Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia mvuke
Welcome Back.
Updated at: 2024-05-25 10:37:33 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mvuke husaidia kusafisha ngozi. Ni rahisi sana kutumia mvuke kutibu chunusi.
Chemsha maji kwenye sufuria jikoni funika na uache nafasi kidgo ya mvuke uwe unatoka, kisha chukua taulo na ujifunike usoni huku ukisogelea karibu na mvuke unapokea na uruhusu mvuke huo ukupate kwa mbali.
Baki hapo kwa dakika 5 mpaka 10 hivi huku ukiwa umetulia (relaxed). Huu mvuke utakusaidia pia kujisikia mtulivu na kukuondolea mfadhaiko wa akili.
Mwishoni mwa zoezi jisafishe uso wako na maji ya baridi.
Endelea kusoma makala hii kujifunza zaidi dawa nyingine za asili za kutibu chunusi.
Updated at: 2024-05-25 10:35:12 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipo vitu mbalimbali ambavyo mama mjamzito hapaswi kuvitumia wakati wa ujauzito kwani vina athari kubwa sana kwake yeye mwenyewe pamoja na mwanaye aliye tumboni.
1. Matumizi ya Pombe wakati wa ujauzito huathiri mtoto hivyo hairuhusiwi kabisa kutumia kwa kipindi hicho.
2. Uvutaji Sigara.
3. Kupunguza unywaji wa kahawa au vinywaji vyenye caffeine nyingi.
4. Samaki aina ya papa, swordfish, tilefish na king mackerel kwani wana mekuryi kwa wingi amabayo ni mbaya kwa afya.
Updated at: 2024-05-25 10:35:34 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Zabibu huweza kutumika kama tiba ya shinikizo la chini la damu kama ifuatavyo
Updated at: 2024-05-25 10:37:29 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
1. Fanya mazoezi ya viungo kwa saa moja kila siku
2. Kunywa maji mengi kila siku
3. Ondoa mfadhaiko (stress)
4. Weka homoni sawa kama hazipo sawa
5. Kuwa msafi wa mwili wote kila mara
6. Usiziguse chunusi au kuzitoboa na mikono yako au na chochote kuepuka makovu yasiyo ya lazima
7. Epuka vyakula vifuatavyo kama unasumbuliwa na chunusi kila mara, navyo ni pamoja na:
a)Vyakula vyenye mafuta sana
b)Vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi
c)Kahawa
d)Chai ya rangie)
e)Pombe na vilevi vingine
f)Chokoleti
g)Popcorn
h)Maziwa
i)Mapera
j)Vyakula vya kwenye makopo
k)Pizza
Updated at: 2024-05-25 10:35:29 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wakati wa ujauzito ni kipindi cha kubadili mambo mengi katika mfumo wa maisha wa mjamzito. Mjamzito anapaswa kubadili mambo mbalimbali ili kuhakikisha anakua na afya nzuri katika kipindi chote cha ujauzito na ili kuhakikisha kwamba atajifungua mtoto mwenye afya nzuri. Moja ya mambo makubwa ni pamoja na tabia ya kuvaa viatu vyenye visigino virefu. Mjamzito hashauriwi kuvaa viatu vyenye visigino virefu kutokana na athari zinazoweza kutokana na aina hizi za viatu.
Mjamzito akivaa viatu vyenye visigino virefu anakua katika hatari kubwa ya kuanguka. Hii huweza kusababisha majeraha makubwa kwa mtoto aliyeko tumboni hali inayoweza kusababisha mimba kutoka.
Wadada hupenda kuvaa âhigh heelsâ husababisha misuli ya mapaja kukaza na kuwa na muonekano mzuri. Katika ujauzito, mabadiliko ya homoni huweza kupelekea misuli hii kuwa na maumivu tofauti na ilivyokua kabla ya ujauzito.
Ni wazi kuwa uzito huongezeka wakati wa ujauzito na mabadiliko ya vichocheo vya mwili huweza kupelekea kizunguzungu cha hapa na pale. Hii huongeza hatari ya kuanguka iwapo utavaa âhigh heelsâ na kupelekea majeraha kwako na kwa mtoto aliyeko tumboni.
Uvimbe miguuni.
Ni jambo la kawaida miguu kuvimba wakati wa ujauzito. Kuvaa viatu vyenye visigino virefu na vyenye kubana huweza kuongeza tatizo hilo na kupelekea maumivu.
Wakati wa ujauzito, uzito mkubwa huhamia mbele na misuli ya nyonga hulegea. Mabadiliko haya ya kimsawazo huweza kusababisha maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo na kiuno.
Iwapo kuna ulazima sana wa kuvaa viatu hivyo, unapaswa kuzingatia yafuatayo:
Updated at: 2024-05-25 10:35:27 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tezi dume (prostate), ni tezi iliyo kwenye kizazi cha mwanaume inayozalisha maji maji yanayobeba manii/shahawa. Inaizunguka urethra, mrija unaotoa mkojo kwenye kibofu kwenda nje. Tezi dume ya kila mwanaume huongezeka ukubwa kadri umri unavyoongezeka. Kadri tezi inapokua na kuongezeka ukubwa,inaweza kukandamiza urethra na kusababisha matatizo ya kibofu na matatizo ya kukojoa. Tezi dume inapoongezeka ukubwa huitwa âbenign prostatic hyperplasiaâ kwa kifupi âBPHâ. Hii sio saratani, na haiongezi hatari ya kupata saratani ya tezi dume.
Saratani ya tezi dume inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vinavyotokana na kansa kwa wanaume duniani. Pia ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wenye umri wa miaka 70 na kuendelea. Hata hivyo, satarani ya tezi dume kwa sasa inawapata sana wanaume kuanzia miaka 25. Lakini kabla ya kuendelea mbele hebu kwanza tujue tezi dume ni zipi.
