Ishara ndogo ya Msalaba juu ya panda la uso, mdomo, na kifua kabla ya Injili ina maana gani?
Maana yake ni kama Ahadi kuwa, Niko tayari kulifahamu Neno la Mungu kwa akili yangu, Nitalitangaza kishujaa kwa Midomo yangu, Nitalipenda na kulishika kwa Moyo wangu wote.
Je ni dhambi kukosa Misa Jumapili?
NDIYO. Ni dhambi kubwa kukosa Misa kwa Makusudi siku ya Jumapili/Dominika na Sikukuu zilizoamriwa.
Sakramenti ya Ekaristi ni nini?
Sakramenti ya Ekaristi ni Sakramenti ya Mwili na Damu ya Yesu Kristo, aliye kweli katika Maumbo ya Mkate na Divai. (Yoh 6:1-17, Mt 26:26-28)
Ni wakati gani katika Misa Mkate na Divai vinageuka Mwili na Damu yake Kristo?
Ni katikati ya Misa padri asemapo maneno Matakatifu aliyosema Yesu mwenyewe: "HUU NDIO MWILI WANGU; HII NDIO DAMU YANGU"
26 Walipokuwa wanakula, Yesu akatwaa mkate, akamshukuru Mungu, akaumega, akawapa wanafunzi wake akisema, βTwaeni mle; huu ni mwili wangu.β 27 Kisha akatwaa kikombe cha divai, akashukuru, akawapa akisema, βKunyweni nyote; 28 maana hii ni damu yangu inayothibitisha agano, damu inayomwagwa kwa ajili ya watu wengi ili kuwaondolea dhambi. 29 Nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka siku ile nitakapoinywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.β
30 Baada ya kuimba wimbo, wakaondoka, wakaenda katika mlima wa Mizeituni. (Mat 26:26-30)
Je Sakramenti ya Ekaristi hujulikana kwa majina yapi?
Majina haya;
1. Ekaristi Takatifu
2. Karamu ya Bwana
3. Misa Takatifu
4. Sakramenti Takatifu ya Altare
5. Komunyo Takatifu
6. Sadaka Takatifu
7. Kumega Mkate
Baada ya Mitume kufa ni nani wanafanya Sakramenti ya Ekaristi
Badaa ya Mitume kufa Maaskofu na Mapadri wanaendelea kuadhimisha Sakramenti ya Ekaristi Takatifu
Ni lini Yesu Kristo aliwapa Maaskofu na Mapadri Uwezo wa kugeuza mkate na divai kuwa Mwili na Damu yake?
Yesu Kristo aliwapa Maaskofu na Mapadri Uwezo wa kugeuza mkate na divai kuwa Mwili na Damu yake alipowafanya Mitume kuwa Mapadri katika karamu ya mwisho aliposema "FANYENI HIVI KWA UKUMBUSHO WANGU" (Lk 22:14-20)
Misa ni nini?
Misa ni sadaka safi ya Wakristo kwa Mungu, ndiyo sadaka ya Agano Jipya ambayo
Kristo kwa njia ya Padri anamtolea Mungu Baba mwili na damu yake katika umbo la mkate na divai kama alivyojitolea mwenyewe juu ya msalaba.
Sadaka ya Msalaba ni nini?
Sadaka ya Msalaba ni tendo la mateso na kifo cha Bwana wetu Yesu Kristojuu ya Msalaba pale Kalvari
Ni kwa nini Sadaka ya Misa Takatifu ni Sadaka ile ile ya Msalaba?
Sadaka ya Misa Takatifu ni ile ile ya Msalaba kwa sababu ni sadaka moja tu, kuhani na kafara ni yule yule.
Tofauti ni namna tu yankuitoa hiyo sadaka. (1Kor 11:26, Ebr 9:14,25-28)
Pale msalabani damu ilimwagika lakini katika Ekaristi damu haimwagiki tena
Misa Takatifu hutolewa kwa nani?
Misa Takatifu hutolewa kwa Mungu Baba Mwenyezi (Ebr 5:1-10, Law 9:7).
Yesu aliweka sadaka ya Misa Takatifu kwa makusudi gani?
Yesu aliweka sadaka ya Misa Takatifu ili;
1. Amtolee Baba sadaka bora siku zote
2. Atujalie mastahili yake Msalabani
3. Azilishe roho kwa neema za sadaka hiyo. (Ebr 5:1-10, 7:27).
Sadaka ya Misa Takatifu yatolewa kwa nia gani?
