Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Jamaa anayependa kuwafanyia watu uhuni leo kapatikana na huyu mdada
Updated at: 2024-05-25 16:59:17 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mdada alienda super-market kununua kuku, bahati mbaya kwenye frij kulikuwa na kuku mmoja tu, muuzaji akamtoa akamuweka kwenye mzani, akaonekana ana kilo moja na robo.
Mdada akamuuliza muuzaji,’Huna mkubwa zaidi?’ Muuzaji akamchukua yule kuku na kujifanya kamrudisha kwenye friji, halafu akamtoa tena kwenye friji na kumrudisha kwenye mzani, safari hii akagandamiza mzani kwa gumba, kuku akaonekana ana kilo mbili. Mdada akasema ‘Duh afadhali huyu mkubwa kidogo, naomba unifungie nawachukua wote wawili’
Mamaaaaa muuzaji sijui atatoa wap kuku wa pili😂
😅😅😅😅😅Hapo ndipo utagundua kwa nini MUWA co TUNDA 🚶🏽🚶🏽
Huyu bwana leo kapatikana, Jamani nyodo nyingine mbaya
Baada ya kumaliza Degree yake ya sheria Bwana Rwegashora aliamua kurudi nyumbani Bukoba mjini na kufungua ofisi yake kwa ajili ya huduma kwa wateja.
Siku moja akiwa ndani ya ofisi yake alimuona mtanashati na mdada mmoja mrembo anakuja ofisini kwake akajua ni mteja anamletea kesi.
Ndipo akanyanyua mkoni wa wa simu ya TTCL na kuanza kuongea huku anajizunguusha kwenye kiti cha kuzunguuka.
Updated at: 2023-04-29 22:52:17 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Baada ya kumaliza Degree yake ya sheria Bwana Rwegashora aliamua kurudi nyumbani Bukoba mjini na kufungua ofisi yake kwa ajili ya huduma kwa wateja. Siku moja akiwa ndani ya ofisi yake alimuona mtanashati na mdada mmoja mrembo anakuja ofisini kwake akajua ni mteja anamletea kesi.
Ndipo akanyanyua mkoni wa wa simu ya TTCL na kuanza kuongea huku anajizunguusha kwenye kiti cha kuzunguuka. Wakati mdada alipokaribia Rwegashora alimkaribisha kwa ishara maana alijifanya yupo busy na kuongea na simu ya umuhimu. Wakati anaongea na simu akisikika akisema No, No, No….. Absolutely No. Wajuulishe hao lay person wa New York kua siwezi kushuhulika na kesi ambayo itanilipa chini ya 50 million. Mimi ni profesional lawyer and im crossing the border to sarve international community.
Aka pose kidogo na akanywa maji kisha akaendelea….. Naweza kuanza kukusanya primary evidence next weak but tell them watume kwanza ten million kwa kuanza… Hahahahaha you dont know my Account Mr Roger. Ok waambie watume kwenye Account ileile walionitumia million 100 last month…
Aka pose tena akameza fundo la maji na kurekebisha tai yake kisha akaendelea… Ok usisahau kumueleza muendesha mashtaka mkuu wa marekani kua nitakuja New York mwezi ujao maana nitapita kwanza Amsterdam kuwasilisha utetezi wa yule mteja wangu mholanzi kisha nitaenda Tokyo kulipia ile gari yangu niloagiza.
Wakati anaongea hayo yote yule mdada alikua ametulia na anamuangalia Bwana Rwegashora anavyojizunguusha kwenye kiti chake huku akiongea kwa tambo kwenye ile simu ya TTCL. Baada ya kumaliza kuongea na simu Bwana Rwegashora aliweka mkono wa simu yake ya TTCL chini kisha akamgeukia mdada mrembo.
Samahan sana kwa kukupotezea muda wako unajua tena kazi zetu zinaumiza kichwa sana kama unavyoona mwenyewe yaani niko busy sana ninapokea simu sana mpaka nimechoka na simu nyingi ni za wateja wa njee ya nchi.
Anyway nikusaidie nn? Mdada akajibu mimi ni mfanyakazi wa kampuni ya TTCL nimekuja kuunganisha line yako ya simu kwani haipo hewani tangu wiki iliyopita…!!!
Alichokisema mtoto baada ya kusikia baba na mama wakiongea mambo yao usiku
MUME: Mke wangu naomba nikubusu
MKE: Sitaki
MUME: Ntakununulia pete ya gold
MKE: Staki
Updated at: 2024-05-25 18:04:32 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MUME: Mke wangu naomba nikubusu
MKE: Sitaki
MUME: Ntakununulia pete ya gold
MKE: Staki
MUME: Ntakununulia gari
MKE: Sitaki….mtoto wao aliyekuwa kalala alisikia haya maneno ya mwisho
MTOTO: Baba basi nibusu mimi uninunulie baiskeli
BABA: Pumbafu lala huko mjinga mkubwa
Updated at: 2024-05-25 17:12:24 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
JAMAA: Baba Padri nimekuja kuungama PADRI: Haya JAMAA: Niliiba kamba PADRI: Kamba? JAMAA: Ndio, kamba lakini kule mwisho kulikuwa kumefungwa ng'ombe PADRI: Kwa hiyo uliiba ng'ombe? JAMAA: Kiukweli nilikuwa nina lengo la kuiba kamba, kwa bahati mbaya mwisho kulikuwa na ng'ombe PADRI: Mi naona mueleze Mungu direct, mi sikuelewi kabisaaa
Updated at: 2024-05-25 17:07:17 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jana usiku kuna Jirani yangu..kanitumia text "mambo vipi?"…halafu tunakaa nae mtaa mmoja nikaona nikimjibu ni uharibifu wa hela nikaenda kumgongea mlango saa 7 usiku. Alipofungua nikamjibu "shwari"halafu nikarudi nyumbani kulala zangu..
Binti: Niletee chipsi kuku, soseji, mayai manne ya kukaangwa pembeni, baga, piza, coke take away baridi, mkate wa moto kwenye ile bekari ya wapemba na maji ya kunywa ya kiimanjaro.
Jamaa:Umesahau viti, meza, masufuria, sahani na beseni na vijiko.
Baada ya kumkuta mwanamme mwingine chumbani kwake na mke wake cheki huyu anachokifanya
NAKUA(BABA) karudi kazini mwanae mdogo akamuwahi, DOGO: Baba usiingie ndani kina jini chumbani kwenu NAKUA: Hakuna kitu kama hicho DOGO: Kweli baba kuna jini liko kwenye kabati lenu la nguo….
Updated at: 2023-04-29 22:53:31 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
NAKUA(BABA) karudi kazini mwanae mdogo akamuwahi, DOGO: Baba usiingie ndani kina jini chumbani kwenu NAKUA: Hakuna kitu kama hicho DOGO: Kweli baba kuna jini liko kwenye kabati lenu la nguo….
NAKUA kaingia ndani kamkuta mkewe kalala kitandani kajifunika shuka gubigubi hadi kichwani. Kaenda kwenye kabati kufungua mlango , akamkuta rafiki yake wa miaka mingi yuko uchi ndani ya kabati NAKUA: Aise unajua we fala sana, we rafiki yangu miaka yote hiyo halafu unamtisha mwanangu eti wewe jini, hebu toka huko nenda kwenu kacheze michezo hiyo na mwanao.