Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 10:34:47 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wali wa hoho ni chakula maalum kinachotumika katika hafla au sherehe. Ni chakula chenye ladha nzuri na kina muonekano wa kuvutia kinapokuwa mezani tayari kwa kuliwa.
Mara nyingi huandaliwa kama zawadi katika harusi hususan kwa watu wa pwani. Kwa kuwa zawadi hiyo au maarufu kama kombe huwa kuna vyakula vingi, ikiwamo chakula hiki ambacho hufanya kombe kuwa na muonekano wa kupendeza.
Mbali na kuliwa kama kombe chakula hiki kinaweza kuandaliwa kama mlo wa usiku.
Mahitaji:
• Mchele ½ kg • Nyanya 3 • Mafuta ya kupika ¼ kikombe cha chai • Chumvi kiasi • Kitunguu swaumu kilichosagwa kijiko 1 cha mezani • Kitunguu maji kilichosagwa kijiko 1 cha mezani • Hoho 4 • Nyama ya kusaga ¼ • Tangawizi kijiko 1 cha chakula • Limao au ndimu kipande
Maadalizi:
• Chukua mchele uoshe vizuri kasha chuja maji • Chukua nyama ya kusaga na kamulia ndimu, weka chumvi na tangawizi, changanya vizuri na weka jikoni.iache ichemke hadi ikauke maji yote. • Chukua maji na kiasi cha robo tatu lita chemsha na weka pembeni • Chukua sufuria kavu yenye uwezo wa kupika kiasi cha kilo moja • Weka mafuta ya kupika kiasi cha vijiko vitatu na acha yapate moto • Weka vitunguu maji, menya nyanya na katakata halafu weeka katika sufuria hiyo. • Weka chumvi na kanga hadi vilainike kabisa • Baada ya kuiva weka vitunguu swaumu na baadaye mchele • Koroga hadi uchanganyike na weka nyama. Endelea kukoroga, baada ya hapo weka maji kiasi cha kuivisha mchele huo. Acha vichemke hadi vikaukie. • Palia mkaa juu yake au kama unatumia jiko la gesi au umeme weka kwenye oven hadi maji yakauke kabisa. • Baada ya hapo chukua hoho na kasha kata upande wa juu kama vifuniko. Kasha ondoa matunda ya ndani yake. Funika na kasha zipange kwenye sufuria yenye maji na chumvi na mafuta kidogo kiasi cha kijiko kimoja. Chemsha jikoni hadi ziive. • Baada ya kuiva, chukua hoho zako na kasha chota wali kw akutumia kijiko kasha jaza katika kila hoho na weka kwenye sahani tayari kwa kuliwa. • Unaweza kupamba na salad ukipenda.
Mapishi ya Muhogo Na Mbatata Za Nazi Kwa Nyama Ngombe
Updated at: 2024-05-25 10:37:34 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo - Mahitaji Ya Nyama
Nyama ya n’gombe ya mifupa - 3 lb
Tangawizi mbichi ilosagwa - 1 kijiko cha supu
Kitunguu thomu - 1 kijiko cha supu
Bizari ya pilau/jira/uzile (cumin) - 1 kijiko cha supu
Ndimu - 1
Kitunguu kilokatwakatwa (chopped) - 1 cha wastan
Pilipili mbichi - 3 Zilizosagwa
Chumvi - Kiasi
Vipimo - Muhogo Na Mbatata/Viazi
Muhogo menya na ukate vipande pande - 2
Mbatata/Viazi menya ukate vipande vikubwa kiasi - 5 kiasi
Tui la nazi zito - 1 gilasi
Nyanya ilokatwakatwa au kusagwa - 1
Kitunguu kilokatwakatwa (chopped) - 1 kiasi
Bizari ya mchuzi - kiasi
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha nyama kisha weka katika pressure cooker au sufuria. Tia viungo vyote vya nyama uchanganye vizuri, kisha ikorogekoroge mpaka maji yake yakaribie kukauka. Usifunike. Tia maji kiasi ya kuivisha nyama na kubakisha supu yake kiasi ya kuivisha muhogo na mbatata. Muda wa kuivisha nyama inategemea nyama yenyewe na kama unatumia pressure cooker ni takriban dakika 35-40. Ikiwa sufuria ya kawaida utakuwa unaikoroga. Mimina ndani ya supu, muhogo, mbatata, nyanya, kitunguu, bizari ya mchuzi, chumvi. Acha ichemke uive muhogo na viazi. Tia tui la nazi, changanya vizuri acha kwenye moto dakika chache tu. Epua ikiwa tayari. Tolea na achari.
Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga - 3 Vikombe vya chai
Siagi - 250 gms
Baking powder - 3 Vijiko vya chai
Mayai - 2
Chumvi - 1 kijiko cha chai
Maziwa - 1/2 Kikombe
Pilipili manga ya unga 1 Kijiko cha chai
MAANDALIZI
Katika bakuli la kusagia (blender) au mashine ya keki, tia siagi, chumvi na mayai, piga mpaka iwe kama malai (cream). Tia Unga, baking powder, pilipili manga. Tia maziwa. Kata usanifu (design) unayotaka na sokota au kunja kwa usanifu unaopenda. Pika (bake) katika moto wa 350º C – usiviache vikawa rangu ya udongo (brown) sana.