Sadaka ya Misa Takatifu yatolewa kwa nia ya kumwabudu Mungu, kumshukuru, kujipatanisha nae na kumwomba. (Ebr 9:14)
Misa Takatifu hutolewa kwa ajili ya nani?
Misa Takatifu hutolewa kwa ajili ya kanisa nzima yaani kwa ajili ya watu wote wazima na wafu. (Ebr 9:14. Rum 1:9)
Kutolea Misa kwa Marehemu maana yake ni nini?
Kutolea Misa kwa Marehemu ni kutolea Misa kwa ajili ya roho zilizoko toharani ili ziweze kuingia mbinguni
Misa Takatifu ina sehemu kuu ngapi?
Misa Takatifu ina sehemu kuu mbili
1. Litrujia ya Neno
2. Liturujia ya Ekaristi
Litrujia ya Ekaristi ina sehemu kuu ngapi?
Litrujia ya Ekaristi ina sehemu kuu tatu
1. Matayarisho ya vipaji
2. Sala ya Ekaristi
3. Ibada ya Komunyo
Ni vitu gani vya msingi na vya lazima katika kuadhimisha Ekaristi Takatifu?
Vitu vya lazima katika kuadhimisha Ekaristi Takatifu ni
1. Mkate wa Ngano
2. Divai ya mzabibu
Kabla ya Kupokea Ekaristi Takatifu Tunasali sala gani?
Tunasali "Ee Bwana sistahili uingie kwangu lakini sema neno tu na roho yangu itapona"
Katika Ekaristi Takatifu Tunampokea nani?
Katika Ekaristi Takatifu Tunampokea Yesu Kristo Katika Maumbo ya Mkate na Divai na tunaungana naye (Yoh 6:57)
Mkristo awe katika hali gani kabla ya kupokea Ekaristi Takatifu?
1. Awe na Neema ya Utakaso yaani asiwe na dhambi ya mauti.
2. Awe na Imani, Ibada na Kumtamani Yesu.
3. Afunge chakula Muda wa saa Moja na Kileo zaidi ya masaa matatu.
4. Awe safi kimwili.
5. Awe na adabu na heshima.
Komunyo Takatifu Hutuletea neema gani?
1. Hulinda na kuongeza neema ya Utakaso iliyo uzima wa roho zetu.
2. Hutuondolea dhambi ndogo na kupunguza hatari ya kutenda dhambio kubwa.
3. Hututia bidii na nguvu ya kutenda mema kwa kutuongezea Imani, Matumaini na Mapendo.
4. Huleta Umoja katika Kanisa, sio sisi na Kristo tuu bali sisi kwa sisi.
Mkristo akipokea Ekaristi Takatifu akiwa na dhambi rohoni anatenda dhambi gani?
Mkristo akipokea Ekaristi Takatifu akiwa na dhambi anatenda dhambi kubwa yaani kufuru Sakramenti.
26 Maana kila mnapokula mkate huu na kukinywa kikombe hiki, mwatangaza kifo cha Bwana, mpaka atakapokuja. 27 Kwa hiyo, kila aulaye mkate huo au kunywa kikombe cha Bwana bila kustahili, atakuwa na hatia dhidi ya mwili na damu ya Bwana. (1 Kor 11;26 - 27)
28Basi, kila mtu ajichunguze mwenyewe kwanza, ndipo ale mkate huo na anywe kikombe hicho; 29 maana anayekula na kunywa bila kutambua maana ya mwili wa Bwana, anakula na kunywa hukumu yake yeye mwenyewe. 30 Ndiyo maana wengi kati yenu ni dhaifu na wagonjwa, na wengine kadhaa wamekufa. 31 Kama tungejichunguza wenyewe vizuri hatungeadhibiwa hivyo. 32Lakini tunapohukumiwa na Bwana, tunafunzwa tuwe na nidhamu, ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu. (1 Kor 11;28 - 32)
Je, Kanisa linahimiza waamini wapokee Ekaristi wakati gani?
Kanisa linahimiza waamini wapokee Komunyo Takatifu kila siku wanaposhiriki Misa
Nani Mhudumu wa adhimisho la Ekaristi Takatifu?
Mhudumu wa adhimisho la Ekaristi Takatifu ni Askofu na Padre
Je, Mkristo akipokea kipande cha Hostia amempokea Yesu Mzima?
Ndiyo, Amempokea Yesu Mzima kabisa, Hata akipewa zaidi ya hostia moja amempokea Yesu Mzima
Sakramenti ya Ekaristi Takatifu Huifadhiwa wapi?