Kama tulivyosema neno saratani ni jina la gonjwa ambalo hutokea wakati chembe chembe za uhai au seli katika sehemu fulani ya mwili zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili na kutengeneza vijiuvimbe vidogo vidogo. Kwa kawaida seli huwa zinajigawa, kupevuka na baadaye kufa kwa kufuata taratibu za mfumo wa mwili. Lakini seli za saratani hazifuati mfumo huo. Badala ya kufa, zenyewe huishi muda mrefu kuliko chembe chembe za kawaida na wakati huo huo huendelea kutengeneza seli nyingine na kuwa uvimbe wa saratani au tumour.
Tezi dume linapatikana katika mwili wa mamalia dume tu na pale seli katika kiungo hicho zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili hapo ndipo mtu hupata saratani ya tezi dume. Ugonjwa huu pia hujulikana kama saratani ya kibofu cha mkojo. Saratani ya tezi dume huwapata wanaume tu na hasa wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea. Kutokana na tafiti mbali mbali, saratani hii imethibitika kushika nafasi ya pili, ukiachia mbali saratani ya mapafu kwa kusababisha vifo vya wanaume wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea.
Tafiti za Chama cha Saratani cha Marekani (ACS) na cha Afrika Kusini (CANSA) zimebaini kuwa, mwanaume mmoja kati ya sita hupata saratani ya tezi dume katika uhai wake. Kutokana na takwimu za mwaka 2010 za dunia nzima, malaria iliua watu laki tano, kifua kikuu watu milioni 2.1, Ukimwi watu milioni 1.8 na saratani watu milioni 9.9. Kwa mujibu wa takwimu hizo, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ugonjwa wa saratani ni kubwa ikilinganishwa na ya magonjwa mengine. Dk Emmanuel Kandusi ambaye ni miongoni mwa waathirika wa saratani hiyo, na mwanzilishi wa kampeni ya kuangamiza saratani ya tezi dume nchini Tanzania ya '50 Plus Campaign' anasema kuwa, ugonjwa huu ukitambuliwa mapema huweza kutibika kwa urahisi. Ameongeza kuwa, kutokana na ugonjwa huo kuwa hatari nchini, ifikapo mwaka 2020 unatarajiwa kuua watu milioni 20.
Kuna vihatarishi vingi vinavyochangia mwanamume kupata saratani ya tezi dume. Vifuatavyo ni baadhi yake:-
đđżKwanza kabisa ni umri. Nafasi ya kupata saratani ya tezi dume huongezeka sana hasa ukifikia umri wa karibu miaka 50 na kuendelea.
đđżNasaba ni kihatarishi kingine ambapo wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zao wamewahi kuugua ugonjwa huu huwa katika hatarini ya kupata kansa hiyo kutokana na kurithi jeni za ugonjwa huo.
đđżSuala jingine ni lishe ambapo wanaume wanaopenda kula nyama au (red meat) na walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama huwa katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume.
Vilevile wataalamu wanatumbia kuwa, wanaume wasiopenda kufanya mazoezi, wanene na wenye upungufu wa virutubisho vya Vitamin E pia wako kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya kibofu cha mkojo.
Wanaume wengine walio katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume ni pamoja na wale wenye asili ya Afrika (Weusi) ikilinganishwa na wazungu, wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea za kemikali, wanaofanya kazi katika viwanda vya kutengeneza matairi na wachimbaji madini, hususan aina ya cadmium.
Hayo yote yakiwa ni tisa, kumi ni je, dalili za saratani ya tezi dume ni zipi?Katika hatua zake za awali, dalili za saratani ya tezi dume hazitofautiani na zile za kuvimba kwa tezi dume au BPH.
Dalili hizo ni pamoja na,
1) Kupata shida wakati wa kuanza kukojoa.
2) Kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa.
3) Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu.
4) Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku.
5) Kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote
6) kutoa mkojo uliochanganyika na damu.
Pamoja na kueleza dalili hizo watu wanapashwa kutambua kuwa, mwanaume anapoanza kuona na kuhisi baadhi ya dalili hizo, anapaswa kujua kuwa, seli za saratani katika tezi dume lake huwa zina umri wa takribani miaka saba na kuendelea.
Iwapo saratani imesambaa mwilini kiasi cha kuhusisha sehemu nyigine za mwili, mgonjwa anaweza kuwa na maumivu makali ya mifupa katika maeneo ya nyonga, mapajani na kiunoni.
Aidha mgonjwa huwa na dalili nyingine zinazoweza kumpata mgonjwa mwingine yeyote wa saratani kama vile kupungua uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu, kizunguzungu na kadhalika.
Wanaume wanashauriwa kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya kibofu cha mkojo au prostate cancer kwa kuwa imegundulika kuwa wanaume wengi wakiziona na kuzihisi dalili hizo huona soni kwenda kumwona daktari na kufanyiwa uchunguzi.
Baadhi ya watu huzihusisha na magonjwa ya zinaa au na dhana potofu za kishirikina. Wapo wanaokwenda mbali zaidi hata kuuita ugonjwa huo kuwa ni wa walawiti huku wengine wakiurahisisha kwa kuuita kuwa ni ugonjwa wa utu uzima kana kwamba saratani ya tezi dume ni jambo la kawaida kwa watu wazee.
Mambo kama hayo hupelekea wanaume wengi kujinyanyapaa wenyewe na hata wengine kujitibu kwa uficho au kwa kutumia waganga wababaishaji mpaka pale mambo yanapokuwa yamewazidi ndipo hupelekwa mahospitalini na mara nyingine huwa wamechelewa na kupoteza maisha yao bure kwa ugonjwa ambao ungeweza kutibiwa mapema.
Kwa ajili hiyo tunatoa wito kwa wanaume kutoona soni na kuwa na tabia ya kufanyiwa uchunguzi wa afya kwa ujumla, na hasa tezi dume angalau mara moja kwa mwaka.
