Utukuzwe ee Bwana wangu Yesu Kristo./ Uliagua kifo chako./ Katika karamu ya mwisho ulitumia mkate wa kidunia/ ukafanya mwujiza na kuugeuza/ kuwa Mwili wako azizi./ Kwa mapendo ukawapa Mitume Mwili huo/ uwe kumbukumbu la mateso yako mastahivu./ Uliwaosha miguu kwa Mikono yako Mitakatifu./
Uheshimiwe, ee Bwana wangu Yesu Kristo./ Kwa kuhofu mateso na kifo,/ Mwili wako usio na kosa ulitoka jasho la damu/ badala ya maji./ Juu ya hayo uliutimiza wokovu wetu/ uliokuwa umetaka kuufanya./ Hivyo ulionyesha waziwazi mapendo yako/ uliyo nayo kwa wanadamu./
Utukuzwe, ee Bwana wangu Yesu Kristo./ Ulipelekwa kwa Kayafa,/ Wewe uliye Hakimu wa wote./ Ukaruhusu kwa unyenyekevu kutolewa kwa Pilato/ uhukumiwe naye./
Utukufu uwe nawe, Bwana wangu Yesu Kristo,/ kwa kuwa ulivumilia kuchekwa tena/ uliposimama huko,/ umevaa joho jekundu,/ umetiwa taji ya miiba mikali sana Kichwani,/ ukavumilia kwa saburi kubwa/ kutemewa mate katika Uso wako mzuri,/ kufumbwa Macho,/ na kupigwa mno na wajeuri/ ngumi na makofi Mashavuni na Shingoni./
Sifa iwe nawe, Bwana wangu Yesu Kristo,/ Kwa uvumilivu mkubwa ulikubali kufungwa nguzoni,/ kupigwa mijeledi kijeuri,/ kujaa damu na hivyo kusukumwa barazani kwa Pilato./ Ulionekana kama mwanakondoo asiye na kosa./
Heshima iwe nawe, Bwana wangu Yesu Kristo./ Umehukumiwa Mwili wako mzima/ Mtukufu wenye kutoka damu/ ufe msalabani./ Ulichukua msalaba kwa Mabega yako Matakatifu/ na kuumwa sana./ Kwa ghadhabu walikusukuma mbele/ mpaka mahali pa mateso,/ wakakunyangβanya nguo zako./ Hivyo ulikubali kupigiliwa msalabani./
Heshima ya milele upate Wewe,/ Bwana wangu Yesu Kristo./ Ulipokuwa katika taabu kubwa hii,/ ulimkazia Mama yako mstahivu/ Macho yako ya hisani na mapendo/ na unyenyekevu,/ ndiye Mama yako asiyekosa hata mara moja/ wala kukubali dhambi yeyote./ Ulimweka katika ulinzi mwaminifu/ wa Mfuasi wako ili kumtuliza./
Milele utukuzwe, ee Bwana wangu Yesu Kristo./ Ulipokuwa mwenyewe taabani,/ uliwapa wakosefu wote/ matumaini ya kuondolewa dhambi/ kwa kumwahidia mnyangβanyi aliyekuendea/ utukufu wa paradisi kwa huruma yako./
Sifa ya milele iwe nawe, Bwana wangu Yesu Kristo,/ kwa kila saa ulipovumilia uchungu/ na taabu kubwa mno msalabani kwa ajili yetu sisi wakosefu,/ maumivu makali sana/ yaliyotoka katika majeraha yako,/ yakapenya bila huruma Roho yako Takatifu./ Yakaingia kikatili katika Moyo wako Mtakatifu/ hata ukakatika,/ ukapumua Roho yako,/ ukainama Kichwa,/ ukaweka Roho yako mikononi mwa Mungu, Baba yako./ Na baada ya kufa uliacha nyuma Mwili baridi./
Utukuzwe, ee Bwana wangu Yesu Kristo,/ kwa Damu yako azizi na kwa kifo chako kitakatifu/ ulizifidia roho za watu,/ ukazitoa ugenini/ na kuzipeleka kwa hisani yako katika uzima wa milele./
Milele uheshimiwe, Wewe Bwana wangu Yesu Kristo./ Siku ya tatu ulifufuka katika wafu,/ ukajionyesha kwa wafuasi wako,/ ukapaa mbinguni/ mbele ya macho yao siku ya arobaini./
Shangilio na sifa ya milele upate Wewe, Bwana wangu Yesu Kristo,/ kwa kuwa umewapelekea wafuasi wako mioyoni mwao/ Roho Mtakatifu,/ ukawasha rohoni mwao mapendo makuu ya Mungu./
Pia, utukuzwe, usifiwe na kushangiliwa milele, Bwana wangu Yesu Kristo./ Umekaa katika ufalme wako wa mbinguni/ juu ya kiti cha enzi cha Umungu wako,/ ukaishi pamoja na Viungo vyako vyote Vitakatifu./ Na hivyo utakuja tena/ kuzihukumu roho za wazima na wafu wote./ Unaishi na kutawala/ pamoja na Baba na Roho Mtakatifu,/ milele. Amina.
(Na Mt. Birgita wa Sweden)
Irene Akoth (Guest) on February 26, 2019
ππ Nakusihi Mungu
Nancy Akumu (Guest) on May 29, 2018
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
Benjamin Kibicho (Guest) on March 11, 2018
ππ Mbarikiwe sana
Anna Mchome (Guest) on January 14, 2018
πππ Mungu akufunike na upendo
Elizabeth Malima (Guest) on November 29, 2017
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
Samson Mahiga (Guest) on November 12, 2017
ππβ€οΈ Nakuombea heri
Chris Okello (Guest) on September 26, 2017
πβ€οΈ Mungu akubariki
Victor Kimario (Guest) on September 2, 2017
πβ€οΈ Mungu ni mkombozi
Anna Malela (Guest) on July 14, 2017
Rehema zake hudumu milele
George Mallya (Guest) on July 6, 2017
πβ¨ Neema ya Mungu iwe nawe
Stephen Kikwete (Guest) on June 22, 2017
Mungu ni mwema, wakati wote!
Mary Sokoine (Guest) on March 15, 2017
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
Tabitha Okumu (Guest) on February 4, 2017
ππ Mungu akujalie amani
Patrick Akech (Guest) on November 5, 2016
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
Moses Kipkemboi (Guest) on November 5, 2016
Katika imani, yote yanawezekana
Moses Mwita (Guest) on November 1, 2016
ππ Asante kwa neema zako Mungu
Joseph Mallya (Guest) on October 15, 2016
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
Rose Amukowa (Guest) on May 10, 2016
πβ€οΈπ Bwana akujalie baraka
Patrick Akech (Guest) on March 19, 2016
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
Agnes Njeri (Guest) on February 25, 2016
ππβ¨ Neema yako ni ya kutosha
Moses Kipkemboi (Guest) on February 13, 2016
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
Joseph Njoroge (Guest) on January 16, 2016
ππ Mungu wetu asifiwe
Joyce Nkya (Guest) on January 14, 2016
πβ€οΈ Mungu ni mwaminifu