Updated at: 2024-05-25 10:37:45 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Pasta (2 na 1/2 vikombe vya chai) Uyoga (mashroom 2 vikombe vya chai) Cream (1 kikombe cha chai) Mafuta (vegetable oil) Kitunguu (onion 1) Chumvi Majani ya basil (dried basil leaves 1/2 kijiko cha chai)
Matayarisho
Chemsha maji ya kutosha kisha tia chumvi na mafuta kidogo katika hayo maji na baadae tia pasta na uzichemshe mpaka ziive kisha uzichuje maji na uziweka pembeni. Baada ya hapo weka mafuta kidogo katika sufuria kisha tia uyoga uliokatwa na uupike mpaka uive. Baada ya hapo tia majani ya basil, chumvi na cream kisha acha ichemke kisha weka vitunguu na upike kwa muda wa dakika 4 kisha malizia kwa kutia pasta. Zichanganye vizuri na mchanganyiko wote kisha zipike kwa muda wa dakika 5. Na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Unaweza kupika nyama ya kuku (chiken breast) iliyokatwa vipande vidogo vidogo kama saizi na shape ya pasta. Vizuri kuikaanga pembeni mpaka iwe brown na kuiva alafu kuimix kwenye chakula baada ya uyoga na vitunguu kuiva alafu unamix cream kumalizia mapishi.
Updated at: 2024-05-25 10:23:11 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Mchele - 3 vikombe
Nyama ya kusaga - 1 LB
Mchanganyiko wa Nafaka upendazo; maharagwe, njegere, mbaazi n.k 1 mug
Vitunguu maji kata vipande vipande - 3 vya kiasi
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi - 2 vijiko vya supu
Mafuta - ½ Kikombe
Mchanganyiko wa bizari (Garam Masala) - 2 vijiko vya chai
Vipande vya supu (Maggi cubes) - 3
Maji (inategemea mchele) - 5
Chumvi - Kiasi
MAPISHI
Osha mchele na roweka. Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitunguu mpaka viwe brown. Tia Thomu na tangawizi, kaanga kidogo. Weka nyama ya kusaga, chumvi na garam masala, endelea kukaanga mpaka nyama iwive. Mwaga maji yaliomo katika kopo la nafaka na utie nafaka pekee humo. Tia maji na vipande vya supu (Maggi cubes) huku unavivuruga, koroga kidogo. Tia mchele, koroga kidogo. Funika na pika kwa moto mdogo mpaka karibu na kukauka ukikorogoka kidogo. (kama unavyopika pilau ya kawaida) *Epua uipike katika moto wa oven 350-400 Deg kwa muda wa dakika 15. *Kama sufuria uliyotumia sio ya kupikia katika oven, mimina katika chombo chochote kinachotumika kwa oven kama bakuli la pyrex au treya za foil. Pakua katika sahani na iko tayari kuliwa.
Jinsi ya kutengeneza Rock-cakes Za Njugu Na Matunda Makavu
Updated at: 2024-05-25 10:23:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga - 4 Vikombe
Sukari -10 Ounce
Siagi - 10 Ounce
Mdalasini ya unga - 2 vijiko vya chai
Matunda makavu/njugu (kama lozi, Zabibu, maganda ya chungwa, Cherries na kadhalika - 4 ounce
Maziwa ya maji - 4 Vijiko vya supu
Maandalizi
Chukua siagi na sukari koroga na mixer mpaka iwe kama cream. Tia vanilla mdalasini, tia yai moja mix tena endelea kuongeza yai lingine mpaka umalize yote, changanya mpaka iwe laini kama sufi (fluffy) Tia unga na baking powder na dried fruits, changanya na mwiko. Chota mchanganyiko na kijiko cha soup weka kwenye treya ya kupikia tandaza na uma ili upate matundu juu ya biskuti. Pika (bake) kwenye oven lenye moto wa 375 F. kwa muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.
Updated at: 2024-05-25 10:37:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (self risen flour 2 vikombe vya chai) Hamira (yeast kijiko 1 cha chai) Sukari (sugar 2 vikombe vya chai) Hiliki (cardamon 1/4 ya kijiko cha chai) Maji kikombe1 na 1/2 Mafuta
Matayarisho
Changanya unga, hamira, maji na mafuta kijiko 1. Koroga vizuri mpaka upate uji mzito usiokuwa na madoge Baada ya hapo uache uumuke kisha zichome kalmati katika moto wa wastani. Baada ya hapo tia sukari, hiliki na maji 1/2 kikombe katika sufuria na ichemshe uku unakoroga mpaka iwe tayari.(ukitaka kujua kama iko tayari chovya mwiko kisha gusa na vidole utaona iko kama nta au gundi) Baada ya hapo tia kalmati na uzichange pamoja mpaka zikolee kisha zitoe na uziache mpaka zipoe tayari kwa kuliwa.