Sidebar with Floating Button
AckySHINE Katoliki
AckyShine

Jinsi ya kuongeza mvuto kwa mpenzi wako

Featured Image

Kama umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka. Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.

Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.

UNAFANYAJE SASA?

Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.

Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.

ANZIA MWANZO

Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.

CHUNGA KAULI ZAKO

Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.

Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine. Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.

Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.

USIRUHUSU MAPENZI

Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.

Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.

Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo yoyote – binafsi au yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo yako!

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

[products columns="2" ids="30827"]

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Njia za Kujenga Uhusiano Imara na Msichana

Njia za Kujenga Uhusiano Imara na Msichana

Kujenga uhusiano na msichana ni jambo muhimu katika maisha ya kimapenzi. Uhusiano unapokuwa imara... Read More

Jinsi ya Kusimamia Fedha pamoja na Mke wako

Jinsi ya Kusimamia Fedha pamoja na Mke wako

Kusimamia fedha pamoja na mke wako ni muhimu katika kudumisha hali nzuri ya kifedha na kuepuka migog... Read More
Vidokezo vya Kufanya Msichana Aonekuwa Muhimu katika Maisha Yako

Vidokezo vya Kufanya Msichana Aonekuwa Muhimu katika Maisha Yako

Mwanamke ni hazina kubwa katika maisha ya kila mwanaume. Ni kiumbe chenye thamani, cha thabiti na... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Ukaribu na Kuunga Mkono Maendeleo ya Kila Mwanafamilia

Kuweka Kipaumbele cha Ukaribu na Kuunga Mkono Maendeleo ya Kila Mwanafamilia

Kuweka kipaumbele cha ukaribu na kuunga mkono maendeleo ya kila mwanafamilia ni jambo muhimu sana... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mazingira ya upendo na uaminifu katika ndoa

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mazingira ya upendo na uaminifu katika ndoa

Ndani ya ndoa, upendo na uaminifu ni vitu ambavyo vinatakiwa kujengwa na kudumishwa kila wakati. ... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na changamoto za kusaidia na kuwajali wazee wa familia

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na changamoto za kusaidia na kuwajali wazee wa familia

Kwa wengi wetu, kutunza wazee wa familia ni jambo linaloweza kuleta changamoto kubwa katika maish... Read More

Kufanya Mapenzi Salama na Kuepuka Hatari za Afya: Miongozo na Mbinu

Kufanya Mapenzi Salama na Kuepuka Hatari za Afya: Miongozo na Mbinu

Habari! Karibu kwenye makala hii ambayo itakupa miongozo na mbinu za kufanya mapenzi salama na ku... Read More

Je, ni muhimu kuwa na usawa wa ngono/kufanya mapenzi katika uhusiano?

Je, ni muhimu kuwa na usawa wa ngono/kufanya mapenzi katika uhusiano?

Habari za leo wapenzi! Sijui kama umewahi kujiuliza kuhusu umuhimu wa usawa wa ngono/kufanya mape... Read More

Ushawishi wa Dini katika Maadili ya Kufanya Mapenzi: Kupata Usawa kati ya Imani na Mahitaji ya Kibinadamu

Ushawishi wa Dini katika Maadili ya Kufanya Mapenzi: Kupata Usawa kati ya Imani na Mahitaji ya Kibinadamu

Ushawishi wa Dini katika Maadili ya Kufanya Mapenzi: Kupata Usawa kati ya Imani na Mahitaji ya Ki... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na changamoto za kusaidia na kuwajali watu wenye magonjwa

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na changamoto za kusaidia na kuwajali watu wenye magonjwa

Jambo rafiki yangu! Leo nitakufundisha jinsi ya kuelewa na kukabiliana na changamoto za kusaidia ... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Uhusiano wa Karibu na Kuweka Nafasi ya Wakati wa Familia

Kuweka Kipaumbele cha Uhusiano wa Karibu na Kuweka Nafasi ya Wakati wa Familia

Kuweka Kipaumbele cha Uhusiano wa Karibu na Kuweka Nafasi ya Wakati wa Familia

Kuweka kipa... Read More

Njia za Kusuluhisha Mazungumzo ya Mgawanyiko katika Uhusiano wako na Msichana

Njia za Kusuluhisha Mazungumzo ya Mgawanyiko katika Uhusiano wako na Msichana

Njia za Kusuluhisha Mazungumzo ya Mgawanyiko katika Uhusiano wako na Msichana

Kila uhusian... Read More

📘 About 🔒 Login 📝 Register 📞 Contact