Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 17:11:24 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna siku nilichalala kipesa nikaamua kuomba dem wangu aniazime 10,000/= akanipa. Baada ya siku mbili nikapata pesa zaidi ya laki nne hivi, nikaamua kumpa 100,000/= mpenzi wangu bila yeye kuniomba. Baada ya siku 3 akaja kuniambia:- "Bae, ile 10,000/- niliyokuazima mwenyewe amekuja kunidai, so kama unayo naomba unipe nimrudishie maana ananisumbua leo siku ya 3." SAA HIZI NIPO ZANGU SINGLE NATAFUTA DEM MWINGINE
Updated at: 2023-04-29 22:53:38 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Karibuni tuangalie aina hizi 10 za ndoa.
1. NDOA YA MKEKA
Inatokana na kufumaniwa na Binti wa watu. Ndoa hii huwa Haina mahari. Hii huvunjika mwaka mmoja tu,baada ya wanandoa kugundua hawakuwa wakipendana!
2. NDOA YA MIHEMKO (NYEGE)
Hufungwa na vijana wenye umri wa miaka kati mume18 mke 16.Huvunjika baada ya miaka 3 au 4 ya ndoa.
4. NDOA YA MAONYESHO
Wenye ndoa Hii hupenda kujionyesha barabarani.Ila ndani hazina utii.Hupigana kila wanaporudi kutoka kwenye mizunguko. Cha kushangaza huwa hazivunjiki lakini ndiyo ndoa zinazoongoza kwa kuchepuka!
5. NDOA YA UHAMISHO.
Hufungwa na watumishi wa vijijini na mjini. Ili wa kijijini ahamie mjini.Mahari utoa anaetaka kuhamia mjini. Hata kama mahari atatoa mume lakini hii ndiyo ndoa yenye ukakasi zaidi.Huvunjika mara tu wanapoanza kuishi wote mjini. Salama ya hii ndoa ni kuhama kutoka mjini kwenda kijijini.
6. NDOA YA MIMBA.
Hufungwa kwa sababu wanaoowana hawataki kuonekana makwao kuwa wamezaa nje. Au muolewaji alikuwa hampendi muoaji kwa dhati.Muoaji hutumia mimba kama mtego wa kuingia ndoani. Hii huvunjika mtoto akizaliwa na kufikisha mwaka 1.
7. NDOA YA MALI (UTAJIRI)
Muolewaji miaka 18 au 28 Muoaji 65 au 70.Ndoa hii pia huitwa ndoa ya babu na mjuukuu. Ndoa ya aina hii hudumu, kwasababu mwenye kauli ni mwenye mali. Asilimia kubwa ya waume wa ndoa hizi hulea watoto wasio wao.
8. NDOA YA KWASABABU.
Hufungwa ili mradi muoaji au muolewaji aonekane tu kwa jamii kuwa naye kaoa au kaolewa.Huwa hazina utii wala upendo dhati. Ndoa ya aina hii ikifikisha miaka 4 huwa hazivunjiki wahusika huishi kwa mazoea.
9. NDOA YA UPENDO.
Ndoa hizi ziliishia mwaka 1978 kabla ya vita vya kagera.Muoaji na muolewaji hawakuangalia vitu ila utu tu ambao uliwaunganisha na kutengeneza upendo wa kudumu. Hii ilidumu miaka yote.
10. NDOA KUCHUMA
Ndoa hii ufungwa ili mradi muoaji au muolewaji akapate kitu au vitu fulani kutoka kwa upande mmoja wapo. Hii hudumu miaka kadhaa kutegemea na malengo ya mhusika. Wengine husubiri mpaka mhusika afe,lkn hujikuta wanakufa wao kwanza. Kuwa mwangalifu!
Updated at: 2024-05-25 17:52:36 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
_Sheria inasema kila anaetembea na chombo cha moto barabarani sharti awe na leseni._ _Sasa hawa wauza kahawa mbona wanatembea na chombo cha moto lakini hawakamatwi π‘._ _Hizi sheria zinapendelea._ πππππππππππ
Cheki wanachokisema vichaa baada ya kuona ndege inapita angani
Updated at: 2024-05-25 18:01:13 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vichaa wawili walikuwa wamekaa sehemu ghafla ikapita ndege angani kichaa mmoja akasema ndege ile hitakua imembeba rais kichaa mwenzake akajibu hapana ile imebeba wazungu kama ingekuwa imembeba rais ungeona mapikipiki mbele
Alichokisema mtoto baada ya kusikia baba na mama wakiongea mambo yao usiku
MUME: Mke wangu naomba nikubusu
MKE: Sitaki
MUME: Ntakununulia pete ya gold
MKE: Staki
Updated at: 2024-05-25 18:04:32 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MUME: Mke wangu naomba nikubusu
MKE: Sitaki
MUME: Ntakununulia pete ya gold
MKE: Staki
MUME: Ntakununulia gari
MKE: Sitakiβ¦.mtoto wao aliyekuwa kalala alisikia haya maneno ya mwisho
MTOTO: Baba basi nibusu mimi uninunulie baiskeli
BABA: Pumbafu lala huko mjinga mkubwa
Updated at: 2024-05-25 17:17:50 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mzee moja alikuwa kila usiku anapita mbele ya bank anasimama,kisha anapiga honi,akitoka askari mlinzi,anaondoka.Hilo jambo likamkera sana askari mlinzi, askari akawa na mvizia yule mzee wa kichaga ,siku alipokuja tena akamkamata, akamuuliza kwa nini unakuja unapiga honi kisha unakimbia? Mzee akasema: Haki ya mungu babaangu , Nina pesa zangu ktk account hapa bank naogopa usilale usingizi ndo maana kila siku usiku napita kukuangalia kama umelala!! ππππππ