Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 15:36:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Usiku wa leo uwe ni wenye faraja kwako, utawaliwe na usingizi wa mahaba kwenye kope zako, naomba ujenge taswira yangu katika mawazo yako, Usisahau kuniota sweet wangu. USIKU MWEMA
Nitaenda mbali Zaidi ya maono yako
Safarini nitajenga hekalu la pendo letu
Nitapuliza filimbi kama ishara ya utambulisho wako
Updated at: 2024-05-25 15:37:54 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nitaenda mbali Zaidi ya maono yako Safarini nitajenga hekalu la pendo letu Nitapuliza filimbi kama ishara ya utambulisho wako Na mwanzo wa sherehe ya ndoa yetu
Mungu akupe umri wa mnazi uishi mingi miaka. Akupe thamani ya mnazi kila kitu chatumika. Kuanzia kuti lake mpaka kwenye kidaka. Kitale katikati yake ukila utaridhika.
Updated at: 2024-05-25 15:37:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mungu akupe umri wa mnazi uishi mingi miaka. Akupe thamani ya mnazi kila kitu chatumika. Kuanzia kuti lake mpaka kwenye kidaka. Kitale katikati yake ukila utaridhika. Matamu na maji yake hukata kiu haraka. Weupe watui lake lina ladha ukipika. Kupaka mafuta yake mwili hulainika. Na kwenye machicha yake kazi nying hufanyika. Hata na upepo wake uvumapo utacheka. Sikijui kitu chake kipi kisichotumika.usiku mwema
SMS ya kumsihi mpenzi wako akupende kabla hajachelewa
Updated at: 2024-05-25 15:27:16 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
ITAKUA" Kama "NDOTO" Pale "MOYO" Wangu Utakapozima Kama "MSHUMAA" Uliopulizwa Kwa Upepo. Utatamani Niamke Angalau Usikie "SAUTI" Yangu Lakini Utakuwa umesha chelewa, ''KILIO' 'HUZUNI' SIMANZI'' na "MAJONZI zitakuwa zimetanda ktk KUTA za MOYO wako MACHOZI Yatakutoka kila utakapo kumbuka ucheshi WANGU kwako na MOYO Utakuwa Mpweke kila utakapoiona namba YANGU Kwenye simu YAKO Utatamani uifute ila ROHO Itakuuma kwa KUWA Umenizoea Hivyo Jaribu Kufurahia Uwepo WANGU Kabla Sijatoweka Dunian Ata Chura Ujua Umuhim Wa Maji Pindi Yanapo Kauka Tuishi Kwa Aman Na Upendo Maish Ya Dunian Ni Mafupi
Updated at: 2024-05-25 15:36:18 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dah! Safari yetu ilikuwa ngumu kweli ila hatimaye tumefika japo ni usiku sana hebu tupige hodi tusije kabwa na vibaka hapa nje. Hodiiiiii, Hodiiiii, Tunaomba tufungulie Mlango,, sisi tunaitwa FURAHA, AMANI na UPENDO. Tumebeba HEKIMA, BUSARA na MAFANIKIO. Tulikuwa wengi HURUMA na UPOLE wanakuja nyuma. CHUKI na WIVU hawana nauli. TABU ni mahututi. SHIDA yuko jela. MATATIZO amepigwa shoti ya umeme. MIKOSI amefariki njiani. LAANA ameliwa na mamba. UVIVU ameungua na maji ya moto hajiwezi. Tutakuwa nawe daima maana tumefika kwa NEEMA . Mungu akulinde na mabaya yote katika dunia hii. ucku mwema.
Updated at: 2024-05-25 15:36:31 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Licha ya upole ulionao! Pia upendo wako ndio kishawishi cha kunifanya nikukumbuke siku zote. Jiulize! nina namba za watu wangapi ktk cmu yangu,na bado sijatamani kujua hali zao ila wewe! kwa kuwa, nakuthamini nakukujali, ndiyo maana nakutakia, SIKU NJEMA
SMS nzuri ya mapenzi ya kimahaba ya kutuma kwa mpenzi wako umpendaye
Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu.
Updated at: 2024-05-25 15:37:51 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu. Mawazoni ama ndotoni, Daima wewe hutawala, Kila asubuhi niamkapo, Nao usiku nilalapo, U chakula changu akilini, Nalo tulizo langu moyoni, Daima huuwaza upekee, Wewe uliojaaliwa, Na hivyo naihisi furaha, Daima wewe uwapo, Mawazoni mwangu.