Kuna vipimo viwili ambavyo daktari anaweza kumpima mwanaume ikiwa ni hatua ya kwanza ya kugundua ugonjwa huo. Vipimo hivyo vya kwanza ni "Digital Rectal Exam (DRE)" na cha pili ni "Prostate Specific Antigen (PSA)". DRE pamoja na PSA huonesha uwepo wa tatizo kwenye tezi dume, lakini vipimo hivi havina uwezo wa kutofautisha iwapo tatizo hilo linamaanisha saratani au uvimbe katika tezi dume. Hivyo basi, ili kuweza kutofautisha kati ya magonjwa hayo mawili, kipimo kiitwacho Prostate biopsy hufanywa. Baada ya vipimo hivyo kama vitaashiria saratani ya tezi dume basi daktari anaweza kuamuru vipimo vingine ili kuthibitisha uwepo wa ugonjwa huo kama vile transrectal ultrasound au prostate needle biopsy.
Kuna njia kadhaa za matibabu ya saratani ya tezi dume. Hata hivyo uamuzi wa njia gani itumike unategemea ushauri na maoni ya daktari kulingana na hatua ya ugonjwa ulipofikia na umri wa mgonjwa husika. Katika hatua za awali za ugonjwa, daktari anaweza kushauri mgonjwa atibiwe kwa kufanyiwa upasuaji na tiba ya mionzi.
Hii ni katika hali ambayo kwa wagonjwa wazee, daktari anaweza kushauri mgonjwa kuwa chini ya uangalizi tu bila kufanyiwa upasuaji au bila kupatiwa tiba ya mionzi.
Alpha 1-blockers kama vile doxazosin, prazosin, tamsulosin, terazosin, na alfuzosin ni dawa zilizo kwenye kundi la dawa zinazotumika kutibu shinikizo la juu la damu. Dawa hizi hulegeza misuli ya shingo ya kibofu na tezi dume. Hii huruhusu mkojo kutoka kwa urahisi. Watu wengi wanatumia dawa ya Alpha 1-blockers, na husaidia sana kupunguza dalili zao.
Finasteride na dutasteride  ni dawa zinazopunguza kiwango cha homoni zinazotengenezwa na tezi dume,hupunguza ukubwa wa  tezi dume, huongeza kiwango cha mtiririko wa mkojo, na kupunguza dalili zinazotokana na ukubwa wa tezi dume kuongezeka. Inaweza kuchukua miezi 3 hadi 6 kabla ya kuona mabadiliko makubwa katika dalili zako. Kutumia finasteride na dutasteride kunaweza kuwa na athari kama vile, kupungua kwa nguvu za kiume na hata kuwa hanithi.
Daktari anaweza kuagiza upewe dawa za antibiotiki ili kutibu kuvimba kwa tezi dume (prostatitis), mara nyingi prostatitis huambatana na kuongezeka kwa ukubwa wa tezi dume.
Upasuaji wa tezi dume unaweza kupendekezwa  iwapo :
Uchaguzi wa aina maalum ya upasuaji, mara nyingi hutegemea ukali wa dalili ,ukubwa na umbo la tezi dume.
Iwapo saratani imesambaa na kuathiri sehemu nyingine za mwili, matibabu yake yanaweza kujumuisha upasuaji wa kuondoa korodani, matumizi ya dawa za kupunguza kiwango cha homoni ya testosterone katika damu au hormonal therapy, au matumizi ya kemikali za kuua seli za saratani (chemotherapy).
Tukumbuke kuwa, saratani ya tezi dume ni ugonjwa wa kawaida kama yalivyo magonjwa mengine na uchunguzi na matibabu ya mapema huweza kuokoa maisha ya waathirika wengi wa ugonjwa huo.
Updated at: 2024-05-25 10:35:30 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wakati mafuta ya nazi yakiwa yamemengâenywa na mwili huhamasisha uundwaji wa nguvu mpya za ubongo zijulikanazo kama âketonesâ.
Ketones zina uwezo wa kusambaza nguvu katika ubongo hata kama insulin itakuwa chini ya kiwango kama matokeo ya ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
Insulin kazi yake kubwa ni kuishughulikia sukari (glucose) na hivyo kuzipa nguvu seli za ubongo.
Ubongo wa mtu mwenye ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu hauwezi kujitengenezea insulin yake kwa usahihi na vya kutosha. Kwa hiyo inashauriwa kutumia mafuta haya.
Mafuta ya nazi yanao uwezo wa kupigana na seli za kansa. Tafiti za karibuni zinasema kitu chochote chenye uwezo wa kuuongezea nguvu ubongo husaidia pia kuzuia kusambaa kwa seli za kansa katika mwili.
Zaidi ni kuwa mafuta haya yana uwezo wa kumdhibiti bakteria ajulikanaye kama âhelicobacter pyloriâ ambaye husababisha vidonda vya tumbo.
Kuongeza kinga ya mwili ni moja ya faida za mafuta ya nazi sababu ni mafuta ambayo hupigana dhidi ya bakteria, fangasi na virusi mbalimbali.
Paka moja kwa moja juu ya ngozi au kuyanywa pia kuchanganya kwenye vyakula mbalimbali kwa ajili ya kuongeza kinga yako ya mwili.
Mafuta ya nazi yana asidi mafuta nzuri zenye uwezo wa kusaidia na kuzilinda seli za ubongo na kuziwezesha kufanya kazi kwa ufasaha zaidi.
Mafuta ya nazi yanajulikana vizuri kwa uwezo wake wa kukuongezea uvumilivu yaani stamina.
Mafuta ya nazi ni dawa ya mba na mara nyingine hutumika kwa kuchanganywa na mafuta mengine
Ni mazuri kwa ngozi na yanatibu magonjwa mbalimbali ya ngozi.
Mfuta ya nazi yanaweza kuzuia mpaka asilimia 20 ya miale ya jua kushindwa kukufikia moja kwa moja kwenye ngozi yako kama utayafanya kuwa ndiyo mafuta yako ya kupakaa.