Sakramenti ya Ekaristi Takatifu Huifadhiwa kwenye Tabernakulo
Tabernakulo ni nini?
Tabernakulo ni mahali Patakatifu anapokaa Yesu wa Ekaristi siku zote
Sakramenti ya Ekaristi Takatifu hukaa Tabernakulo kwa sababu gani
Sakramenti ya Ekaristi Takatifu hukaa Tabernakulo kwa ajili ya watu wote hasa wagonjwa
Ishara wazi ya Sakramenti ya Ekaristi Takatifu ni nini?
Ishara wazi ya Sakramenti ya Ekaristi Takatifu ni maumbo ya mkate na divai, na maneneo ya mageuzo ya Yesu mwenyewe Padri akiyatamka.
Baada ya kumpokea Yesu wa Ekaristi tufanye nini?
Baada ya kumpokea Yesu wa Ekaristi: Tumwabudu,tumshukuru, tumwombe kwani yeye ni Mwenyezi. (Mt 2:11, Lk 17:11)
Frank Macha (Guest) on June 8, 2024
Nakuombea π
Samuel Were (Guest) on March 16, 2024
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
Robert Ndunguru (Guest) on December 14, 2023
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
David Ochieng (Guest) on July 20, 2023
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
Janet Mbithe (Guest) on May 17, 2023
Neema na amani iwe nawe.
Lydia Mutheu (Guest) on May 10, 2023
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Lydia Mahiga (Guest) on December 13, 2022
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
Vincent Mwangangi (Guest) on October 31, 2022
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
Richard Mulwa (Guest) on September 26, 2022
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
Alice Wanjiru (Guest) on September 2, 2022
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
Richard Mulwa (Guest) on August 18, 2022
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
Agnes Lowassa (Guest) on August 9, 2022
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
Grace Mushi (Guest) on June 30, 2022
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
Vincent Mwangangi (Guest) on April 16, 2022
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
John Kamande (Guest) on November 14, 2021
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
John Lissu (Guest) on June 13, 2021
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
Esther Cheruiyot (Guest) on May 24, 2021
Mwamini Bwana; anajua njia
Linda Karimi (Guest) on May 14, 2021
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
Peter Mwambui (Guest) on April 14, 2021
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
John Lissu (Guest) on April 1, 2021
Tembea kwa imani, si kwa kuona
Tabitha Okumu (Guest) on September 15, 2020
Mwamini katika mpango wake.
Janet Wambura (Guest) on July 20, 2020
Neema ya Mungu inatosha kwako
Vincent Mwangangi (Guest) on May 18, 2020
Baraka kwako na familia yako.
Monica Nyalandu (Guest) on April 17, 2020
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
Grace Mligo (Guest) on April 5, 2020
Dumu katika Bwana.
Betty Akinyi (Guest) on March 16, 2020
Nguvu hutoka kwa Bwana
Jane Muthoni (Guest) on February 8, 2020
Mungu akubariki!
Grace Mushi (Guest) on October 16, 2019
Wakati wa Mungu ni kamilifu
Martin Otieno (Guest) on July 19, 2019
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
Peter Mwambui (Guest) on July 14, 2019
Mungu ni mwema, wakati wote!
Alice Wanjiru (Guest) on February 26, 2019
Katika imani, yote yanawezekana
Anna Kibwana (Guest) on January 28, 2019
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
David Kawawa (Guest) on December 30, 2018
Sifa kwa Bwana!
John Mwangi (Guest) on November 30, 2018
Endelea kuwa na imani!
Janet Mwikali (Guest) on June 9, 2018
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
Sarah Achieng (Guest) on June 7, 2018
Kwa Mungu, yote yanawezekana
Jackson Makori (Guest) on March 3, 2018
Rehema hushinda hukumu
Lydia Mahiga (Guest) on February 9, 2018
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Joseph Njoroge (Guest) on November 9, 2017
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
Faith Kariuki (Guest) on April 29, 2017
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
David Kawawa (Guest) on March 14, 2017
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
Lucy Mushi (Guest) on December 19, 2016
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
Peter Otieno (Guest) on November 21, 2016
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
Lucy Wangui (Guest) on July 12, 2016
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
David Kawawa (Guest) on June 1, 2016
Tumaini ni nanga ya roho
Samuel Were (Guest) on May 27, 2016
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
Agnes Njeri (Guest) on April 13, 2016
Rehema zake hudumu milele
Patrick Kidata (Guest) on August 25, 2015
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
David Nyerere (Guest) on July 29, 2015
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
George Mallya (Guest) on July 3, 2015
Imani inaweza kusogeza milima