Yesu aliweka Kitubio na Mpako wa Wagonjwa kwa sababu gani?
Yesu aliweka Kitubio na Mpako wa Wagonjwa kwa sababu alijua udhaifu wa binadamu hauishi mara anapopokea uzima wa Mungu kwa sakramenti tatu za kuingizwa katika Ukristo. Hivyo alipanga kusaidia mpaka mwisho wa dunia waamini wake watakaopatwa na dhambi na ugonjwa, kama alivyowasaidia wengi aliokutana nao katika maisha yake.
โYesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, โJipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zakoโโฆ โLakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambiโ โ amwambia yule mwenye kupooza โ โOndoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwakoโ. Akaondoka, akaenda zake nyumbani kwake. Makutano walipomwona, walishikwa na hofu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu amri ya namna hiiโ (Math 9:2,6-8).
Mpako wa Wagonjwa ulianzishwa na nani?
Mpako wa Wagonjwa ulianzishwa na Yesu, kama sakramenti zote. Maandiko yanasimulia huruma yake iliyomfanya awaponye wengi kwa namna mbalimbali na kuwapa Mitume uwezo wa kufanya vilevile kwa โkupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila ainaโ (Math 10:1). Nao
โwakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapozaโ (Mk 6:13).
โMtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa, nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewaโ (Yak 5:14-15).
Mafuta ya mpako wa wagonjwa yanamaanisha nini?
Mafuta ya wagonjwa yanamaanisha lengo la kuwaponya na kuwarudishia nguvu na uzuri.
Kama kawaida, maneno yanaweka wazi zaidi kuwa lengo si kuponya mwili tu, bali hasa roho kwa kuitia msamaha na faraja katika mateso ambayo huenda yakaendelea. Kwa kuwa Mungu haponyi mwili kila mara, isipokuwa kwa faida na wokovu wa mgonjwa na wa wengine. Kama ndiyo mapenzi yake, kila mmoja ajifunze kufaidika vilevile na ugonjwa:
โMakusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi. Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke. Naye akaniambia, โNeema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifuโ. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yanguโ (2Kor 12:7-9).
โSasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu, tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lakeโ (Kol 1:24).
Sakramenti ya Mpako wa wagonjwa ni nini?
Ni Sakramenti ambayo Padri humuombea neema ya Mungu na kumpaka Mafuta Matakatifu mgonjwa aliye katika hatari ya kifo kwa ajili ya neema ya roho na mwili. (Yak 5:14-15, Mk 6:13)
Sakramenti ya Mpako wa wagonjwa ilianza lini? Je, wakati wa Yesu kulikuwa na sakramenti hii?
Sakramenti ya mpako wa wagonjwa ilikuwepo tangu wakati Yesu akiwa hai. Tunaweza kuiona Kwenye Biblia tunaposoma Yesu alivyowatuma wanafunzi wake waliwapaka watu mafuta. "Waliwatoa pepo wengi Wabaya, wakawapaka wagonjwa wengi mafuta wakawaponya. (Marko 6:13)
Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa inaadhimishwaje?
Inaadhimishwa kwa Padre kumuombea mgonjwa, kumuwekea mikono na kumpaka mafuta katika panda la uso na viganja vya mikono; kwa kutumia mafuta aliyobariki Askofu siku ya Alhamisi kuu.
Sakramenti ya Mpako Wa Wagonjwa inamanufaa gani rohoni mwa mtu?
Manufaa ya Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa ni
1. Nguvu ya kuvumilia mateso na kuyaunganisha na mateso ya Yesu Kristo
2. Maondoleo ya dhambi zote asizoweza kuziungama
3. Nafuu ya mwili, hata uzima ikifaa kwa wokovu wa roho yake
4. Neema ya kujiandaa kuaga dunia na kuingia katika uzima wa milele
2. Maondoleo ya dhambi zote asizoweza kuziungama
3. Nafuu ya mwili, hata uzima ikifaa kwa wokovu wa roho yake
4. Neema ya kujiandaa kuaga dunia na kuingia katika uzima wa milele
Ni nani anayetoa Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa?
Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa hutolewa na kuhani tuu yaani Askofu au Padri
Padri aitwe kwa mgonjwa lini?
Padri aitwe kwa mgonjwa mara inapoonekana Hatari ya Kifo na kamwe isisubiriwe mpaka mgonjwa apoteze fahamu.
Ni nani aweza kupokea Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa?
Ni kila Mkatoliki aliyefikia umri wa kufikiri na aliye katika hatari ya kufa kwa ugonjwa au uzee aweza kupokea Sakramenti hii.
Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa yaweza kupokelewa mara ngapi?
