Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/katoliki/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Jinsi ya kutibu tatizo la kukosa choo bila kutumia dawa

Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image

Kukosa choo ni tatizo kubwa katika jamii zetu japo huwa halionekani kama ni tatizo. Hata hivyo kuna vyakula ambavyo vinapatikana kwa urahisi na vinasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa njia rahisi kabisa.

Kwa kawaida mtu mwenye afya njema anatakiwa kwenda chooni angalau mara tatu kwa siku, lakini si ajabu kusikia mtu hajaenda chooni siku tatu na tunaona ni kawaida sana kwenda chooni mara moja kwa siku.

Tatizo la kukosa choo (Constipation) linatokana na chakula tunachokula kuchelewa kuunguzwa tumboni hivyo kuchukua muda mrefu katika mfumo wa usagaji.

Tatizo hili linasababishwa na mfumo wa chakula kukosa baadhi ya mahitaji ili kufanya kazi yake ya usagaji. Vitu hivi ni maji na vyakula vya fiba(Vyakula vyenye nyuzinyuzi) ambavyo ni muhimu sana kuharakisha zoezi la usagaji wa chakula tumboni.

Vifutavyo ndivyo vyakula ambavyo husaidia kutibu tatizo la kukosa choo.

Tende

Tende zikiwa kavu au kama juisi inasaidia kuondoa tatizo la kukosa choo. Tende zina fiba kwa wingi hivyo kusaidia zoezi la usagaji chakula tumboni. Pia Tende zina kemikali ya sorbitolโ€“aina ya sukari ambayo inatajwa kusaidia usagaji chakula.

Maji

Kunywa maji kwa wing kunasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa kuwa maji yanahochea usagaji wa chakula na kufanya choo kuwa laini. Fiba zinahitaji maji ili kufanya kazi ya kufagia uchafu tumboni na maji yanapokosekana hunyonya toka katika uchafu tumboni na kufanya choo kuwa kikavu na kusababisha ugumu wa kutoka.

Wataalamu wa afya wanashauri kunywa glasi 6 mpaka 8 za maji kila siku( Lita 1-2 kwa siku)

Kama kunywa maji ni ngumu kwako basi jaribu kuweka vipande vya matunda kama ndimu ,limao,tikiti maji na aina nyingine ya matunda.

Kahawa na Vinywaji Vingine vya Moto

Kahawa na vinywaji vingine vya moto husaidia kusukumwa kwa chakula tumboni na kupata choo.

Matumizi ya muda mrefu ya kahawa yanaweza pia yakaongezea tatizo. Kama unatumia kahawa kwa wingi unashauriwa kunywa maji mengi pia,vinginevyo itaongezea tatizo la kukosa choo

Ulaji wa Matunda au Saladi

Matunda yanasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa vile yana fiba kwa wingi. Lakini matunda yanasaidia kuongeza maji maji hasa matunda kama matikiti.

Pia ulaji wa matunda ni muhimu kuzingatia muda wa kula, ni vyema kula matunda saa moja au dakika 30 kabla au baada ya chakula. Kula matunda mara baada ya kula kama wengi wanavyofanya ni makosa na kunakukosesha faida zinazotarajiwa.

Ulaji wa Mboga za Majani

Mboga za majani kama ilivyo matunda ni chanzo kizuri cha faiba ambazo ni muhimu sana katika usagazi na usukumaji wa chakula.

Mchicha, Spinachi,karoti na mboga mboga nyingine ni muhimu kuwepo katika chakula cha kila siku.

Maharage na aina nyingine za kunde kunde pia zina fiba kwa wingi na zinasaidia kupunguza tatizo.

Mazoezi Husaidia Kutibu Tatizo la Kukosa Choo Pia:

Ukiachia vyakula,ufanyaji mazoezi au kazi zinazoshughulisha mwili zinazaidia kuzuia na kutibu tatizo la kukosa choo.

Kufanya mazoezi kila siku angalau kwa dakika 30 ni jambo linalowezekana kama utalipa muda na kuweka katika ratiba zako. Mazoezi rahisi kabisa ni kukimbia (jogging) na pia hushughulisha mwili mzima(Total Body Exercise).

Ukiachia kutibu tatizo la kukosa choo pia mazoezi yanasaidia kuzuia magonjwa mengine mengi kama presha na kisukari.

Kama unasumbuliwa na tatizo la kukosa choo au unamfahamu mtu mwenye shida hii basi mshilikishe na ajaribu kufuta maelekezo kama yalivyotolewa hapa ili kuweza kutibu tatizo la kukosa choo kwa kupangilia vyakula tu unavyokula kila siku.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

Alex musyoka (Guest) on September 24, 2023

<ul><li>Thanks </li></ul>

Related Posts

Vyakula 7 vya kuepuka kula ili uwe na afya nzuri

Vyakula 7 vya kuepuka kula ili uwe na afya nzuri

Inasemwa kuwa โ€œwewe ni kile unachokulaโ€ kwa kumaanisha kuwa mwonekano wetu na afya ya mwili n... Read More

Faida za kufanya Masaji kiafya

Faida za kufanya Masaji kiafya

Masaji uongeza kinga ya mwili

Masaji kushuka kwa homoni inayohusika na kupunguza maambuki... Read More

Mambo ya msingi kujua kuhusu ugonjwa wa ngiri

Mambo ya msingi kujua kuhusu ugonjwa wa ngiri

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinaz... Read More
Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia asali

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia asali

Asali hasa asali mbichi ya asili ni dawa nzuri sana ya kutibu chunusi. Asali ni antibiotiki ya as... Read More

Faida za ulaji wa Peasi

Faida za ulaji wa Peasi

Peasi ni tunda ambalo limekuwa halithaminiwi licha ya kuwa na faida lukuki katika mwili wa binada... Read More

Jinsi ya kuongeza kiasi cha utokaji wa maziwa kwa kina mama wanaonyonyesha na kwa afya ya mtoto

Jinsi ya kuongeza kiasi cha utokaji wa maziwa kwa kina mama wanaonyonyesha na kwa afya ya mtoto

Maziwa ni chakula kikuu cha mtoto punde anapozaliwa. Mama anahitaji kuwa na Maziwa ya kutosha ili... Read More

Umuhimu wa kupata chanjo

Umuhimu wa kupata chanjo

Siku zote sisi wanadamu huwa tunaambizana kuwa, kinga ni bora kuliko tiba, tukiwa na maana kwamba... Read More

Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya Dengu (Dengue fever)

Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya Dengu (Dengue fever)

Ugonjwa wa dengue ni tishio la ugonjwa hatari linaongezeka siku hadi siku. Dengue ni ugonjwa unao... Read More

Madhara ya kutumia dawa bila ushauri wa Dakitari

Madhara ya kutumia dawa bila ushauri wa Dakitari

Mara nyingi watu wanaugua maradhi mbalimbali, lakini wengi wao hawapendi kwenda hospitali kufanya... Read More

Sababu ya meno kubadilika rangi

Sababu ya meno kubadilika rangi

Wapo baadhi ya watu wanashindwa hata kuachia kicheko chenye bashasha hii ni kwa sababu meno yao y... Read More

Dondoo muhimu kwa Afya yako unapostuka usiku

Dondoo muhimu kwa Afya yako unapostuka usiku

Kumekuwepo na tatizo la vifo vya ghafla sana tena kwa watu ambao wana afya njema na hii inatokana... Read More

Ifahamu Saratani ya Tezi Dume, chanzo, Dalili, Uchunguzi na Tiba

Ifahamu Saratani ya Tezi Dume, chanzo, Dalili, Uchunguzi na Tiba

Tezi Dume ni nini?