Njia za Kuzuia Mimba
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Date: April 16, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Njia za uzazi wa mpango zinatofautiana sana na zinaweza kugawanywa katika makundi mengi:
Vizuizi
(hizi huzuia mbegu kulifikia yai): Kuna mpira wa kiume (kondomu ya kiume), yaani mfuko wa mpira uliozibwa upande moja. Unavishwa kwenye uume uliosimama kabla ya kuingia ukeni. Pia kuna mpira wa kike (kondomu ya kike), yaani mpira unaoingizwa ukeni kabla ya kujamiiana.
Vidonge vya kuzuia mimba:
Lazima mwanamke anywe vidonge hivi kila siku hata kama hajamiiani.
Njia nyingine za kuzuia mimba kwa muda mrefu
. Njia hizi hazihitaji maandalizi maalum, ili kuzuia mimba, kabla ya kujamiiana na pia mwanamke hahitaji kukumbuka kufanya chochote kila siku. Kati ya njia hizi ni pamoja na sindano anazopewa mwanamke kila baada ya miezi mitatu. Pili, kuna vipandikizi, yaani vijiti vyembamba vya plastiki vinavyowekwa kwenye sehemu ya juu ya mkono wa mama kwa njia ya upasuaji mdogo. Vijiti vina kichocheo kinachozuia kupevuka kwa yai. Pia, kuna kitanzi ambacho ni kitu kidogo kilichotengenezwa kwa aina maalum ya plastiki. Kwa ufupi kinaitwa IUD. Huwekwa kwa utaalamu ndani ya mfuko wa uzazi. Sindano, vipandikizi na vitanzi lazima viwekwe na mtaalamu mwenye ujuzi kwenye kituo cha afya chenye vifaa vya kutosha. Kwa vile dawa za kuzuia mimba kwa muda mrefu zinaingiliana na mzunguko wa kawaida wa hedhi kwa kiasi, athari zake ni kubwa kuliko kutumia vidonge.
Kwa mwanaume na mwanamke kuna njia ya kudumu ya kufunga kizazi kwa njia ya upasuaji
. Kwa mwanaume mirija inayopitisha mbegu hukatwa na kufungwa, ili kuzuia mbegu zisitoke. Akijamiiana, anaweza kumwaga shahawa, lakini ndani ya shahawa hakuna mbegu. Kama mwanaume amefunga kizazi uume utadinda kama kawaida na kufikia mshindo atamwaga maji ya shahawa ambayo hayatakuwa na mbegu. Kwa mwanamke mirija ya kupitisha mayai hukatwa na kufungwa, ili kuzuia mayai kufika kwenye mfuko wa uzazi. Baada ya upasuaji huu, mama ataendelea na hedhi kama mwanzo, lakini yai halitaweza kukutana na mbegu za kiume tena.
Vilevile kuna njia nyingine mbalimbali ambazo hazina uhusiano na matumizi ya dawa au vizuizi vya mimba. Njia hizi hazina uhakika mkubwa wa kutopata mimba. Mara nyingine mama anatumia ishara mbalimbali, au tarehe kujua lini anaweza kupata mimba, ili kuepuka kujamiiana katika kipindi hicho. Kumwaga mbegu za kiume nje ya uke, au kutegemea kwamba mimba hazishiki wakati wa kunyonyesha ni njia nyingine za asili zinazotumiwa. Kumbuka kwamba njia hizi hutumika sana, lakini si njia salama sana za kuzuia mimba wala kuambukizwa na magonjwa ya zinaa.
Ni muhimu kukumbuka kwamba njia ya uzazi wa mpango inaweza kufaa kwa mtu huyu na isifae kwa mtu mwingine. Kwa hiyo, ni vizuri kila mtu aliyeamua kupanga uzazi apate ushauri kwenye kliniki kuhusu njia inayomfaa zaidi
Please log in or register to leave a comment or reply.
Related Posts
Je, ni lazima kufanya ngono kwa sababu ya marafiki au shinikizo za kisiasa? π€
Ndugu vij...
Read More
Ndiyo, hata akitoa uume nje ya uke kabla ya kumwaga mbegu anaweza akaambukizwa Virusi vya UKIMWI...
Read More
Ile ngozi ndani ya uke i inabakia kuwa nyembamba na laini sana, hata mwanamke akiwa bikira katika...
Read More
Ni kweli kwamba mara nyingi hali hii huwatokea wavulana na wanaume. Ndani ya uume kuna mishipa mingi...
Read More
Leo tutazungumzia kuhusu kwa nini watu wanapendelea kujaribu aina mbalimbali za ngono/kufanya map...
Read More
Hakuna mtu wa kulaumiwa, lakini i i inabidi kila mtu awajibike. Kila mtu i inambidi afanye lolote...
Read More
Je, ni muhimu kuzungumzia upendeleo wako wa ngono kabla ya kuingia katika uhusiano? Jibu ni ndio!...
Read More
Nchini Tanzania ni 7% ya watu wenye umri kati ya miaka 15-49 wana maambukizi ya Virusi vya UKIMWI...
Read More
Ugumba wa mwanaume ni hali ya mwanaume kushindwa kumpa mwanamke mimba. Kuna mambo mengi yanayowez...
Read More
Si kweli.
Pombe haiongezi damu, vitamini wala nguvu. Ukweli ni kwamba unywaji po...
Read More
Hakuna hata mmoja anayejua hasa kwa nini, na lini desturi
imeanza. Jamii inatoa maelezo tofa...
Read More
Jinsi ya Kupanga Tarehe ya Kipekee na Msichana Wako
Kupanga tarehe ya kipekee na msichana ...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!