Wengi mnapenda kufanya scrub hasa usoni (facial). Kwa lugha nyepesi ni kitendo cha kusugua ngozi kwa dawa maalumu ili kuondoa uchafu wote na kuifanya ionekane nyororo na yenye kupendeza.
Sasa huhitaji dawa zenye kemikali kwa ajili hiyo wakati mafuta ya nazi yanaweza kukusaidia hilo bila madhara yoyote mabaya.
Fanya hivi changanya nusu kikombe (mln125) cha mafuta ya nazi na sukari kikombe kimoja na ufanye dawa ya kusugua na kusafisha uso wako.
Unaweza pia kutumia nazi yenyewe moja kwa moja kabla hujapata mafuta yake.
Tumezoea kutumia nazi jikoni kwenye mapishi, lakini nazi pia inaweza kutumika kama scrub ya asili ya ngozi yako.
Fuata hatua hizi zifuatazo ili kufanya ngozi ya uso wako iwe laini, nyororo na kufanya uso wako uwe laini, nyororo na wenye mvuto.
Scrub hii unaweza pia kuitumia kwa mwili mzima, lakini hapa nitaelezea namna ya kutumia kwa uso wako.
*Safisha uso wako kwa maji safi na sabuni ya kawaida isiwe sabuni ya dawa (medicated)
*Ukishamaliza hapo, utakaa hivyo bila kuuosha uso wako kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.
Ili kupata matokeo mazuri fanya hivi kwa muda wa siku 5 mfululizo bila kuacha, yaani mara moja kwa siku.
Amini nakuambia utapata matokeo mazuri mpaka mwenyewe utaifurahia ngozi yako na hata vocha utaninunulia kunipongeza.
Unatakiwa kupakaa tu sehemu yenye tatizo moja kwa moja huku ukinywa kijiko kidogo kimoja kila siku na hutakawia kupona hivyo vidonda.
Yanangarisha kucha na kuzikinga na wadudu.
Mafuta ya nazi Yanaweza kutumika kama dawa ya asili ya kufukuza wadudu (insect repellent) wakiwemo mbu. Unachohitaji ni kuchanganya pamoja na kiasi kidogo cha mafuta ya karafuu au ya mnanaa (mint) na ujipake juu ya ngozi yako na hakuna mdudu yoyote akiwemo mbu atakayekusogelea.
Mafuta ya nazi yana viondoa sumu vyenye nguvu zaidi ambavyo vinaweza kuulinda mwili wako dhidi ya vijidudu nyemelezi.
Zaidi, matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kurahisisha umengâenywaji wa madini ya kalsiamu tumboni mwako.
Upungufu wa madini ya kalsiamu mwilini husababisha mifupa kuwa hafifu jambo linaloishia kuleta ugonjwa wa mifupa (osteoporosis).
Kuzuia ugonjwa wa mifupa unahitaji kuongeza mafuta ya nazi kuwa sehemu ya chakula chako. Hii ndiyo faida ya mafuta ya nazi ambayo niliona si vema kama sitakuambia.
Watu wenye vitambi au unene uliozidi wanatakiwa kuongeza mafuta ya nazi kwenye milo yao na miili yao itakaa sawa yenyewe.
Matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kusaidia mafuta kuchomwa zaidi mwilini huku kiasi chako cha njaa kikishuka.
Mifadhaiko ni jambo lisiloweza kuepukika katika maisha yetu. Kazi ya mfadhaiko au stress ni kukufanya uwe imara zaidi, mpole na unayejiamini zaidi.
Unapofadhaishwa mwili wako huwa unajiongeza na kuwa na shauku ya kufanikiwa zaidi. Hata hivyo mfadhaiko unapodumu kwa muda mrefu unaweza kuleta madhara makubwa kwa mhusika kihisia na hata kimwili pia.
Mfadhaiko wa muda mrefu unaweza kupelekea huzuni mbaya na hatimaye kuathiri muonekano wako.
Watu wenye mifadhaiko (stress) ya muda mrefu huonekana ni wenye umri mkubwa hata kama umri wao bado ni mdogo.
Tafiti za karibuni zimeonyesha uhusiano wa karibu uliopo kati ya matumizi ya mafuta ya nazi na kupungua kwa mfadhaiko wa akili.
Tunaweza kusema kuwa, kitendo hiki cha kuondoa mfadhaiko au stress ni moja ya kazi ya kustajaabisha kabisa ya mafuta ya nazi. Asidi mafuta zilizomo ndani ya mafuta haya ndizo zinazohusika na kazi hii mhimu.
Ili mwili wako ubaki ni wenye afya na kuzuia usipatwe na magonjwa unahitaji kuwa na mfumo mzuri wa mmengâenyo wa chakula na wakati huo huo mfumo imara wa uchukuwaji wa viinilishe, madini na vitamini mbalimbali kutoka kwenye chakula unachokula.
Kwa bahati nzuri, kuuongezea nguvu mfumo wa mmengâenyo wa chakula ni kazi nyingine ambayo mafuta ya nazi yanaweza kukusaidia bila madhara mengine mabaya.
Matumizi ya mafuta ya nazi yatakuwezesha kuongeza uchukuwaji wa viinilishe mhimu kutoka kwenye chakula sababu mafuta haya yana madini ambayo huweza kuyeyuka kwenye mafuta kama kalsiamu na magnesiamu.
Zaidi, mafuta haya yanaweza kusaidia umengâenywaji wa mafuta mengine magumu ndani ya mwili kama matokeo ya kuimarishwa kwa vimengâenya vinavyohusiana na mmengâenyo wa chakula.
Kama unapata maumivu au matatizo yoyote katika kongosho au kibofu cha mkojo unahitaji kuongeza matumizi ya mafuta ya nazi.
Ukiendelea kutumia mafuta ya nazi kila mara utaweza kujitibu pia tatizo la mawe katika kibofu cha mkojo na kuondoa hali ya kutojisikia vizuri kutokana na magonjwa katika kongosho au kibofu cha mkojo.
Faida kubwa ya mafuta ya nazi haiishii katika uwezo wake wa kuchoma mafuta, bali yana kazi nyingine ya kushangaza zaidi nayo ni kutengeneza misuli ya mwili.
Kwenye bidhaa nyingi zinazouzwa zaidi duniani za kutengeneza virutubishi vya kutengeneza misuli ya mwili mafuta ya nazi lazima yawemo.
Kama unataka kuongeza misuli mingi mwilini kirahisi zaidi changanya tui zito la nazi kikombe kimoja (robo lita), ongeza vanilla vijiko vikubwa vitatu, ongeza maji maji ya chungwa vijiko vikuwa viwili na ndizi zilizoiva mbili.
Saga na mashine ya kusagia matunda jikoni (blender) mchanganyiko huu kwa pamoja na ule wote kutwa mara 1 kila siku.
Kuzuia kuoza kwa jino na magonjwa ya fizi ni moja ya kazi nyingine nzuri ya kushangaza ya mafuta ya nazi ambayo nimependa kukufahamisha kupitia makala hii.
Mafuta ya nazi ni dawa inayoweza kudhibiti bakteria wabaya na hivyo kuzuia kuoza kwa jino na maumivu mengine katika fizi. Ili kuzuia haya unahitaji tu kutumia mafuta yako ya nazi kama dawa yako ya mswaki kila siku.
Unaweza pia kuongeza kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto ili kutengeneza dawa ya kusafisha mdomo (mouthwash).
Kwa mjibu wa madaktari wengi, kuna uhusiano wa karibu kati ya madhara ya figo na kushindwa kufanya kazi kwa ogani hii mhimu.
Kama tatizo la kufeli kwa figo halitapatiwa ufumbuzi linaweza kupelekea kifo. Figo na Ini ni ogani mhimu zaidi katika mwili ambazo zinatakiwa kupewa uangalizi wa karibu kila mara zisipatwe na madhara yoyote.
Kwa bahati nzuri, mafuta ya nazi yanayo uwezo wa kulinda figo na Ini visipatwe na madhara yoyote mabaya moja ya kazi ya mafuta ya nazi mwilini ulikuwa huijuwi bado.
Wanasayansi wameviona viinilishe katika mafuta ya nazi ambavyo ni mhimu sana kwa afya ya Ini na figo katika mwili wa binadamu.
Nazi pamoja na mafuta ya nazi huwa na asidi mafuta mhimu sana ambazo huhamasisha uundwaji wa âMonooctanoinâ ambayo hufanya kazi ya kuyeyusha mawe katika kibofu cha mkojo na figo.
Wagonjwa ambao hawawezi kumudu gharama za upasuwaji kuondoa mawe katika figo na katika kibofu cha mkojo wanaweza kujitibu hilo kwa kutumia mafuta ya nazi kama dawa mbadala.
Unachohitaji kufanya ni kunywa tu kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi kila siku kutwa mara 1 mpaka utakapokuwa umepona.
Mafuta ya nazi hudhibiti uvimbe na kuondoa sumu mwilini, kazi hizi mbili zinayafanya kuwa dawa bora ya kutibu ugonjwa wa baridi yabisi.
Unahitaji kijiko kidogo kimoja cha mafuta haya kila siku ili kujitibu na ugonjwa wa baridi yabisi.
Faida za mafuta ya nazi zinahusu pia kurekebisha kazi za ogani za mwili kama kuweka sawa mapigo ya moyo, kupumua na kuzalisha homoni mhimu.
Tezi koromeo huzalisha homoni mbili ambazo huwa na msaada mkubwa katika kuongeza nguvu katika mfumo wa mmengâenyo wa chakula.
Ufanisi mzuri wa tezi hii huweza kuhakikisha mapigo ya moyo ni sawa, uzito sawa wa mwili, na usawa ulio sawa wa homoni.
Kutibu kisukari aina ya kwanza ni moja ya kazi nyingine nzuri za mafuta ya nazi sababu mafuta haya yanao uwezo wa kuiweka sawa damu sukari (blood glucose) ndani ya mwili.
Mafuta ya nazi yamethibitika siyo katika kushusha kisukari aina ya kwanza tu bali pia katika kuweka sawa aina mbalimbali za homoni mwilini.
Kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi kwa siku kinatosha kwa kazi hii.
Mafuta ya nazi ni moja ya dawa nyingine nzuri kwa ajili ya kutibu maambukizi ya fangasi kwa sababu moja kuu kwamba ni mafuta yanayoweza kuua bakteria na virusi mbalimbali.
Hii ni kazi ya mafuta haya ambayo isingekuwa vema kama nisingekujulisha kupitia makala hii. Hii ni matokeo ya kuwa na âlauric acidâ na âcapric acidâ.
Tafiti mbalimbali zimeonyesha uhusiano uliopo baina ya matumizi ya mafuta yenye afya na kushuka kwa maambukizi ya fangasi.
Kwa fangasi yoyote juu ya ngozi unaweza kutumia mafuta haya kama mafuta yako ya kupakaa kila siku pia unaweza kunywa kijiko kidogo kimoja kila siku kuongeza kinga zaidi ya mwili.
Maradhi mengi mwilini huja kama sababu ya homoni zako kutokuwa sawa. Ni bahati kufahamu kuwa mafuta ya nazi ni moja ya dawa za asili nzuri katika kuziweka sawa homoni zako.
Hii ni kwa sababu mafuta ya nazi yana mafuta mazuri yajulikanayo kama âlauric acidâ. Mafuta ya nazi huiweka sawa homoni mhimu sana kwa upande wa uzazi kwa mwanamke homoni ijulikanayo kama âestrogenâ. Chanzo kingine kizuri cha homoni hii ni pamoja na tunda la parachichi.
Kuzeeka mapema ni jambo lisilopendwa karibu na watu wote. Kuzeeka mapema hakuathiri muonekano wako tu bali huathiri pia afya yako.