Sakramenti hii yaweza kupokelewa mara nyingi ugonjwa ukizidi au akipatwa na ugonjwa mwingine mkubwa
Alama wazi ya Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa ni nini?
Alama wazi ya Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa ni tendo la kupaka Mafuta Matakatifu wagonjwa na kutamka maneno
"Kwa mpako huu Mtakatifu na kwa pendo lake kuu, Bwana Akujaze na nguvu ya Roho Mtakatifu. Amina Akuondoe katika enzi ya dhambi, akuweke huru. Kwa wema wake akupe nafuu katika mateso yako na kukujalia neema. Amina"
Kama padri hatapatika na mgonjwa afanye nini?
Kama padri hatapatikana mgonjwa aweke nia ya kuungama na afanye majuto kamili
Komunyo pamba ndio nini?
Komunyo pamba ndio Ekaristi inayopokelewa na wale wanaokaribia kuaga maisha ya duniani na wanaojiandaa kuvukia uzima wa milele
Paul Ndomba (Guest) on July 1, 2024
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
Jane Muthoni (Guest) on May 3, 2024
Rehema zake hudumu milele
Stephen Amollo (Guest) on February 28, 2024
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
Agnes Lowassa (Guest) on August 16, 2023
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
Stephen Malecela (Guest) on July 2, 2023
Katika imani, yote yanawezekana
George Tenga (Guest) on May 18, 2023
Nguvu hutoka kwa Bwana
Edward Lowassa (Guest) on October 17, 2022
Mungu akubariki!
Paul Kamau (Guest) on July 23, 2022
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
Ruth Mtangi (Guest) on June 18, 2022
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
Nora Lowassa (Guest) on April 11, 2022
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
Monica Lissu (Guest) on March 19, 2022
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
Grace Mushi (Guest) on March 12, 2022
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
Peter Mbise (Guest) on November 10, 2021
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
Catherine Naliaka (Guest) on November 3, 2021
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
Nancy Akumu (Guest) on August 29, 2021
Wakati wa Mungu ni kamilifu
Lydia Mutheu (Guest) on August 24, 2021
Nakuombea ๐
Rose Amukowa (Guest) on April 28, 2021
Rehema hushinda hukumu
John Lissu (Guest) on December 14, 2020
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
Janet Wambura (Guest) on December 9, 2020
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
Charles Mboje (Guest) on September 13, 2020
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
Emily Chepngeno (Guest) on April 8, 2020
Mungu ni mwema, wakati wote!
Peter Tibaijuka (Guest) on March 6, 2020
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
Paul Kamau (Guest) on January 4, 2020
Endelea kuwa na imani!
Victor Kamau (Guest) on December 1, 2019
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
Anna Malela (Guest) on September 28, 2019
Kwa Mungu, yote yanawezekana
Benjamin Masanja (Guest) on September 27, 2019
Mwamini katika mpango wake.
Joyce Mussa (Guest) on June 9, 2019
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
Patrick Akech (Guest) on December 31, 2018
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
Frank Macha (Guest) on November 20, 2018
Sifa kwa Bwana!
Nora Lowassa (Guest) on November 2, 2018
Baraka kwako na familia yako.
Esther Cheruiyot (Guest) on September 25, 2018
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
Henry Sokoine (Guest) on September 25, 2018
Imani inaweza kusogeza milima
Joyce Mussa (Guest) on August 26, 2018
Tembea kwa imani, si kwa kuona
George Ndungu (Guest) on February 7, 2018
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Grace Wairimu (Guest) on December 31, 2017
Dumu katika Bwana.
Samson Mahiga (Guest) on December 5, 2017
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
Joyce Nkya (Guest) on September 9, 2017
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
Nancy Kabura (Guest) on April 17, 2017
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Ruth Kibona (Guest) on February 23, 2017
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
Peter Tibaijuka (Guest) on January 28, 2017
Tumaini ni nanga ya roho
John Mushi (Guest) on January 23, 2017
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
Paul Kamau (Guest) on October 4, 2016
Mwamini Bwana; anajua njia
Lydia Mzindakaya (Guest) on September 30, 2016
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
Rose Kiwanga (Guest) on September 6, 2016
Neema ya Mungu inatosha kwako
Frank Macha (Guest) on July 30, 2016
Neema na amani iwe nawe.
Victor Malima (Guest) on April 9, 2016
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
Joseph Kitine (Guest) on March 1, 2016
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
Isaac Kiptoo (Guest) on January 25, 2016
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
Hellen Nduta (Guest) on November 23, 2015
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
Thomas Mtaki (Guest) on September 28, 2015
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia