

1. "Jifunze kushindwa na ujifunze kusimama tena." - Unknown