Tunapozungumzia juu ya faida za kushangaza zilizomo katika mafuta ya nazi lazima ujuwe kuwa mojawapo ni hili la kukufanya usizeeke mapema.
Viuajivijasumu vilivyomo kwenye mafuta ya nazi hufanya kazi mhimu katika kupunguza vijidudu nyemelezi na matatizo mengine katika ini.
Kuzuia magonjwa ya ubongo ni faida nyingine ya mafuta ya nazi ambayo unapaswa kuijua.
Asidi mafuta zilizomo kwenye mafuta ya nazi hubadilishwa na kuwa âketonesâ ambazo huzuia kutokea tatizo la kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
Kupoteza kumbukumbu ni matokeo ya kuongezeka kwa kemikali ijulikanayo kwa kitaalamu kama âamyloid beta peptidesâ.
Kwenye mafuta ya nazi kuna kitu mhimu sana kijulikanacho kama âPhenolic compoundsâ ambacho hudhibiti ile kemikali ya âamyloid beta peptidesâ na hivyo kukuondolea tatizo la kupoteza kumbukumbu kirahisi zaidi.
Mafuta ya nazi yanaweza kukupunguzia hitaji lako la kutaka kula chakula kila mara kwa kuwa hufanya kazi ya kupunguza njaa ndani ya mwili.
Kutumia mafuta ya nazi kutakufanya ujisikie umeshiba kwa kipindi kirefu na kama matokeo yake kutakusaidia kupunguza kiasi cha nishati unaingiza ndani ya mwili wako kila siku.
Kuna uhusiano wa karibu kati ya mafuta safi kwa afya na kuwa na njaa ya wastani.
Tafiti mbalimbali Zimeonyesha kwamba Msongamano wa juu wa lipoprotini kolesto (high-density lipoproteins -HDL) unao uwezo wa kulinda moyo wako.
Hivyo mafuta ya nazi yanaweza kupunguza hatari kwako ya kupatwa na ugonjwa wa moyo moja ya kazi nyingine mhimu sana ya mafuta haya.
Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo âlauric acidâ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolesteroli/lehemu mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla.
Lauric acid huongeza uwepo wa kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalamu kama High Density Lipoprotein (HDL) huku ikiishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni mhimu kwa afya ya moyo kama anavyosema Lovisa Nilsson, mtaalamu wa lishe wa Lifesum.
Tafiti zimeendelea kuonyesha uhusiano uliopo kati ya matumizi ya mafuta ya nazi na kuimarika kwa mfumo mzuri wa mmengâenyo wa chakula.
Mafuta ya nazi yanapokuwa yamemengâenywa ndani ya mwili wako hutumika kama nguvu yako moja kwa moja.
Watu wanaotumia mara kwa mara mafuta ya nazi kwenye vyakula vyao kila siku wanakuwa na mfumo mzuri wa mmengâenyo wa chakula jambo ambalo ni mhimu katika kuchoma mafuta na nishati ndani ya mwili.
Mafuta ya nazi yanasaidia kuimarisha kinga yako ya mwili kwani mafuta ya nazi yana kiasi cha kutosha cha viuajivijasumu (antioxidants) dhidi ya vijidudu mbalimbali nyemelezi.
Tafiti zimeonyesha kwamba matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kuwa msaada mkubwa katika kuotesha na kukuza nywele.
Mafuta ya nazi ni mazuri kwa kupaka mdomoni. Vilevile kama una tatizo la midomo kukauka basi uwe unapakaa mafuta ya asili ya nazi kila mara.
Mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa wa kuungua na bado yakabaki na viinilishe vyake kama kawaida hata baada ya kuunguzwa au kuchomwa katika moto.
Mafuta ya nazi hubaki katika hali yake hata katika joto la kawaida tofauti na mafuta mengine.
Mafuta ya nazi ni mafuta mazuri kwa ajili ya masaji na kukupatia hali ya utulivu unaouhitaji kupitia masaji.
Pakaa mafuta ya nazi katika uke kulainisha. Faida nyingine unapopaka mafuta haya ukeni ni kutibu fangasi na bakteria tena bila madhara.
Mafuta ya nazi yanaweza kudhibiti dalili za ugonjwa wa aleji. Kila siku pakaa mafuta ya nazi ndani ya pua zako na hauta piga chafya unapokuwa karibu na kile kinachokuletea aleji/mzio.
Updated at: 2024-05-25 10:35:13 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Utakubaliana na mimi kwamba, kitendo cha mtu kubanwa na haja ndogo siyo kitu cha hiyari kwamba sasa mtu anaamua ngoja nibanwe na mkojo, hili ni jambo la asili na ni matokeo ya vyakula, matunda au vinywaji tunavyotumia. Kwa lugha nyingine tumekuwa tukiita kuwa ni wito wa asili au natureâs call.
Yawezekana mtu akawa katika mkutano, safarini, akawa katika mitandao ya kijamii anachati au popote pale akiwa anafanya jambo fulani na kutokana na jambo hilo, mtu akaendelea kujibana na kutokwenda kuyapunguza maji haya kutoka katika kibofu cha mkojo kwa kutoa kipaumbele kwa shughuli anayoifanya kuliko kusikiliza kwanza wito huu wa asili. Mambo haya tunayafanya sana, utasikia, mkojo umenibana kweli, ila ngoja nimalizie hii kazi halafu niende kujisaidia, hivi ndivyo watu wengi wanafanya.
Kutokana na vyakula na vinywaji tunavyotumia, kibofu cha mkojo huanza kujaa mkojo, mkojo unapofikia karibu mililita 50 mpaka 500 mtu huanza kuhisi hitaji la kwenda kukojoa. Kibofu cha mkojo kimezungukwa na vigunduzi asili (Receptors) vinavyopeleka taarifa katika Ubongo kuonyesha kuwa kibofu cha mkojo kimekaribia au kimejaa, baada ya taarifa hizi kufika katika ubongo, ubongo unatoa taarifa katika kibofu cha mkojo ili kiweze kushikilia mkojo huo kwa kuikaza misuli maalumu (Sphincters) mpaka hapo muda wa wewe kwenda kukojoa utakapofika.
