Familia Kwanza: Wasichana wawili waliwasili kwenye Kikao huku wamevaa nguo ambazo zilikuwa zikionyesha miili yao.
Hiki ndo kitu ambacho Mwenyekiti wa kikao alichowaambia, aliwatazama kwa muonekano mzuri kisha akawataka wakae, kisha akawaambia jambo ambalo hawatoweza kusahau katika Maisha yao.
Aliwaangalia moja kwa moja katika macho yao, kisha akasema;
"Wasichana, kila kitu ambacho MUNGU amekiumba chenye thamani katika Dunia hii kimesitiriwa, na ni vigumu kukiona au kukipata.
1.Wapi unapoipata Almasi?
Ni chini kabisa ndani zaidi katika ardhi, na yamefunikwa na kuhifadhiwa humo
2. Wapi mnapoweza kuipata Lulu? Pia ni ndani zaidi kwenye kina kirefu zaidi katika Bahari, na yamehifadhiwa humo na kujificha ndani ya Sanamu zuri la Baharini
3. Wapi mnapoweza kuipata Dhahabu? napo pia ni ndani zaidi katika Migodi, na yamefunikwa juu na Ardhi za Miamba na ndio uyapate hapo. Yatupasa tufanye kazi ya ziada zaidi na tulime kwa undani zaidi ndipo tuyapate.
Kisha Mwenyekiti akawaangalia wale Mabinti kwa Jicho kali zaidi na kisha akawaambia;
"Miili yenu ni ya kuogopwa na ina thamani sana, na inazidi sana hata thamani ya Dhahabu, Almasi au Lulu. Na yawapasa muihifadhi zaidii.
Kama mtatunza Madini yenu kama ilivyotunzwa Almasi, Dhahabu na Lulu basi Makampuni yenye sifa nzur katika Jamii, Makampuni ya uhakika, Makampuni ya kuaminika yenye Mitambo mizuri yatatenga Muda wa miaka kadhaa katika kufanikisha kuyapata Madini hayo.
Kwanza itawapasa wawasiliane na Serikali (ambayo ndio familia yako) pia kusahihisha Mikatabata muhimu (ndoa) na mwisho ni Mgodi wenye dhana kubwa (ambayo ndiyo ndoa) lakini kama ukiacha madini yako yenye thamani nje hayajahifadhiwa katika uso wa Dunia basi utamvutia kila Mmoja (Mwanaume) na hasa wale ambao ni Wachimbaji haramu watakuja na kuchimba kiharamu (Zinaa), kwa hiyo kila mmoja atachukua kwa vifaa vilivyo na Makali na hivyo ndio watakavyokulima kirahisi.
Hivyo basi nawashauri hifadhini Miili yenu vizuri ili iwavutie wachimbaji wa halali (Waoaji) ndio wakukaribie upate kuheshimika
No comments yet. Be the first to share your thoughts!