Kibofu cha mkojo hufanya kazi kwa mfumo wa kujiendesha wenyewe yaani, automatic, kitendo cha mtu kupuuzia kwenda kukojoa husababisha Ubongo upate usumbufu wa taarifa za kujaa kwa kibofu cha mkojo na kwa kuwa Ubongo nao hutuma taarifa katika kibofu cha mkojo kusema kuwa mkojo uendelee kushikiliwa mpaka muda muafaka utakapofika, itafika kipindi uwezo wa ubongo kutoa taarifa hizi na pia uwezo wa vigunduzi asili (Receptors) vilivyoko katika kibofu cha mkojo kupoteza uwezo wake tena wa kufanya kazi hizo au uwezo kuwa mdogo. Matokeo yake ni mtu siku kweli anahitajika kuvumilia kidogo ili afike sehemu inayostahihi kujisaidia, lakini hawezi tena na kujikuta muda mdogo tuâŚ.mtu tayari kaloanisha nguo yake.
Mpenzi msomaji, mtu kujibana na kupuuzia kwenda kukojoa husababisha uwezo wa kibofu cha mkojo kujitawala (control) upotee. Pia kama uwezo wa neva zinazopeleka taarifa kwenye ubongo kuhusu mabadiliko/ujazo wa kibofu cha mkojo zitaharibika, basi misuli maalumu ya kubana mkojo (sphincter) itashindwa kuachia na matokeo yake mtu ataendelea kukaa na mkojo katika kibofu chake kwa muda mwingi zaidi kitu ambacho ni hatari kwa afya yake. Endapo mkojo huu utashindwa kutoka, utatengeneza mazalia ya bakteria na kukusababishia magonjwa ya kibofu (bladder infection). Magonjwa ya kibofu cha mkojo ni pamoja na U.T.I (Urinary Tract Infections), pia huweza kusababisha magonjwa ya figo na mchafuko wa damu, bacteremia.
Kuna hali huwa inajitokeza kwa baadhi ya watu, yawezekana alikuwa kabanwa na mkojo au alikuwa hajahisi kwenda kukojoa, ila akinywa maji au akisikia sauti ya maji yanachuluzika mfano maji yakitoka bombani, basi atahisi kwenda kukojoa.
Mpenzi msomaji, ni vyema tukawa wasikivu pale mtu unapobanwa na mkojo, hii ni kwa ajili ya afya ya kibofu chako cha mkojo lakini pia ni kwa ajili ya afya yako kwa ujumla. Kama unalo tatizo, usisite kuonana na wataalamu wa afya.
Updated at: 2024-05-25 10:35:33 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Juisi hii ni nzuri sana katika kutibu shinikizo la juu la damu.
Lakini inaweza pia kutumika kutibu shinikizo la chini la damu hasa ikiwa hili shinikizo la chini la damu limesababishwa na upungufu wa maji mwilini (dehydration).
Kutibu shinikizo la chini la damu unaweza kuchanganya juisi ya limau na chumvi kidogo na sukari au unaweza kutumia maji maji ya miwa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:55 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya mhimu zaidi mwilini kama madini ya zinki, kopa, maginizia, manganizi na chuma, mbegu za maboga ni tamu na zinaweza kutafunwa nyakati zozote na mahali popote hasa kwa wapenda kutafuna-tafuna kama mimi. Tafiti mbalimbali zimethibitisha pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida nyingi kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10 yafuatayo:
1. UGONJWA WA MOYO:
Kiasi kingi cha madini ya magnesium katika mbegu za maboga yanazifanya mbegu hizi kuwa mhimu sana kwa watu wenye magonjwa mbalimabli ya moyo. Madini ya magnesium ni mhimu kwa ajili ya kuimarisha msukumo wa damu kwenye moyo na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hatimaye kutibu na kuzuia magonjwa ya moyo. Mbegu hizi pia zina mafuta mengine mhimu zaidi kwa watu wenye ugonjwa wa moyo yenye OMEGA 3.
2. HUIMARISHA KINGA YA MWILI:
Mbegu za maboga zimebarikiwa kuwa na kiasi cha kutosha cha madini ya zinki (zinc). Kazi kubwa ya madini ya zink ni kuimarisha kinga ya mwili. Upungufu wa madini ya zink unaweza kupelekea matatizo kadhaa mwilini ikiwemo kuzaa watoto njiti, kuishiwa nguvu za kiume, matatizo ya homoni, chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo shuleni kimasomo na matatizo mengine kadhaa ya kimwili na kiakili.
3. HUONGEZA UWEZO WA MACHO KUONA
Mbegu za maboga zina Vitamini E, vitamini A, lutein, beta-carotene na zeaxanthin, vitu hivi vinavyopatikana katika mbegu za maboga ni mhimu kwa ajili ya nuru ya macho. Vitamini A na madini ya zinki ni mhimu kwa ajili ya uzalishaji wa âmelaninâ kimengâenya mhimu ambacho hutengenezwa kwa asili na miili yetu kwa ajili ya ulinzi wa afya ya macho.
4. KINGA YA KISUKARI
Kisukari ni moja ya ugonjwa unaoendelea kwa kasi kuwasumbua watu wengi kila pembe ya dunia. Mbegu za maboga zina vitu vitatu mhimu zaidi ambavyo ni âNicotinic acidâ, âTrigonellineâ na âD-chiro-inositolâ ambavyo husaidia kushusha damu sukari mwilini na kudhibiti kazi za insulini hivyo kuwa kinga na kuleta ahueni kubwa kwa watu wenye kisukari.
Kama unasumbuliwa na kisukari fanya mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku na unipe mrejesho hapa.
5. DAWA BORA YA USINGIZI
Mbegu hizi zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha homoni za usingizi. Kwenye mbegu za maboga kuna vimengâenya viwili mhimu zaidi ambavyo huhusika na usingizi na afya ya akili moja kwa moja navyo ni âL-tryptophanâ na âtryptophanâ. Gramu 100 tu za mbegu za maboga zina kiasi cha kutosha cha âtryptophanâ mpaka mg 576. Tryptophan ndiyo inahusika kuleta usingizi wenye utulivu pia huondoa msongo wa mawazo au stress mwilini. Kwa kuongezea mbegu za maboga zina kiasi kingi cha vitamini za kundi B. Muda mchache kabla ya kwenda kulala tafuna mbegu za maboga na utapata usingizi mtulivu kabisa mpaka asubuhi.
Kwahiyo kama una tatizo la kukosa usingizi jaribu kutumia mbegu za maboga na uniletee majibu hapa. Kumbuka kukosa usingizi mara nyingi huwa ni matokeo ya msongo wa mawazo na kama ulivyoona mbegu hizi zinaondoa pia stress! Kazi ni kwako ndugu.
6. DAWA BORA YA UVIMBE
Mbegu za maboga zinao uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini sambamba na uvimbe (inflammation). Kama ujuavyo sehemu kubwa ya vivimbe mwilini ni matokeo ya sumu kadhaa mwilini. Mbegu za maboga zitakuondolea uvimbe mwilini bila kukuachia madhara yoyote mabaya hapo baadaye. Kama unasumbuliwa na uvimbe popote jaribu kutumia mbegu za maboga na utuletee majibu. Mbegu za maboga pia ni dawa nzuri kwa aina nyingi za kansa mwilini.
7. HUONGEZA MAZIWA KWA MAMA ANAYENYONYESHA
Mbegu za maboga zina protini nyingi bora itokanayo na mimea isiyo na madhara kama ile ya kwenye wanyama. Pia zina OMEGA 3. Mama mjamzito hata unayenyonyesha tumia mbegu za maboga na utakuwa na uhakika wa kutoa maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto.
8. DAWA NZURI KWA MATATIZO YA TEZI DUME
Wataalamu wengi wa lishe wanapendekeza mbegu za maboga zitumike kwa wanaume wa rika zote yaani vijana hadi wazee kwani zimethibitika kuwa msaada mkubwa kwa afya ya tezi dume. Tafiti nyingi zinasema mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya Zinki madini ambayo ni mhimu SANA kwa afya ya tezi dume na husaidia uponyaji wa tatizo la tezi dume moja kuwa kubwa kuliko nyingine tatizo lijukanalo kwa kitaalamu kama âbenign prostatic hyperplasiaâ. Wanaume kazi ni kwenu.
9. ZINAONGEZA NGUVU ZA KIUME
Maajabu mengine ya mbegu za maboga ambayo ulikuwa huyajuwi bado.
Utaniuliza kivipi zinaondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume? Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo/stress kitu ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, lakini pia zinashusha lehemu (cholesterol), zinatibu kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk), zinashusha kisukari, zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya zaidi ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili. Bado huelewi? Zina madini ya chuma pia
Uzuri ni kuwa mbegu hizi hazina uchungu wowote, ni tamu kuzitafuna wakati wowote na mahali popote hata ukiwa ofisini unaweza kuwa nazo pembeni unatafuna huku unaendelea na kazi zako. Sambamba na hilo kama tulivyoona pale juu kwamba zinaongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha kwa upande wa wanaume zinaongeza pia uwingi wa mbegu za kiume (sperm count) ukitafuna mbegu za maboga siku mbili tu utaona ukimwaga bao linatoka la kutosha na zito kweli kweli basi ujuwe ni mbegu za maboga hizo.
10. ZINAONDOA PIA MSONGO WA MAWAZO (STRESS)
Msongo wa mawazo au stress kama mlivyozoea wengi ni tatizo linaloendelea kuwasumbua watu wengi miaka ya sasa. Mbaya zaidi wengi huwa hawaelewi nini madhara ya hizo stress wanazojipa. Yaani stress au msongo wa mawazo unaweza kukuletea magonjwa mengine mwilini zaidi ya 50, hivyo utaona ni jinsi gani ilivyo mhimu kwako kuweka chini stress zako na uendelee na maisha kwani kuendelea kuwa na stress ni hatari zaidi kwa afya yako.
Moja ya sababu kuu ya watu wengi kuwa na stress ni usawa usio sawa wa homoni zao (hormonal imbalance). Hivyo kama una tatizo la homoni kwenye mwili hebu weka mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku na hutakawia kuona tofauti. Mbegu za maboga zina kimengâenya mhimu sana kwa kutuliza mawazo kiitwacho âtryptophanâ na asidi amino zingine mhimu zinazohusika kutengenezwa kwa homoni nyingine ijulikanayo kama âserotoninâ. Kama ulikuwa hujuwi ni kuwa serotonin ni homoni inayohusika na kazi mhimu sana ya kurekebisha matendo ya kitabia na kutoa matokeo chanya kwa mambo yanayohusu usingizi, hali ya mawazo kwa ujumla na mambo yanayohusu njaa.
Mbegu za maboga ni msaada mkubwa kwa kina mama waliofikia ukomo wa siku zao na huondoa matatizo ya kiafya yatokanayo na kukoma kwa hedhi. Ni msaada kwa watu wenye saratani mbalimbali, huimarisha ukuaji na ustawi wa mifupa na meno, huondoa harufu mbaya ya kinywa na husaidia pia wenye tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara.
NAMNA NZURI YA KULA MBEGU ZA MABOGA:
Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi ingawa mimi napenda kuzikaanga kidogo kama dakika 15 hivi na huwa nazichanganya na maji ya chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa mbali ili kupata radha.
Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za maboga kwa siku ujazo wa kama nusu kikombe cha chai hivi kwa siku.